Kwanini Tanzania tunanyonyana sana?

Jicholamwewe

JF-Expert Member
Jan 2, 2021
307
348
Wazima nyote?

Nikienda moja kwa moja katika mada. Jamani kwanini watanzania tuna nyonyana sana? Hasa viongozi, tajiri anamnyonya mtu wa hali ya chini.

Juzi kati nilienda kufanya mishe Fulani katika kiwanda cha konyagi yani nikawa napewa habari na vijana wa pale ambao kwa pale nikama vibarua yani hawajaajiriwa lakni wengi wao wanamiaka zaidi ya mmoja lakini bado ni vibarua hawajapewa mkataba lkn wanafanya kazi sawa na wajiriwa pale na ukiangalia pesa wanayopokea ni ndogo sana ukilinganisha na kazi wanazofanya yani mfanyakazi anapewa kipaumbele sana katika haki kuliko kibarua.

Yani niliumia sana nilipopata taalifa hizo .kingine wanapewa pesa kwa wiki na pesa yao inakatwa NSSF lakini pesa yao haiingizwi katika account yao ya NSSF. Kuja kuchunguza niligundua viongozi wa pale wanakula chajuu ndo maana hawalifatilii sana jambo hill na ukizingatia ile ni international company.

Ningeomba serikali iingilie kati kuhusu unyonyaji huu maana rushwa imeenea sana .serikali fanyeni kazi yenu siyo kuchukua mapato tu na huko watu wanaumizwa na wanafaidika watu wachache tena kutegemea nguvu za wanyonge.
 
Ningekushauri ungesikiliza na upande wa management mkuu. Umetoa tuhuma na ukahukumu. Jipe nafasi chunguza na upande wa pili
 
Kwa sisi tuliofundishwa enzi hizo kuhusu Capitalism as a mode of Production, wala hatushangai kusikia hayo malalamiko.

Maana Mabepari kote duniani hupambana ili kutengeneza maximum profit kupitia huo ujira mdogo kwa wafanyakazi wao, kuzalisha kwa gharama ndogo na kuuza kwa bei juu, nk.

Hivyo kwa ufupi tu ni kwamba, katika mfumo wa ubepari;unyonyaji haukwepeki. Na usisahau Serikali nayo inapata kodi! Hivyo usitegemee msaada wowote ule wenye tija.
 
Hakuna tajiri duniani atakaekufanya uwe tajiri wala upate kipato kikubwa zaidi ya mishahara duni na kazi kubwa

Kila mmoja atakuambia hatupati faida kabisa
Ukitegemea tajiri asikukandamize, hilo sahau kabisa
 
Back
Top Bottom