Kwanini Tanzania inakwamisha EAC?

Kwanini Tanzania inakwamisha EAC?

Sijali

JF-Expert Member
Joined
Sep 30, 2010
Posts
2,700
Reaction score
1,853
Nimekuwa nikifuatia kwa karibu sana tabia ya Tanzania ya kukwamisha maendeleo ya Jumuiya ya Afrika Mashariki. Kuanzia kuzuia uhuru wa kugura (movement) kwa raia wa Jumuiya, hadi kulipisha ushuru bidhaa za nchi hizo; ingawaje yote mawili hayo yalizungumzwa na kuafikiwa kwa ndiyo na hapana.

Kwa kweli uhuru wa movement (kugura) kwa raia wa nchi za EAC ndiyo msingi mkubwa wa Jumuiya hii kufikia muungano kamili.

Nini hasa kinachoendelea kwa nchi hii ambayo mwanzishi wake alisifika kupigania Umoja wa Afrika, na alidiriki kutaka kuchelewesha uhuru wa Tanzania ili mradi nchi zote tatu ziungane?

Watawala wetu (nawaita watawala na wala siyo viongozi) wanawarubuni Watanzania eti kukataa mambo fulani ni kwa sababu ya kuchunga maslahi ya Watanzania. La hasha! Ukweli ni kuwa wanasiasa wetu wanaogopa kwamba endapo Jumuiya hii itasimama kama inavyopendekezwa, basi wataumbuka.

Kwa maana ule uwongo wanaowalisha Watanzania kila siku kwamba sisi tuko "huru sana" na tuna "amani na demokrasia sana", "hatuna ukabila" "tumeendelea kuliko..." nk utaonekana wazi ni mangati (mirage). Pindi Watanzania watakapoingiliana na kuwajua kikweli Wakenya, au Banyarwanda au hata Waganda wataona dhahiri kuwa wenzetu hawa wameendelea mno kifikra na kisiasa kuliko sisi.

Kutokana na elimu yao kubwa, hawatishwitishwi kama Watanzania. Hilo huenda likawageuza Watanzania na kuona wazi ukiukaji mkubwa wa haki zao za kibinadamu unaofanywa na Watawala na vyombo vyao...polisi na wakuu wa kisiasa, na huenda wakataka uhuru kama walionao wenzao.

Kwa mfano, wakati Tanzania mtu mmoja tu (rais) anaweza kuzuia matangazo mubashara ya Bunge, jambo kama hilo haliwezekani Kenya au Uganda. Kwa maana nyingine, taasisi (institutions) za Kenya, Uganda na hata Rwanda zimeendelea zaidi kuliko za Tanzania.
HII HASA NDIYO SABABU WAJANJA HAWA WANAKWAMISHA MUUNGANO KAMILI WA EAC.

Na ndiyo maana watawala hawa hupendelea zaidi SADCC, kwa vile shirikisho hili ni butu, halina ndani yake mechanism ya kuweza kuwabadilisha Watanzania kifikra.
 
Kwa tabia za akina Museveni et-al kutaka kuwa marais wa milele.
 
Hii nchi tuna asili ya unafiki,wivu,husuda na chuki bila ya sababu za msingi,nilimsikia JPM alivyochaguliwa kuwa mwenyekiti EAC hutuba yake ya kwanza na matendo yake ni mbingu na ardhi.
Umeelezea vizuri sana.
 
Nimekuwa nikifuatia kwa karibu sana tabia ya Tanzania ya kukwamisha maendeleo ya Jumuiya ya Afrika Mashariki. Kuanzia kuzuia uhuru wa kugura (movement) kwa raia wa Jumuiya, hadi kulipisha ushuru bidhaa za nchi hizo; ingawaje yote mawili hayo yalizungumzwa na kuafikiwa kwa ndiyo na hapana.

Kwa kweli uhuru wa movement (kugura) kwa raia wa nchi za EAC ndiyo msingi mkubwa wa Jumuiya hii kufikia muungano kamili.

Nini hasa kinachoendelea kwa nchi hii ambayo mwanzishi wake alisifika kupigania Umoja wa Afrika, na alidiriki kutaka kuchelewesha uhuru wa Tanzania ili mradi nchi zote tatu ziungane?

Watawala wetu (nawaita watawala na wala siyo viongozi) wanawarubuni Watanzania eti kukataa mambo fulani ni kwa sababu ya kuchunga maslahi ya Watanzania. La hasha! Ukweli ni kuwa wanasiasa wetu wanaogopa kwamba endapo Jumuiya hii itasimama kama inavyopendekezwa, basi wataumbuka.

Kwa maana ule uwongo wanaowalisha Watanzania kila siku kwamba sisi tuko "huru sana" na tuna "amani na demokrasia sana", "hatuna ukabila" "tumeendelea kuliko..." nk utaonekana wazi ni mangati (mirage). Pindi Watanzania watakapoingiliana na kuwajua kikweli Wakenya, au Banyarwanda au hata Waganda wataona dhahiri kuwa wenzetu hawa wameendelea mno kifikra na kisiasa kuliko sisi.

