Kwanini Tanzania inakwamisha EAC?

Kwanini Tanzania inakwamisha EAC?

Nyie mnaojua mambo hamieni Kenya mkaungane, sisi mtuache hapahapa kwa bibi. Ya nini kupata taabu ya kutuelewesha wakati Kenya ni free WaTz kwenda? Nyie nendeni mkaungane tutawakuta.

EAC si Kenya pekee!
 
Hii jumuiya mfu Faida zake ni kiduchu sana ukilinganisha na hasara lukuki.
Misingi ya kujiunga na jumuiya hii ni ya kizezeta na haijaweka kukuza MAENDELEO ya mwananchi wa kawaida wa nchi wanachama.
Huu na mipango mingi ya VIONGOZI wa kiafrika ndio kiini cha mabalaa na majanga katika baraka letu, UFISADI, uchu wa madaraka, ubinafsi na RUSHWA ndio Misingi ya kuanzishwa kwa jumuiya ya Afrika mashariki na watanzania wamelipotezea hilo litaasisi la kikabila kabla halijakomaa.
KUSHIRIKIANA SIO MPAKA MUUNGANE , KUJUANA MWISHO MIPAKANI, KILA MMOJA A BAKI KWAO
 
La, mie naona Wahenga walikuwa sawa: "Umoja ni nguvu, utengano ni udhaifu"
 
La, mie naona Wahenga walikuwa sawa: "Umoja ni nguvu, utengano ni udhaifu"
NI kweli tupu neno la wahenga, tushirikiane pale inapibidi lakini kuungana HAPANA,tulijaribu awali tukaishia njiani hakuna sababu ya Kurudisha tena NO.
 
NI kweli tupu neno la wahenga, tushirikiane pale inapibidi lakini kuungana HAPANA,tulijaribu awali tukaishia njiani hakuna sababu ya Kurudisha tena NO.

Sentebe, umeoa wewe? Kama ume, utajua "mavi ya kale hayanuki" na...."yaliyopita si ndwele (ugonjwa) tugange yajayo."
Halafu, mara nyingi watu wenye mawazo kama yako huwa hawaja interact na Mkenya kama mtu binfsi au hata pengine kumwona. Ni mawazo ya kujumuisha (generalization) yanayochochewa na wivu na chuki za kisiasa na...to be frank, a sense of inferiority tuliyonayo Watanzania!
Zaidi, hii siyo thread juu ya Ukenya na Utanzania. Soma kichwa cha habari.
 
Heri nusu shari kuliko shari kamili, wahenga walinena , ukishaumwa na NYOKA basi hata unyasi utaogopa, hivyo watanzania tulishagongwa na NYOKA kwenye jumuiya iliyokufa sasa msitulaumu kwa kuwa na tahadhari, NI RAHISI SANA KWA MLAKUNDE(KENYA NA UGANDA) KUSAHAU ILA SISI WATUPA MAGANDA (TANZANIA) HATUWEZI SAHAU TULIVYOSALITIWA.
TUSHIRIKIANE lakini muungano HAPANA
 
