Kwanini Tanzania inakwamisha EAC?

Kwanini Tanzania inakwamisha EAC?

Well said, na ukiangalia Nchi zote wanachama wa EAC yenye neema ya Rasilimali asilia nyingi ni Tanzania wote wanangalia namna ya kutupiga tu, ukizingatia bado Hatuna Sheria na taratibu madhubuti ya kulinda rasilimali zetu ni bora tusiwe vimbele mbele, turekebishe na kuimarisha kwanza mifumo ya ndani. Muungano sio wakutegemea sana na kujiachia kijinga siku ukivunjika unaweza jikuta unaingiza taifa shimoni

La hasha! Siyo nchi zote zinahitajia Tanzania. Hivi ndivyo tunavyodanganywa. Kweli, huenda nchi kama Kenya inatuhitajia kama soko tu, lakini haina maana kama hatufungulii hawatapata masoko mengine. Kenya pengine inafanya business kubwa zaidi na South Sudan na Ethiopia kuliko Tanzania. Hivyo usidanganywe kuwa Tanzania ni muhimu mno kwa Kenya kiasi isipokuwepo Kenya itakufa. Haya ni mawazo ya watu wasio safiri na wanaolishwa daily dish of propaganda.
Pili, wasema hakuna faida kwa nchi ambazo hazikuweka vikwazo? Nenda Rwanda leo. Kitu cha kwanza utakachokishuhudia ni maendeleo makubwa ya kupatikana kwa bidhaa. Hilo limefanya bei zake zishuke. Ukiwa Rwada unaweza kupiga simu Kenya, Uganda kwa tarrif ile ile kama ambavyo ungekuwa Kenya. Hebu jaribu kupiga simu Tanzania kwenda Kenya uone gharama zake. Lakini faida kubwa ni ugurishaji wa ujuzi unakuja kwa kuingiliana na watu wenye experience mbali mbali.
Kwa vile Rwada imekubali "movement of people" watu wengi "wenye akili" kutoka Kenya, Uganda etc wanafanya kazi Rwanda, na hivyo kuongeza ufanisi wa nchi hiyo. Leo hii Wanyarwanda wanazungumza Kiingereza, Kiswahili na Kinyarwanda pengine more proficient kuliko sisi. Jambo hili si suala la lugha pekee. Hii inamaanisha mwekezaji atachagua Rwanda kuliko Tanzania kutokana na "human development" iliyoko Rwanda.
Umezungumzia rasilmali. Kuna "kutoelewa" kwa watu katika suala hili la rasilimali. Kuwa na "rasilimali" hakumaanishi nchi kuwa tajiri. Rasilimali yabakia kuwa rasilimali tu hadi utakapoweza kuigeuza kuwa 'mali". Ndiyo maana DRC ina rasilimali kuliko Tanzania au nchi yeyote Afrika. Jee, DRC ni tajiri kuliko Egypt ambayo ni jangwa tu? Ili kuifanya rasilimali kuwa "mali" unahitajia "critical mass" ya watu wenye "practical knowledge". Ili kupata idadi hiyo kubwa ya watu wa "caliber" hiyo, Tanzania itahitajia miaka 100-200 ijayo (tena pamoja na juhudi kubwa za kusudi). Njia fupi ni kuwaruhusu watu kama hawa waliofundishwa kwingine kuja na kuchangia maendeleo ya nchi. Hii ndiyo faida kuu kwa kweli itakayopatikana kutokana na muungano wa EAC. Nchi zote kuu duniani zilizoendelea, labda ukitoa China (na hii ni stori nyingine na ndefu), zimefanya hivi. Soma asili ya maendeleo ya Marekani na nchi za Magharibi, nani walichangia....utaona kulikuwa na "infusion" kubwa wakati fulani ya watu waliotoka kwingine.
Mi nadhani watu wengi humu wanaojadili masuala haya, hawajadili kwa "usomi" bali kwa hisia, jazba na matamshi ya viongozi! Changanya na akili zako. Na zaidi, fanya utafiti. Siku hizi kuna kitu kinaitwa Google!
 
