baada ya chanzo hufuata kitendo......
jumuia ya africa mashariki iliuwawa na aliye iuwa anajulikana labda tuanzie huko.......
malengo na muundo wa SADCC na EAC ni tofauti.
EAC sio jumuia ya kwanza kuanzishwa wala si ya mwisho na kuna jumuia kubwa km EU waingereza wamejitoa je kisa wakiwemo 'watatishwa tishwa"?
kagame,nkurunziza,magufuli,kenyatta,museveni wote wana kasoro na mazuri yao,ndo maana wananchi waliamua kuwapa uongozi.
kuna miungano mingi km senegambia ,USSR nk ambayo imeshakufa labda tujifunze,pia hata wa tanganyika na znz una kasoro zake ila kwa hili tanzania tumejaribu na tunajua faida za muungano kuliko wote kwenye EAC.
km nchi tuna haki na wajibu wa kuamua tuyatakayo kwa gharama yeyote,
huwezi ukakataa unga wangu kwa kigezo kulinda viwanda vya wananchi wako,ila unanafasi ya mahindi je lengo lako ni lipi?unanipenda kwa dhati wote tufikie uchumi wa kuchakata mazao au nibakie mzalishaji wa malighafi?
hata km tutakuwa na jumuia uhuru wa maamuzi ya ndani utabaki wa mwanachama husika.
kwa kuwa walowezi na washirika wao wengi wako kwako unataka nisichukue kodi wakiingiza bidhaa kwangu lengo lako ni lipi? ulipo amua kukubali EPA uliamua km nchi na mm ninapokataa naamua km nchi.
mwisho ndoa ni hiyari sio lazima,pia ndoa ina kuvumiliana na ina mipaka yake.