Kutokana na elimu yao kubwa, hawatishwitishwi kama Watanzania. Hilo huenda likawageuza Watanzania na kuona wazi ukiukaji mkubwa wa haki zao za kibinadamu unaofanywa na Watawala na vyombo vyao...polisi na wakuu wa kisiasa, na huenda wakataka uhuru kama walionao wenzao.

Kwa mfano, wakati Tanzania mtu mmoja tu (rais) anaweza kuzuia matangazo mubashara ya Bunge, jambo kama hilo haliwezekani Kenya au Uganda. Kwa maana nyingine, taasisi (institutions) za Kenya, Uganda na hata Rwanda zimeendelea zaidi kuliko za Tanzania.
HII HASA NDIYO SABABU WAJANJA HAWA WANAKWAMISHA MUUNGANO KAMILI WA EAC.

Na ndiyo maana watawala hawa hupendelea zaidi SADCC, kwa vile shirikisho hili ni butu, halina ndani yake mechanism ya kuweza kuwabadilisha Watanzania kifikra.
Wakati tunafundishwa Kuhusu hizi regional economic integration kuna vitu kama
Political will
Level of development
Ideology
Currency
Na mambo mengine kadha wa kadha so ili EAC iwepo na kila nchi ipate ku'benefit lazma ivo vitu hapo juu waviangalie. Unaweza kuta wana delay kwasababu there is no mutual benefits
 
baada ya chanzo hufuata kitendo......
jumuia ya africa mashariki iliuwawa na aliye iuwa anajulikana labda tuanzie huko.......
malengo na muundo wa SADCC na EAC ni tofauti.
EAC sio jumuia ya kwanza kuanzishwa wala si ya mwisho na kuna jumuia kubwa km EU waingereza wamejitoa je kisa wakiwemo 'watatishwa tishwa"?
kagame,nkurunziza,magufuli,kenyatta,museveni wote wana kasoro na mazuri yao,ndo maana wananchi waliamua kuwapa uongozi.
kuna miungano mingi km senegambia ,USSR nk ambayo imeshakufa labda tujifunze,pia hata wa tanganyika na znz una kasoro zake ila kwa hili tanzania tumejaribu na tunajua faida za muungano kuliko wote kwenye EAC.
km nchi tuna haki na wajibu wa kuamua tuyatakayo kwa gharama yeyote,
huwezi ukakataa unga wangu kwa kigezo kulinda viwanda vya wananchi wako,ila unanafasi ya mahindi je lengo lako ni lipi?unanipenda kwa dhati wote tufikie uchumi wa kuchakata mazao au nibakie mzalishaji wa malighafi?
hata km tutakuwa na jumuia uhuru wa maamuzi ya ndani utabaki wa mwanachama husika.
kwa kuwa walowezi na washirika wao wengi wako kwako unataka nisichukue kodi wakiingiza bidhaa kwangu lengo lako ni lipi? ulipo amua kukubali EPA uliamua km nchi na mm ninapokataa naamua km nchi.
mwisho ndoa ni hiyari sio lazima,pia ndoa ina kuvumiliana na ina mipaka yake.
 
Nimekuwa nikifuatia kwa karibu sana tabia ya Tanzania ya kukwamisha maendeleo ya Jumuiya ya Afrika Mashariki. Kuanzia kuzuia uhuru wa kugura (movement) kwa raia wa Jumuiya, hadi kulipisha ushuru bidhaa za nchi hizo; ingawaje yote mawili hayo yalizungumzwa na kuafikiwa kwa ndiyo na hapana.

Kwa kweli uhuru wa movement (kugura) kwa raia wa nchi za EAC ndiyo msingi mkubwa wa Jumuiya hii kufikia muungano kamili.

Nini hasa kinachoendelea kwa nchi hii ambayo mwanzishi wake alisifika kupigania Umoja wa Afrika, na alidiriki kutaka kuchelewesha uhuru wa Tanzania ili mradi nchi zote tatu ziungane?

Watawala wetu (nawaita watawala na wala siyo viongozi) wanawarubuni Watanzania eti kukataa mambo fulani ni kwa sababu ya kuchunga maslahi ya Watanzania. La hasha! Ukweli ni kuwa wanasiasa wetu wanaogopa kwamba endapo Jumuiya hii itasimama kama inavyopendekezwa, basi wataumbuka.

Kwa maana ule uwongo wanaowalisha Watanzania kila siku kwamba sisi tuko "huru sana" na tuna "amani na demokrasia sana", "hatuna ukabila" "tumeendelea kuliko..." nk utaonekana wazi ni mangati (mirage). Pindi Watanzania watakapoingiliana na kuwajua kikweli Wakenya, au Banyarwanda au hata Waganda wataona dhahiri kuwa wenzetu hawa wameendelea mno kifikra na kisiasa kuliko sisi.

