Kwanini Tanzania inapata idadi ndogo ya watalii japo ina vivutio vingi?

Loxodona

JF-Expert Member
Apr 3, 2019
354
618
Nimeona kwenye taarifa mbalimbali kuwa Mbuga yetu ya Serengeti imetajwa kama kivutio Bora zaidi. Zaidi ya Mbuga hiyo, Tanzania imekuwa ikijizolea umaarufu mkubwa kwa kuwa na vivutio vingi na vizuri vya Utalii Afrika na Duniani Kwa Ujumla. Baadhi ya vivutio vinavyotajwa ni Ngorongoro Conservation Area, Mlima Kilimanjaro, Fukwe nzuri, Pori la Akiba la Selous n.k.

Pamoja na idadi kubwa ya vivutio Bora tulivyonavyo, nchi yetu imekuwa nyuma katika ukanda wa Afrika Mashariki kwa kupata watalii wengi.

Je nini kinakwamisha nchi yetu kupata watalii wengi pamoja na kuwa na vivutio lukuki vyenye sifa za kimataifa?? Kama nchi tunakwama wapi??

Hapa nitaainisha maeneo machache ambayo yanatukwamisha kwenye kupata idadi kubwa ya wageni.

1) Gharama kubwa za kutalii nchini Tanzania. Gharama hizi zinatokana na tozo mbalimbali ikiwemo gharama za malazi kwa mtalii. Ukiachilia mbali gharama zinazotozwa ili Kuingia ktk hifadhi zetu, mtalii analazimika kulipa fedha nyingi Sana kwenye mahoteli yetu yaliyopo Mbugani. Mfano Mhe. Rais alisema katika Pori la Akiba la Selous kuna lodge inatoza US$ 3000 Kwa usiku mmoja. Hii ni fedha nyingi Sana Kwa watalii walio wengi. Hapa nashauri uwekwe mkakati wa makusudi wa kuongeza idadi ya Vitanda katika Mbuga zetu ili kupunguza gharama za malazi kwenye mahoteli ya Mbugani.

2) Idadi ndogo ya Vitanda (mahoteli) katika Mbuga zetu. Kwa Ujumla wake, kuna idadi ndogo Sana ya Vitanda katika Mbuga zetu. Hali hii inapelekea bei ya malazi katika hoteli/lodges chache zilizopo Mbugani kuwa juu Sana Hali inayo-discourage watalii kutembelea kwenye Mbuga zetu.

Takwimu zinazonyesha kuna wakati Occupancy rate inashuka Hadi 47% Kwa mwaka. Kwamba pamoja na uchache wa vyumba vya kulala wageni katika Mbuga zetu, karibu nusu ya vyumba hivyo vinakosa wateja. Unaweza ukaangalia bei za vyumba katika lodges za Mbugani Kupitia Booking.com au mitandao mingine ndio utaelewa vizuri.

3) Mikakati Butu ya kupata watalii toka nje ya nchi. Pamoja na kutumia nguvu nyiiingi kutangaza vivutio vyetu nchi za Ulaya na America. Takwimu zilizopo zinaonesha, wageni wengi wanatoka nchi za Africa, then Ulaya na America. Kwa bahati mbaya, hakuna mkakati wa makusudi wa kulifikia soko hilo la Afrika. Ifahamike kwamba, mtalii sio lazma awe Mzungu. Hivyo kama tukijipanga vizuri, tunaweza pata watalii na fedha nyingi toka barani Africa kuliko kwingineko duniani. Mfano, bei za kulala katika mahoteli yetu ya Mbugani, ni prohibitive Kwa waafrika walio wengi, hali inayoathiri soko letu. Hivyo, tunaweza kuwa na bei maalum Kwa waafrika wanaokuja kutembelea kwenye Mbuga zetu.

