SoC03 Kwanini Tanzania haipigi hatua kimaendeleo kama inavyostahili

Stories of Change - 2023 Competition

shadrack lutengano

New Member
Jul 13, 2023
2
2
Maendeleo, ni hali ya kutoka hatua moja hadi hatua nyingine ambayo ni bora kuliko ile ya awali. Hatua hizo ni zinaweza kuwa ni za kiuchumi,kijamii au kisiasa.

Maendeleo hujumuisha maendeleo ya mtu mmoja mmoja,taasisi au nchi. ambapo maendeleo ya nchi au taasisi yanategemea sana maendeleo ya watu kwanza ikiwa ni maendeeo katika sekta ya elimu,afya na kichumi ya mtu binafsi ambapo kwa ujumla wa haya maendeleo ya mtu mmoja mmoja ndo chanzo cha haya mengine mfano maendeleo ya taasisi mbalimbali na nchi kwa ujumla.

Sasa nikwanini nchi yetu ya Tanzania haipigi hatua kama inavyostahiri licha yakua na vyanzo vingi vya maendeleo mfano malihasili nyingi mfano mbuga za Wanyama,madini,misitu n.k , sababu hizo nikama zifuatazo;

1).Mifumo ya elimu ya kikoloni ambayo haikidhi mahitaji ya Tanzania ya sasa, mifumo kielimu ambayo imechukua sura ya mfumo wa elimu ya kikoloni imekua changamoto kwani inaonekana kutokidhi mahitaji ya Tanzania ya sasa mfano elimu iliyokuwa ikitolewa na mkoloni kwa lengo la kupata wafanyakazi katika sekta mbalimbaliza kikoloni ndo hiyo imekuwa ikitolewa hata sasa katita taasisi mbalimbali za kielimu mfano mavyuoni ambapo utaona mwanafunzi anaandaliwa kuwa mfanyakazi na sio msomi, msomi kwa maana ya kwamba mtu ambae anaenda kuwa msaada kwa jamii nakua chanzo cha ajira kwa watu wengine ambao hawajafanikiwa kupata elimu lakini hii elimu ya sasa imemfanya mwanafunzi kutokua na uwezo ata wa kujiajili yeye mwenyewe badala yake amekua akitegemea ajira kama ndo chaguo lake namba moja kama ndo msaada wa kumfanya aweze kujikimu na Maisha lasivyo anaenda kuwa mtu wa chini tena chini Zaidi ya yule ambae hakufanikiwa Kwenda shule . sasa nini kifanyike?

Kwanza wanafunzi wapunguziwe idadi ya masomo wanayoyasoma mbadala wake mfumo wa elimu ubadirishwe na uwe na uwezo wa kutambua uwezo wa mwanafunzi mmoja mmoja katika hatua za awali za elimu hapa nikimaanisha shule za msingi ili elimu ianze kumjenga mapema mwanafunzi katika eneo analoonekana ana uwezo nalo mfano kompyuta.

Hii itasaidia kupunguza gharama za kumfundisha mwanafunzi masomo mengi na kwa ufanisi mdogo ambapo mengi ya hayo masomo mwanafunzi anakua hana uwezo nayo na hayatokua na msaada kwake hii husaidia sana kwani manafunzi anapoanza kuwa na sehemu ndogo ya machaguo yake inakua rahisi kwa mwanafunzi kuwa bora katika eneo hilo na kuwa na uwezo wa kujiendeleza yeye mwenyewe kwakua atakua na uzoefu mkubwa kwatika eneo hilo.

Hii itasaidia kupata wataalamu wabobezi katika sekta mbalimbali tofauti na sasa ambapo wataalamu ni wachache pia wengi wa hao wachache sio wabobezi ambapo imipelekea tuwe tunatafuta wabobezi kutoka nje ya nchi nakufanya nchi kuingia gharama kubwa napia kukosa watu ambao wangeweza kusimama wao na kujitegemea kutokana nakua na uzoefu mdogo katika yale mambo ambayo ameyasomea.

Pili mfumo wa ufundishaji inabidi ubadirike kuachana na wanafunzi kutumia muda wmingi sana wakukaa darasani na kujifunza nadharia wawe wanatumia muda mwingi pia kwenye kujifunza kwa vitendo kwasababu hiki ndo kitu pekee kinaweza mfanya mwanafunzi akawa na uelewa juu ya jambo analolisoma darasani na kuweza kulifanya likawa na matokea chanya kwa jamii inayomzunguka. Inaweza ikaonekana kawaida lakini hili suala ndo inabidi lianze mapema kwa wanafunzi hasa katika shule za msingi ikiwa ni njia ya kumfanya mwanafunzi asiwe mgeni na ulimwengu wa vitendo na teknolojia anapofika katika ngazi za juu za elimu mfano vyuo na kutufanya tunakua nyuma tunapoingia kwenye ushindani wa teknolojia na nchi zingine.


2). Kukosekana kwa mfumo wa utawala wenye sera zenye mwendelezo.hapa nazungumzia Zaidi katika vipindi mbalimbali vya ma Raisi wanapoingia madarakani ambapo kila Raisi amekua akiyapa kipaumbele mamboyake ambapo kwa namna moja au nyingine yanaonekana kuwa tofauti sana na ya maraisi walio mtangulia mfano wakati wa Raisi jakaya mrisho Kikwete alitia kipaumbele kwenye kilimo bali wakati wa hayati John pombe Magufuli aliltia nguvu sana kwenye viwanda na kuacha lile alilolianza Kikwete kwaiyo inapita miaka mingi tunajikuta kila eneo tulianza na tukaishia njiani bila yakua na mafanikio yaliyokusudiwa katika wakati uo. nini kifanyike?

Haya yote yanatokea yakianzia kutoka kwenye vyama vya siasa pia kukosekana kwa elimu ambayo ingetoa taswila ya faida yakua na mwendelezo wa sera baina ya maraisi hivyo ni bora kwa vyama vya siasa kulitazama hili kama fursa ya kuifanya Tanzania ifikiie yale maendeleo yanayo stahiri kwakuweka malengo ya chama yenye muendelezo na uhusiano na yale ya kipindi kilichopita pindi chama kinapoingia madarakani katika awamu nyingine pia niwakati sahihi wa maraisi kulichukua hili na kuona kuwa ni njia sahihi ya kulipeleka mbele taifa letu la Tanzania kuliko kila raisi kuja na sera yake ambayo inakua haina uhuhsiano wa karibu na sera za raisi wa awamu iliyopita.

Kwa ujumla elimu ndo msingi wa kilakitu katika Maisha ya mwanadamu na shughuri mbalimbali anazozifanya ambazo ndo huleta matokeo mbalimbali ikiwemo maendeleo ya nchi hivyo upatikanaji wa elimu sahihi kwa watu itasaidia kuweka mambo yote kama yalivyo pendekezwa katika andiko hili,hapa nazungumzia haswa ukombozi wa kifikra wa namna ya kuyatazama na kuyatatua mambo mbalimbali katika jamii mfano tupate watu ambao wameanza mapema kujifunza mambo ya utawala ambapo itasaidia kuwapa uzoefu wa uongozi hivyo kuleta viongozi ambao wanaelewa namna sahihi ya kuongoza nchi ili kufikia yale malengo ambayo kila raia anatarajia kuyaona katika nchi.
 
Back
Top Bottom