Nimekuwa nikifuatia kwa karibu sana tabia ya Tanzania ya kukwamisha maendeleo ya Jumuiya ya Afrika Mashariki. Kuanzia kuzuia uhuru wa kugura (movement) kwa raia wa Jumuiya, hadi kulipisha ushuru bidhaa za nchi hizo; ingawaje yote mawili hayo yalizungumzwa na kuafikiwa kwa ndiyo na hapana.

Kwa kweli uhuru wa movement (kugura) kwa raia wa nchi za EAC ndiyo msingi mkubwa wa Jumuiya hii kufikia muungano kamili.

Nini hasa kinachoendelea kwa nchi hii ambayo mwanzishi wake alisifika kupigania Umoja wa Afrika, na alidiriki kutaka kuchelewesha uhuru wa Tanzania ili mradi nchi zote tatu ziungane?

Watawala wetu (nawaita watawala na wala siyo viongozi) wanawarubuni Watanzania eti kukataa mambo fulani ni kwa sababu ya kuchunga maslahi ya Watanzania. La hasha! Ukweli ni kuwa wanasiasa wetu wanaogopa kwamba endapo Jumuiya hii itasimama kama inavyopendekezwa, basi wataumbuka.

Kwa maana ule uwongo wanaowalisha Watanzania kila siku kwamba sisi tuko "huru sana" na tuna "amani na demokrasia sana", "hatuna ukabila" "tumeendelea kuliko..." nk utaonekana wazi ni mangati (mirage). Pindi Watanzania watakapoingiliana na kuwajua kikweli Wakenya, au Banyarwanda au hata Waganda wataona dhahiri kuwa wenzetu hawa wameendelea mno kifikra na kisiasa kuliko sisi.

Kutokana na elimu yao kubwa, hawatishwitishwi kama Watanzania. Hilo huenda likawageuza Watanzania na kuona wazi ukiukaji mkubwa wa haki zao za kibinadamu unaofanywa na Watawala na vyombo vyao...polisi na wakuu wa kisiasa, na huenda wakataka uhuru kama walionao wenzao.

Kwa mfano, wakati Tanzania mtu mmoja tu (rais) anaweza kuzuia matangazo mubashara ya Bunge, jambo kama hilo haliwezekani Kenya au Uganda. Kwa maana nyingine, taasisi (institutions) za Kenya, Uganda na hata Rwanda zimeendelea zaidi kuliko za Tanzania.
HII HASA NDIYO SABABU WAJANJA HAWA WANAKWAMISHA MUUNGANO KAMILI WA EAC.

Na ndiyo maana watawala hawa hupendelea zaidi SADCC, kwa vile shirikisho hili ni butu, halina ndani yake mechanism ya kuweza kuwabadilisha Watanzania kifikra.
Acha bhla-bhla! na kuuliza mambo ambayo mwenyewe ungeweza kuyajibu. JF ni sehemu ya wenye reasoning na kama hujui, uliza tukusaidie kufikiri. EAC had never been effective institution tangu iundwe upya. Hakuna inegration, kuna competion, ndo maana unaona Kenya inatishiana na Uganda kwa ajili ya kakisiwa ka wavuvi, Burundi inatishiana na Rwanda, wachache wanaunda CoW, Tanzania na Kenya wanashindania Bomba la mafuta, nk. Jiulize kwa nini ni rahisi CRDB kuwa na tawi KIgali, lakini ni tatizo kuwa na tawi Nairobi. Wakati huo huo KCB ina matawi TZ. kwa nini unataka Tz iwe serious na jumuiya ya aina hiyo? Au TZ tufanye unafiki?

Ni wapi ktk karne hii kuna regional integration yenye kwenda sawa? Rudi Africa uitafute integration ya aina hiyo kama ipo. Kama hakuna, kwa nini upoteze muda.
 
