BABA TUPAC
JF-Expert Member
- Sep 30, 2015
- 1,533
- 3,838
Siku chache baada ya Raisi Magufuli kutangaza kubomolewa kwa jengo la Tanesco kuna sms ilisambazwa kwenye mitandao ya kijamii kuwa watu wajiandae, wanunue umeme mapema maana siku yoyote yawezekana LUKU inaweza kuwa shida kununua.
Tanesco walijitokeza hadharani kupinga hicho kitu, lakini jana jioni wakasambaza taarifa kuwa mfumo wa LUKU utakuwa haufanyi kazi kuanzia saa mbili usiku mpaka saa nne. Huu ni uongo, jana kuanzia asubuhi ulikuwa huwezi kununua umeme mpaka muda huu asubuhi naandika hapa huwezi kununua umeme.
1. Tanesco wangesema ukweli, watu wangenunua umeme mapema. Kuna watu wana mashine za kusaga hazifanyi kazi toka jana, sisi wafugaji hatuna pumba. Vipi wenye bucha, wachomeleaji, viwanda nk ambao waliishiwa umeme jana? Tanesco mna akili kweli?
2. Jana umesema watu hawataweza kununua umeme kuanzia saa mbili usiku wakati kiuhalisia watu hawawezi kununua umeme toka jana asubuhi. Kwanini hili taifa limekuwa la uongo uongo? kwanini hatupendi ukweli