La hasha! Siyo nchi zote zinahitajia Tanzania. Hivi ndivyo tunavyodanganywa. Kweli, huenda nchi kama Kenya inatuhitajia kama soko tu, lakini haina maana kama hatufungulii hawatapata masoko mengine. Kenya pengine inafanya business kubwa zaidi na South Sudan na Ethiopia kuliko Tanzania. Hivyo usidanganywe kuwa Tanzania ni muhimu mno kwa Kenya kiasi isipokuwepo Kenya itakufa. Haya ni mawazo ya watu wasio safiri na wanaolishwa daily dish of propaganda.
Pili, wasema hakuna faida kwa nchi ambazo hazikuweka vikwazo? Nenda Rwanda leo. Kitu cha kwanza utakachokishuhudia ni maendeleo makubwa ya kupatikana kwa bidhaa. Hilo limefanya bei zake zishuke. Ukiwa Rwada unaweza kupiga simu Kenya, Uganda kwa tarrif ile ile kama ambavyo ungekuwa Kenya. Hebu jaribu kupiga simu Tanzania kwenda Kenya uone gharama zake. Lakini faida kubwa ni ugurishaji wa ujuzi unakuja kwa kuingiliana na watu wenye experience mbali mbali.
Kwa vile Rwada imekubali "movement of people" watu wengi "wenye akili" kutoka Kenya, Uganda etc wanafanya kazi Rwanda, na hivyo kuongeza ufanisi wa nchi hiyo. Leo hii Wanyarwanda wanazungumza Kiingereza, Kiswahili na Kinyarwanda pengine more proficient kuliko sisi. Jambo hili si suala la lugha pekee. Hii inamaanisha mwekezaji atachagua Rwanda kuliko Tanzania kutokana na "human development" iliyoko Rwanda.
Umezungumzia rasilmali. Kuna "kutoelewa" kwa watu katika suala hili la rasilimali. Kuwa na "rasilimali" hakumaanishi nchi kuwa tajiri. Rasilimali yabakia kuwa rasilimali tu hadi utakapoweza kuigeuza kuwa 'mali". Ndiyo maana DRC ina rasilimali kuliko Tanzania au nchi yeyote Afrika. Jee, DRC ni tajiri kuliko Egypt ambayo ni jangwa tu? Ili kuifanya rasilimali kuwa "mali" unahitajia "critical mass" ya watu wenye "practical knowledge". Ili kupata idadi hiyo kubwa ya watu wa "caliber" hiyo, Tanzania itahitajia miaka 100-200 ijayo (tena pamoja na juhudi kubwa za kusudi). Njia fupi ni kuwaruhusu watu kama hawa waliofundishwa kwingine kuja na kuchangia maendeleo ya nchi. Hii ndiyo faida kuu kwa kweli itakayopatikana kutokana na muungano wa EAC. Nchi zote kuu duniani zilizoendelea, labda ukitoa China (na hii ni stori nyingine na ndefu), zimefanya hivi. Soma asili ya maendeleo ya Marekani na nchi za Magharibi, nani walichangia....utaona kulikuwa na "infusion" kubwa wakati fulani ya watu waliotoka kwingine.
Mi nadhani watu wengi humu wanaojadili masuala haya, hawajadili kwa "usomi" bali kwa hisia, jazba na matamshi ya viongozi! Changanya na akili zako. Na zaidi, fanya utafiti. Siku hizi kuna kitu kinaitwa Google!
Maandishi mengi umejaza pumba tupu. Eti kuongea kiingereza unaijua EAC wewe au unabwabwaja tu. Nenda kaulizie EAC human capital ya jumuiya inategemea watu wa kutoka wapi! !!.Mnaongea vitu msivyofanyia utafiti. Pale EAC think tankers zinatoka Tanzania. Kwa kuhakikisha NENDA EAC kafanye utafiti siyo kubwabwaja tuuu . EAC ni Tanzania bila Tanzania hakuna EAC. Wanatuhitaji kuliko wao tunavyowahitaji tulia wanyooshwe
 
Sipendi kuugeuza uzi huu kuwa ni wa kuzungumzia Kenya na Tanzania. Hayo siyo makusudio. Lakini kwa kutaka kukufahamisha tu na kuondoa ufahamu makosa wa Watanzania wengoi juu ya Kenya:
Uliwahi kufika Kenya wewe? Usingeuliza hilo. Watu wanaopata taabu Kenya ni wale ambao wana "deficit" ya elimu. Kwa sababu uchumi wa Kenya umepiga hatua kubwa, naturally, unahitaji watu walioelimika kuweza kupata manufaa. Hi ni kawaida kabisa. Kuna Watanzania chungu nzima wame-invest Kenya, katika stock exchange yao treasury bills au hata hisa za kawaida. Sasa kipi cha kuchukia? Angalia: ubepari (capitalism) kama system ya utawala, haiwezi kumchukia yeyote mwenye "capital" aidha ya akili au ya pesa. Ni system za kuchelewa-chelewa na kuangalia nyuma (atavistic ) ndio zina wivu kama huo!
unaandika ujinga..unasifia uchumi unaopendelea wasomi wachache na watu wenye mtaji kwenye jamii ambayo sehemu kubwa hawakwenda shule!?
 