Kutokana na elimu yao kubwa, hawatishwitishwi kama Watanzania. Hilo huenda likawageuza Watanzania na kuona wazi ukiukaji mkubwa wa haki zao za kibinadamu unaofanywa na Watawala na vyombo vyao...polisi na wakuu wa kisiasa, na huenda wakataka uhuru kama walionao wenzao.

Kwa mfano, wakati Tanzania mtu mmoja tu (rais) anaweza kuzuia matangazo mubashara ya Bunge, jambo kama hilo haliwezekani Kenya au Uganda. Kwa maana nyingine, taasisi (institutions) za Kenya, Uganda na hata Rwanda zimeendelea zaidi kuliko za Tanzania.
HII HASA NDIYO SABABU WAJANJA HAWA WANAKWAMISHA MUUNGANO KAMILI WA EAC.

Na ndiyo maana watawala hawa hupendelea zaidi SADCC, kwa vile shirikisho hili ni butu, halina ndani yake mechanism ya kuweza kuwabadilisha Watanzania kifikra.
Hadisi ndeeeefu, wanaokuelewa ni wale wanaokuelewa tu
 
Wakati tunafundishwa Kuhusu hizi regional economic integration kuna vitu kama
Political will
Level of development
Ideology
Currency
Na mambo mengine kadha wa kadha so ili EAC iwepo na kila nchi ipate ku'benefit lazma ivo vitu hapo juu waviangalie. Unaweza kuta wana delay kwasababu there is no mutual benefits

Unazijua sababu kwa nini tunakwamisha EAC? Si hizo ulizozitaja.
Political will: Ni dhahiri kwamba ni Tanzania ndiyo haina
Level of Development: Kwa kweli Muungano utasaidia development ya Tanzania. Kwanza utaepusha ku duplicate viwanda ambavyo tayari vipo kwingine na hivyo kutoa nafasi ya viwanda vipya na vya kisasa. Hapa tulipo bado tunafikiria viwanda vya kukoboa mpunga na kuondoa magamba ya samaki!
Ideology: Unajua ideology ya Tanzania hivi sasa wewe? Hatuna ideology yeyote, tunafuata upepo. Si Ujamaa si Ubepari nadhani ni "Utemi" zaidi!
Currency: Moja ya mapendekezo ni political union ambayo itapelekea kwenye currency union. Hii nayo mbaya? Kama unajoua economy?
 
Tuzungumzie upande wa level of development, Tanzania kwa upande wa viwanda bado sana ivyo basi tukijoin EAC lazma tuwe consumers sidhan kama tutakuwa na bidhaa za ku'export. Sasa na ww nakuulza kipi bora kujoin then Tz ikawa damping place au tukae ivi tu endelea ku'consume bidhaa za kwetu japo ziko local????
 
Mheshimiwa wanaokataa EAC wanakitu cha siri au wengine wanabaruzwa na mfumo wa siasa bila fikra fullstop
 
Tuzungumzie upande wa level of development, Tanzania kwa upande wa viwanda bado sana ivyo basi tukijoin EAC lazma tuwe consumers sidhan kama tutakuwa na bidhaa za ku'export. Sasa na ww nakuulza kipi bora kujoin then Tz ikawa damping place au tukae ivi tu endelea ku'consume bidhaa za kwetu japo ziko local????

Ajabu sana process ya kufikiria kwako. Yaani kutojiunga ndiyo kutaifanya Tanzania iwe na viwanda? Miaka zaidi ya 60 ya Uhuru hamkujiunga popote kwa nini hamkuleta viwanda wakati huo?
Angalia bara Ulaya. Si wote wana/walikuwa na maendeleo sawa. Wakati Ureno na Spain zajiunga na EEC mwaka 1986 zilikuwa nchi mkia barani Ulaya. Angalia hii leo. Hivyo hivyo nchi mpya kujiunga kama Hungary, Bulgaria zote zinaelekea kuimarika zaidi. Yaani waona suluhisho la matatizo na kuzorota kwa Tanzania ni kujichimbia kwenye shimo? Twashindwa na Rwanda kijinchi kimeanza juzi juzi hapa, leo hii kina watu wanaojiamini, wasioogopaogopa mwingine kuliko jinchi jikubwa la Tanzania? Huu Ujamaa umewazubaisha sana Watanzania. Kila mtu ataka alelewe na kubembelezwa kuwa "usiogope huko nje nitakukinga" Hatutafika.
Bahati mbaya, viongozi wako pia wanafikiria kama wewe!
 
Me nadhan suluhisho c mpka wa join EAC labda ni kuset policies ambazo zitaendana na kauli mbiu
Labda unikumbshe kipnd cha industrialization hko Uingereza walikuwa wamejiunga na economic integration yoyote??
Jibu kama ni hapana bac hata Tz inawezekana hata bila ya kujoin EAC
 
Back
Top Bottom