4) Kuzorota Kwa Utalii waa Ndani. Pamoja na juhudi nyingi za kuhamasisha Utalii WA ndani, bado aina hii ya Utalii ipo Chini Sana ukilinganisha na nchi zinazotuzunguka. Zipo sababu nyingi zinazoathiri Utalii wa ndani nchini Tanzania, baadhi ya vitu vinavyoathiri Utalii wa ndani ni pamoja na Hali ya kiuchumi Kwa wananchi walio wengi, Tabia, na gharama za kutalii kuwa juu Sana. Pamoja na ukweli kwamba gharama za viingilio kwenye Mbuga zetu zipo Chini Sana Kwa wazawa, Ukweli ni kwamba, Gharama za kutalii hazihusishi tu gharama za viingilio. Hivyo, mkakati wa makusudi inabidi uandaliwe ili kupunguza gharama za kutalii Kwa watanzania.

5) Mapungufu ya Miundombinu ya kuhudumia watalii. Pamoja nanjitihada kubwa za kuvutia wageni kuja kutembelea Mbuga zetu au vivutio vyetu, ubora wa Miundombinu yetu bado ipo Chini Sana. Mfano ulitembelea Serengeti ukaenda kulala kwenye public camping sites utajionea Hali ilivyo. Mabanda ya kulia chakula ni duni na mengi yapo kama mabanda ya kufugia kuku. Tunahitaji kuboresha public camping sites zetu kwani ndio kimbilio la watalii wenye bajeti ndogo. Vile vile yapo maeneo ambayo Hadi leo hayana Miundombinu mahsusi Kwa watalii mfano Pande Game Reserve/Pori la Akiba la Pande lililopo Wilaya ya Kinondoni Dar Es Salaam. Sasa hata kama tutatumia mabilioni kutangaza vivutio vyetu Ulaya na Marekani, je itasaidia nn kama kwenye Mbuga hamna hata Choo? Watalii wakija watajisaidia wapi? Hivyo Kwa ujumla bado tuna mengi ya kufanya ili kuongeza idadi ya watalii katika nchi yetu na hifadhi zetu

Hitimisho: Sekta ya Utalii ni sekta ambayo ikitumika vizuri inaweza ikatuletea manufaa makubwa Sana kwa Taifa. Sekta hii inao uwezo mkubwa wa kutoa ajira Kwa watanzania wengi Sana na kuchangia Pato la Taifa kama itasimamiwa Vizuri. Rai yangu, Sekta hii itupiwe jicho zaidi kwani mchango wake bado haujajitoshereza.


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hilo ni kweli kabisa mkuu gharama kwa mzawa ni kubwa sana japo wanatudanganya na viingilio kidogo vyakula bei juu,malazi bei juu bado umlipe mtu anaeenda kuwatembeza kuna gharama tena zakulipia gari yako kuingiza mbugani yani ni tabu tupu
 
ushauri watumie mbinu ya kagame visit rwanda then unabadili tu visit tanzania kwenye timu yoyote EPL utaona wanavyojaa watalii hakuna anyetujua
 
Hilo ni kweli kabisa mkuu gharama kwa mzawa ni kubwa sana japo wanatudanganya na viingilio kidogo vyakula bei juu,malazi bei juu bado umlipe mtu anaeenda kuwatembeza kuna gharama tena zakulipia gari yako kuingiza mbugani yani ni tabu tupu
Kwa utalii wa ndani kuna gharama unaweza kuzipunguza, kama malazi ya hotel za mbugani, chakula cha bei mbaya, so gharama kubwa kwa mtanzania ni kukodi gari la kutembela mbugani, ambayo kwa half day ni kati ya laki 2 hadi 3 tu.