HA
Maandishi mengi umejaza pumba tupu. Eti kuongea kiingereza unaijua EAC wewe au unabwabwaja tu. Nenda kaulizie EAC human capital ya jumuiya inategemea watu wa kutoka wapi! !!.Mnaongea vitu msivyofanyia utafiti. Pale EAC think tankers zinatoka Tanzania. Kwa kuhakikisha NENDA EAC kafanye utafiti siyo kubwabwaja tuuu . EAC ni Tanzania bila Tanzania hakuna EAC. Wanatuhitaji kuliko wao tunavyowahitaji tulia wanyooshwe

Hata mtoto hawezi ku reason namna hii. Watanzania watu wa ajabu sana. Wale wanaoesabika "wanajua" wamejaa majivuno na mikogo. Si ingekuwa vyema kuelezea tu unachoona kimekosewa?
Sentensi yako ya mwisho yaonesha ujinga na kiburi.
 
unaandika ujinga..unasifia uchumi unaopendelea wasomi wachache na watu wenye mtaji kwenye jamii ambayo sehemu kubwa hawakwenda shule!?

Statistics or you are writing rubbish.
 
Bado tunatofauti kubwa kimfumo, mfano umiliki wa ardhi ampapo Tz ni mali ya Rais na kwa wenzetu kila mtu na chake.

Ili kufikia muungano, tungeachia madaraka ya baadhi ya rasilimali ziwe chini ya states (sijapata kiswahili chake).

Ninamaanisha kwamba.
  • Tuwe na Federation of East Africa.
  • Kila nchi iwe state na iwe chini ya govenor.
  • Kila state iwe na bunge lake na mamlaka yake ya mambo ya ndani.
  • Kila state iwe na sera yake ya ardhi, elimu na makusanyo na matumizi.
East Africa
  • iwe ni serikali itakayo simamia mambo ya nje zaidi.
  • Ihusike na kusimamia elimu kwa level ya juu zaidi.
  • Bunge la East Africa liwe kwenye ratio ya wingi wa watu na ukubwa wa state. Kwa mimi naprefer zaidi ukubwa.
  • Pia tuondoe ile tabia ya Ukenya, Utanzania, Unyarwanda n.k.
  • Tuondoe tabia ya kupenda madaraka, tuheshimu katiba haswa katika ukomo wa muda wa kutawala.
Kwa mimi nitasupport kama hayo yatafanyika, ila sio kuungano na kisha kuja kuwa kama Tanganyika na Zanzibar.
 
Nimekuwa nikifuatia kwa karibu sana tabia ya Tanzania ya kukwamisha maendeleo ya Jumuiya ya Afrika Mashariki. Kuanzia kuzuia uhuru wa kugura (movement) kwa raia wa Jumuiya, hadi kulipisha ushuru bidhaa za nchi hizo; ingawaje yote mawili hayo yalizungumzwa na kuafikiwa kwa ndiyo na hapana.

Kwa kweli uhuru wa movement (kugura) kwa raia wa nchi za EAC ndiyo msingi mkubwa wa Jumuiya hii kufikia muungano kamili.

Nini hasa kinachoendelea kwa nchi hii ambayo mwanzishi wake alisifika kupigania Umoja wa Afrika, na alidiriki kutaka kuchelewesha uhuru wa Tanzania ili mradi nchi zote tatu ziungane?

Watawala wetu (nawaita watawala na wala siyo viongozi) wanawarubuni Watanzania eti kukataa mambo fulani ni kwa sababu ya kuchunga maslahi ya Watanzania. La hasha! Ukweli ni kuwa wanasiasa wetu wanaogopa kwamba endapo Jumuiya hii itasimama kama inavyopendekezwa, basi wataumbuka.

Kwa maana ule uwongo wanaowalisha Watanzania kila siku kwamba sisi tuko "huru sana" na tuna "amani na demokrasia sana", "hatuna ukabila" "tumeendelea kuliko..." nk utaonekana wazi ni mangati (mirage). Pindi Watanzania watakapoingiliana na kuwajua kikweli Wakenya, au Banyarwanda au hata Waganda wataona dhahiri kuwa wenzetu hawa wameendelea mno kifikra na kisiasa kuliko sisi.