"EAC had never been (an) effective institution since...." Kwa nini? Nadhani moja ya sababu ni Tanzania.
Hayo matatizo uliyoyataja si sababu kabisa ya kutokuwa na EAC ya muungano. Umesikia sehemu iitwayo Gibraltar? Hadi leo Uingereza ina mgogoro mkubwa na Spain juu ya eneo hili, kiasi cha kutaka kupigana. Uingereza na Spain zote ni EU. Ninachotaka kusema ni kuwa, Muungano utasaidia kwa kiasi kikubwa kutatua haya kuliko kutokuwa nao. Kama huamini, ngoja muungano na Zanzibar ufe, uone aina gani ya migogoro itakayozuka!
Kuhusu CRDB kukubaliwa Kigali na si Kenya.... kwanza ungeelezea sababu. Inawezekana ni sababu za kiidara zaidi na siyo kiushindani. Kama Kenya ina sheria kuwa yeyote anayetaka kufungua benki lazima awe na capital ya dola 200 m kwa mfano, na CRDB ikashindwa, huwezi kulaumu ushindani hapo. Lete hoja za kimantiki na siyo kuchukua mfano mmoja ambao yaelekea hata wewe hujui sababu yake, na kufanya ni moja ya sababu kwa nini Tanzania ikwamishe EAC.
 
Nimekuwa nikifuatia kwa karibu sana tabia ya Tanzania ya kukwamisha maendeleo ya Jumuiya ya Afrika Mashariki. Kuanzia kuzuia uhuru wa kugura (movement) kwa raia wa Jumuiya, hadi kulipisha ushuru bidhaa za nchi hizo; ingawaje yote mawili hayo yalizungumzwa na kuafikiwa kwa ndiyo na hapana.

Kwa kweli uhuru wa movement (kugura) kwa raia wa nchi za EAC ndiyo msingi mkubwa wa Jumuiya hii kufikia muungano kamili.

Nini hasa kinachoendelea kwa nchi hii ambayo mwanzishi wake alisifika kupigania Umoja wa Afrika, na alidiriki kutaka kuchelewesha uhuru wa Tanzania ili mradi nchi zote tatu ziungane?

Watawala wetu (nawaita watawala na wala siyo viongozi) wanawarubuni Watanzania eti kukataa mambo fulani ni kwa sababu ya kuchunga maslahi ya Watanzania. La hasha! Ukweli ni kuwa wanasiasa wetu wanaogopa kwamba endapo Jumuiya hii itasimama kama inavyopendekezwa, basi wataumbuka.

Kwa maana ule uwongo wanaowalisha Watanzania kila siku kwamba sisi tuko "huru sana" na tuna "amani na demokrasia sana", "hatuna ukabila" "tumeendelea kuliko..." nk utaonekana wazi ni mangati (mirage). Pindi Watanzania watakapoingiliana na kuwajua kikweli Wakenya, au Banyarwanda au hata Waganda wataona dhahiri kuwa wenzetu hawa wameendelea mno kifikra na kisiasa kuliko sisi.

Kutokana na elimu yao kubwa, hawatishwitishwi kama Watanzania. Hilo huenda likawageuza Watanzania na kuona wazi ukiukaji mkubwa wa haki zao za kibinadamu unaofanywa na Watawala na vyombo vyao...polisi na wakuu wa kisiasa, na huenda wakataka uhuru kama walionao wenzao.

Kwa mfano, wakati Tanzania mtu mmoja tu (rais) anaweza kuzuia matangazo mubashara ya Bunge, jambo kama hilo haliwezekani Kenya au Uganda. Kwa maana nyingine, taasisi (institutions) za Kenya, Uganda na hata Rwanda zimeendelea zaidi kuliko za Tanzania.
HII HASA NDIYO SABABU WAJANJA HAWA WANAKWAMISHA MUUNGANO KAMILI WA EAC.