Niliwahi kwenda ngorongoro kwa kudrive mpaka karatu, nikalala hapo, kesho yake nikaingia ngorongoro asubuhi mpaka saa 7 hivi, nikarudi nikalala moshi, na keaho yake nikarudi dar, so ukijipanga, ukiwa na kati la laki 5 mpaka 8, kutegemea na mbuga unayotaka kwenda na mahali unayoishi, inawezekana

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hilo ni kweli kabisa mkuu gharama kwa mzawa ni kubwa sana japo wanatudanganya na viingilio kidogo vyakula bei juu,malazi bei juu bado umlipe mtu anaeenda kuwatembeza kuna gharama tena zakulipia gari yako kuingiza mbugani yani ni tabu tupu


watanzania tulipofikia kwa unafki hatuna wapinzani, tummeenda manyara tumelipa kiingilio 2000 tu, kama hio ni kubwa hama tu nchi maaana hamna unachosaidia hii nchi, baadhi ya skukuu hua ni bure kuingia

And yes vitu vingine ni bei juu, biashara za watu we ulitaka usafiri bure? Ule bure: kama unavoheshimu mshahara wako heshimu na biashara za watu
 
'Mhe. Rais alisema katika Pori la Akiba la Selous kuna lodge inatoza US$ 3000 Kwa usiku mmoja'

Kuna staa mmoja hivi wa kike wa Marekani alienda pale kenya,kuna lodge alilala hapo ambapo lodge hio ni maarufu kwa twiga yaani unaweza ukawa unakunywa chai twiga akaingiza kichwa hapo dirishani kwako ukamlisha msosi kwa mkono wako fresh kabisa.

Ila breakfast hapo ni $400(karibu mil.1 ya kwetu).

Sent using Jamii Forums mobile app
 
watanzania tulipofikia kwa unafki hatuna wapinzani, tummeenda manyara tumelipa kiingilio 2000 tu, kama hio ni kubwa hama tu nchi maaana hamna unachosaidia hii nchi, baadhi ya skukuu hua ni bure kuingia

And yes vitu vingine ni bei juu, biashara za watu we ulitaka usafiri bure? Ule bure: kama unavoheshimu mshahara wako heshimu na biashara za watu
Ndugu yangu nadhani hukufanya tathmini vizuri.

Unaposema tumeenda maana yake ulitoka sehem moja kwenda hapo Manyara. Je usafiri ulilipia Kiasi gani? Ulilala wapi? Hata kama ulitumia gari la ofisi na hela ya ofisi kulala lodge, jua walipa Kodi wamekugharamia hivyo usiseme ulienda Bure au ulilipa 2000 tu. Na pia faham sio watanzania wote wanaweza pelekwa Mbugani Kwa magari ya ofisi na kulipiwa na ofisi zao.

Nakushauri uangalie Utalii Kwa maana Pana zaidi kuliko kunarrow down your focus.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kutekana tekana na kuviziana giza kwa giza mtalii lazima ashituke maisha yake.
 
Jiulize wewe binafsi na familia yako lini mmefanya utalii - kama hamkufanya unataka nani afanye utalii. Anza wewe kisha wengine watafuata
 
Umewahi kujiuliza kwanini bidhaa kama Coca-Cola zinatangazwa kila siku ingawa zinapendwa?
Kwa sababu watu wanazaliwa kila siku
Sasa kama tukisema mlima Kilimanjaro na Serengeti zipo kwenye ramani kila mtu aone ni maajabu sana
Matangazo ya uhakika yanatakiwa na gharama lazima zitutoke
Kujitangaza kwenye ligi za Ulaya ni pesa ndefu lakini italipa kwa mda mfupi sana
Waziri namuona kutwa Twitter akiandika tu sijui huyo mtalii alieko Australia anaijua hiyo Twitter


Sent from my iPhone using Tapatalk
 
Halafu usisahau pia ni miongoni mwa nchi tatu Afrika zinazopata fedha nyingi kupitia utalii
 
Mkuu Loxodona, hakuna mahali umethibitisha kuwa tuna watalii wachache Tanzania. Nilitegemea uoneshe takwimu za watalii waliokuja Tanzania ukiwalinganisha na waliokwenda nchi kama tatu zingine hapa Africa kwa angalau miaka mitatu iliyopita.
 
Back
Top Bottom