Kutokana na elimu yao kubwa, hawatishwitishwi kama Watanzania. Hilo huenda likawageuza Watanzania na kuona wazi ukiukaji mkubwa wa haki zao za kibinadamu unaofanywa na Watawala na vyombo vyao...polisi na wakuu wa kisiasa, na huenda wakataka uhuru kama walionao wenzao.

Kwa mfano, wakati Tanzania mtu mmoja tu (rais) anaweza kuzuia matangazo mubashara ya Bunge, jambo kama hilo haliwezekani Kenya au Uganda. Kwa maana nyingine, taasisi (institutions) za Kenya, Uganda na hata Rwanda zimeendelea zaidi kuliko za Tanzania.
HII HASA NDIYO SABABU WAJANJA HAWA WANAKWAMISHA MUUNGANO KAMILI WA EAC.

Na ndiyo maana watawala hawa hupendelea zaidi SADCC, kwa vile shirikisho hili ni butu, halina ndani yake mechanism ya kuweza kuwabadilisha Watanzania kifikra.

Labda useme kenya, uganda n rwanda nchi gan inaendeshwa na mtu mmoja kutoka bunge ,military had mahakama!! Hizo nazo nchi au n mashamba ya pk n m7?

Ss ndo nchi
 
Wewe ni mTanzania?

Hata kama wewe ni mTanzania, basi una walakini, pengine ndio uraia wa kununua.

Unasikia 'propaganda' halafu na wewe unazirukia bila hata kujiridhisha ukweli ni upi? Umeangalia takwimu zinazoonyesha kiasi cha watu wa Afrika Mashariki walioingia katika kila nchi mwanachama wa jumuia hiyo unayo zungumzia hapa?

Wewe utakuwa ni mtu toka Kenya, kwa sababu huko ndiko kwenye kiwanda cha kuilalamikia Tanzania kila mara kwa kila jambo, huku wenyewe ndio wakiwa vinara wa kutofuata wanayolalamikia.

Lakini hili linajulikana sababu zake.mmekuwa na hofu kubwa sana juu ya Tanzania jinsi inavyoinukia na kuchukua nafasi yake kwenye ukanda huu. Elewa kwamba malalamiko yenu hayatazuia chochote, Tanzania itaendelea kusonga mbele, mtake msitake. Hamuwezi kuzuia chochote.
 
Ajabu sana process ya kufikiria kwako. Yaani kutojiunga ndiyo kutaifanya Tanzania iwe na viwanda? Miaka zaidi ya 60 ya Uhuru hamkujiunga popote kwa nini hamkuleta viwanda wakati huo?
Angalia bara Ulaya. Si wote wana/walikuwa na maendeleo sawa. Wakati Ureno na Spain zajiunga na EEC mwaka 1986 zilikuwa nchi mkia barani Ulaya. Angalia hii leo. Hivyo hivyo nchi mpya kujiunga kama Hungary, Bulgaria zote zinaelekea kuimarika zaidi. Yaani waona suluhisho la matatizo na kuzorota kwa Tanzania ni kujichimbia kwenye shimo? Twashindwa na Rwanda kijinchi kimeanza juzi juzi hapa, leo hii kina watu wanaojiamini, wasioogopaogopa mwingine kuliko jinchi jikubwa la Tanzania? Huu Ujamaa umewazubaisha sana Watanzania. Kila mtu ataka alelewe na kubembelezwa kuwa "usiogope huko nje nitakukinga" Hatutafika.
Bahati mbaya, viongozi wako pia wanafikiria kama wewe!
Nilijua wewe ni boya, na wala siyo raia wa hapa.

Korea Kusini nao wako kwenye umoja gani? Japan ilijiunga na umoja gani kabla haijapata maendeleo. Kuendelea kwa ujerumani kulisubiri awe kwenye hiyo EEC?

Bure Kabisa.
 
Sasa si uhamie huko Kenya na Uganda ili ukaungane nao huko badala ya kutuletea ujinga na mawazo ya kitoto hapa. Kama unadhani Kenya wameendelea ebu nenda huko Karamoja kwa wakaramajong ukaone!
Unataka tuungane kesho, una haraka ya kwenda wapi? Hatupendi ujinga sisi.
 
Back
Top Bottom