Na ndiyo maana watawala hawa hupendelea zaidi SADCC, kwa vile shirikisho hili ni butu, halina ndani yake mechanism ya kuweza kuwabadilisha Watanzania kifikra.
Who wants political federation?
Nani anataka muungano kamili na mafisadi na wauaji? Tufanye biashara tu na tuwe na muungano wa kiuchumi basi kama wa nchi za Ulaya EEC. Kisiasa hatuivi.
 
Tatizo watanzania hatujui kutumia fulsa, na hiyo ni weakness yetu kubwa. Let us learn to think like Kenyans, that there is an opportunity in every situation. Kama tunajua wao wanatuhitaji zaidi kuliko tunavyowahitaji, kwa nini tusitumie hiyo advantage ku-demand maslahi zaidi kwenye EAC?
unaweza kupata fursa Kenya wewe!?..au umeamua kuharisha tu hapa..huwezi kushirikiana na watu wenye haiba ya uhayawani
 
"EAC had never been (an) effective institution since...." Kwa nini? Nadhani moja ya sababu ni Tanzania.
Hayo matatizo uliyoyataja si sababu kabisa ya kutokuwa na EAC ya muungano. Umesikia sehemu iitwayo Gibraltar? Hadi leo Uingereza ina mgogoro mkubwa na Spain juu ya eneo hili, kiasi cha kutaka kupigana. Uingereza na Spain zote ni EU. Ninachotaka kusema ni kuwa, Muungano utasaidia kwa kiasi kikubwa kutatua haya kuliko kutokuwa nao. Kama huamini, ngoja muungano na Zanzibar ufe, uone aina gani ya migogoro itakayozuka!
Kuhusu CRDB kukubaliwa Kigali na si Kenya.... kwanza ungeelezea sababu. Inawezekana ni sababu za kiidara zaidi na siyo kiushindani. Kama Kenya ina sheria kuwa yeyote anayetaka kufungua benki lazima awe na capital ya dola 200 m kwa mfano, na CRDB ikashindwa, huwezi kulaumu ushindani hapo. Lete hoja za kimantiki na siyo kuchukua mfano mmoja ambao yaelekea hata wewe hujui sababu yake, na kufanya ni moja ya sababu kwa nini Tanzania ikwamishe EAC.
Short and clear hamia Kenya!
 
Boss, tuliambiwa TZ tumekwamisha na wao wanaanzisha kiitwacho CoW. Wako wapi? Ikaanzishwa visa ya pamoja kwa manufaa ya utalii wa wahusika, manufaa yako wapi?
Nasema unahangaika kufanya analysis wakati sababu ni moja tu. Kuna members ambao wako mashindanoni na hawaihitaji TZ kama mwanachama, bali kama soko la kufanikisha kwao. Wewe unahangaika na mambo rundo yaliyoko kwenye nadhalia tu.

Uko Kenya au TZ? Nini kilifanya Kenya kufukuza wa-TZ wasipeleke abiria JK airport?
 
unaweza kupata fursa Kenya wewe!?..au umeamua kuharisha tu hapa..huwezi kushirikiana na watu wenye haiba ya uhayawani
FYI, kuna watanzania wengi tu wanaofanya biashara na shuguli nyingine Kenya.
PS, hukunielewa, nilichosema ni kwamba kama nchi nyingine wanatuhitaji zaidi, Kwa nini tusitumie kuhitajika kwetu katika kuweka masharti ambayo yatatunufaisha kwenye huo umoja? Au hata Hilo hatuwezi?
 
You hit it! Nachukia watu wanaolalamika juu ya Kenya kutufanya punda wa kupanda. Kwa nini nasi hatutumii mbinu za kuwafanya wao pia? Au hatuna akili?
Kenya ni taifa na kama mataifa yote duniani yanajali maslahi yao. Ujinga ni wetu tusiojua namna ya kupata maslahi yenu katika misingi ya mashindano. Tusiwaze hata siku moja kama Kenya itakua vinginevyo. Hivi hivi ndivyo inavyoamiliana na Sudan, Rwanda, Uganda etc. katika kuendeleza maslahi yao. Hakuna uadui kwa sababu tu ni Tanzania!
Acheni ujinga na wivu wa.....
Kenya kuna Watanzania kwa maelfu wanaofanya shughuli zao za biashara kama kawaida. Suluhisho siyo kujichimbia ndani ya shimo, hilo ni suluhisho la wavivu wa kufikiria.
 
