Kwanini Tanzania tusitengeneze mabomu yetu ya nuclear?

olesiteti Jr

Member
Jul 6, 2016
96
59
Tanzania tuna madini ya Uranium kwa wingi na wataalam wa nuclear physics kama Dr. Gharib Bilal kwanini tusianze kujenga makobora ya nuclear incase ikilipuka nuclear war na sisi tuweze kushambulia endapo tutachokozwa?
 
Mimi nafikiri tuanze kuimalisha kwanza sekta ya Afya ,Elimu ,Barabara na welfare za wahudumu mbalimbali halafu tufikirie mambo makubwa kama hayo.
 
Mko tayari kupeleka makusanyo kwenye utengenezaji huo?maanake kujenga reli kwa hela zetu za ndani watu wanahoji.
 
Tanzania tuna madini ya Uranium kwa wingi na wataalam wa nuclear physics Kama Dr. Gharib Bilal kwa nini tusianze kujenga makobora ya nuclear incase ikilipuka nuclear war na sisi tuweze kushambulia endapo tutachokozwa?

Wanaotumia nuklia si kwa mabomu tu, kuna upande mwingine mzuri wa kutoa nishati ya uhakika.
 
Nchi ambayo wanafunzi 300 wanatumia tundu moja la Choo na wanakwenda peku eti ndio ina ndoto za Kutengeneza "Nyukiria".
 
Tuna makomandoo wanapasuliwa matofali ya mchanga mwilini wanatosha. Nyuklia anasa
 
Mmmh kama hajatulipukia wenyewe. Na yatakua na impact gani kwa taifa kiuchumi tukishayatengeneza.
 
Dah hii kweli jamii forums, kila mtu anatoa hisia zake, ila umewasilisha hisia zako, mimi nawaza kwanini hatuwezi kukopi hata tecnolojia kutengeneza pikipiki, na baadae magari tukishaweza yauzwe kwa bei nafuu.
 
Tutaanzia wapi wakati hata ukitengeneza tu la petrol na kuweka kwenye chupa ya konyagi, wenye dunia yao wana kutia korokoroni fasta.
Tanzania tuna madini ya Uranium kwa wingi na wataalam wa nuclear physics Kama Dr. Gharib Bilal kwa nini tusianze kujenga makobora ya nuclear incase ikilipuka nuclear war na sisi tuweze kushambulia endapo tutachokozwa?
 
Jana FaizaFox aliandika, hebu tujaribu nkutumia google kabla hatujapost post zetu. tunaweza kupata majibu huko. Investment ya nuclear plant ni hadithi nyingine.
 
Back
Top Bottom