Tatizo kuna watu wanatamani kuishi ugenini kama kwao. Kupitia kivuli cha eac.
 
You are very backward minded. Kwa nini kuishi ugenini liwe tatizo. Ujinga wa mtu mweusi, atakubali Mchina aishi TZ kuliko Mkenya!
 
FYI, kuna watanzania wengi tu wanaofanya biashara na shuguli nyingine Kenya.
PS, hukunielewa, nilichosema ni kwamba kama nchi nyingine wanatuhitaji zaidi, Kwa nini tusitumie kuhitajika kwetu katika kuweka masharti ambayo yatatunufaisha kwenye huo umoja? Au hata Hilo hatuwezi?
wanatuhitaji ili wafaidike..ndomana wanalilia ardhi iwe bwerere kwa kila MTU,huwezi kupata kazi Kenya lakini huku wanapata,sakata LA kampuni ya azam,wakiwa na shibe wanadai nafaka zetu zina sumu wakiwa na njaa wanazihitaji..hao sio watu
 
You hit it! Nachukia watu wanaolalamika juu ya Kenya kutufanya punda wa kupanda. Kwa nini nasi hatutumii mbinu za kuwafanya wao pia? Au hatuna akili?
Kenya ni taifa na kama mataifa yote duniani yanajali maslahi yao. Ujinga ni wetu tusiojua namna ya kupata maslahi yenu katika misingi ya mashindano. Tusiwaze hata siku moja kama Kenya itakua vinginevyo. Hivi hivi ndivyo inavyoamiliana na Sudan, Rwanda, Uganda etc. katika kuendeleza maslahi yao. Hakuna uadui kwa sababu tu ni Tanzania!
Acheni ujinga na wivu wa.....
Kenya kuna Watanzania kwa maelfu wanaofanya shughuli zao za biashara kama kawaida. Suluhisho siyo kujichimbia ndani ya shimo, hilo ni suluhisho la wavivu wa kufikiria.
Kenya kuna nini cha kuchukua!?
 
Nyie mnaojua mambo hamieni Kenya mkaungane, sisi mtuache hapahapa kwa bibi. Ya nini kupata taabu ya kutuelewesha wakati Kenya ni free WaTz kwenda? Nyie nendeni mkaungane tutawakuta.
 
Fanyeni yenu huko, kwani lazima kuungana. Mbona mnapenda kujipendekeza??
 
Kenya kuna nini cha kuchukua!?

Sipendi kuugeuza uzi huu kuwa ni wa kuzungumzia Kenya na Tanzania. Hayo siyo makusudio. Lakini kwa kutaka kukufahamisha tu na kuondoa ufahamu makosa wa Watanzania wengoi juu ya Kenya:
Uliwahi kufika Kenya wewe? Usingeuliza hilo. Watu wanaopata taabu Kenya ni wale ambao wana "deficit" ya elimu. Kwa sababu uchumi wa Kenya umepiga hatua kubwa, naturally, unahitaji watu walioelimika kuweza kupata manufaa. Hi ni kawaida kabisa. Kuna Watanzania chungu nzima wame-invest Kenya, katika stock exchange yao treasury bills au hata hisa za kawaida. Sasa kipi cha kuchukia? Angalia: ubepari (capitalism) kama system ya utawala, haiwezi kumchukia yeyote mwenye "capital" aidha ya akili au ya pesa. Ni system za kuchelewa-chelewa na kuangalia nyuma (atavistic ) ndio zina wivu kama huo!
 
Back
Top Bottom