Kwanini sisi Waafrika ni Masikini?

Tatizo kubwa la sasa barani Afrika sio ukoloni mamboleo kama wanavyoimba viongozi wetu bali tatizo la Afrika ni viongozi wenyewe wanaokimbilia madaraka kujilimbikizia mali wao na familia zao, ndugu zao, jamaa zao, na marafiki zao hawapo kwa ajili ya manufaa ya taifa bali kwa manufaa binafsi hiyo neo colonialism, World Bank na IMF wanatumia kama kinga kutafuta sehemu za kulaumu.

Utashangaa ni Afrika tu kwenye uchaguzi always chama tawala kinashinda wakati hakijafanya lolote kwa wananchi wakati ulaya na Marekani ambapo viongozi hudeliver kwa wananchi sio lazima chama tawala kishinde na hubwagwa sana lakini Afrika story ni tofauti always vinashinda vyama tawala kichekesho ni kwamba pindi yakitokea mapinduzi wanajeshi wakaitisha uchaguzi vyama tawala Afrika hubwagwa vibaya sana hapa maana yake ni nini?

Maana yake chaguzi za Afrika haziko huru na si za haki zipo kulinda vyama tawala mpaka mapinduzi yatokee.
 
Rais anamiliki mahoteli mbugani,mtoto anamiliki vituo vya mafuta na malori na mama anamiliki taasisi isiyokaguliwa wala kuhojiwa na yeyote pamoja na kupokea mabilioni ya misaada kwa niaba ya watanzania bado mnasubiria maendeleo ya nchi?mtakaa sana.
 
Ndugu yangu sababu umeshaeleza hapo juu, tuwe wawazi ndio maana bado mimi huwa namaswali mengi sana kupitia kuanzia kizazi cha Adam na Hawa ilikuwa mabara yakajitenga kama tulikuwa kitu kimoja???? Lakini histori inaonyesha kabisa wazungu wanakuja Africa kwa lengo la rasilimali nambaya kabisa nikutufanya sisi vijakazi hali yakuwa mababu zetu hawajui A wala B.

Wenzetu miaka ya 1800 wanajua technology nikitu gani sisi tunaishi kama wanyama na walikuja kutukamata kama unavyokamata swala au kuku.

Hatuwezi kutoka kwenye mikono ya Hawa jamaa na elimu wametupa sisi. Isipokuwa ignorance yetu ndio imeendelea kuwafaidisha wazungu na sisi tukiendelea kuwa maskini. Tumetoka mbali jamani sometimes najiuliza m/mungu bara letu kwanini alilisahau kwasababu hata Imani zetu tumeletewa natunauana kwa vitu tulivyoletewa hawa watu weupe!!??
 
swali lako lina majibu mengi. historia ya bara hili ni ndefu mno na mpaka sasa tumeshindwa kujinasua ingawa tunauelewa wa mambo mengi kwasasa.
 
Ni siasa kila kitu siasa, viongozi wa africa wengi wanajali matumbo yao na maslahi yao ukiwagusa kama usipokufa basi meno na kucha ni halali yao, wako tayari kuuza migodi,aridhi,kuua watu wote ili mradi matumbo yao yasiguswe sasa hapo unategemea nini?
 
Bado hatuna uelewa maana kama tunajua tukifanya hivi tutaendelea na hatufanyi kuna tatizo kubwa. Uelewa tulio nao ni ni kwamba kuiba Mali ya lazima utajirike na pia usipotoa na kupokea rushwa huwezi pata haki,ni huu ndo mfumo ulio rasimi na unaotafuna akili zetu. Pia ni wachache sana wanaoumia na matatizo ya watu wao au bara la Afrika kwa sasa.
 
swali lako lina majibu mengi. historia ya bara hili ni ndefu mno na mpaka sasa tumeshindwa kujinasua ingawa tunauelewa wa mambo mengi kwasasa.

Tutajitetea sana na issue ya bara la africa, nitanue mjadara, nchi kama Haiti, Jamaica n.k hazipo bara la Africa lakini kwanini nazo ni masikini!? Well hata huko Marekani, maeneo yanayokaliwa na Waafrika na yenyewe ni masikini, Zimbabwe (ipo Afrika) ilipofukuza wazungu tu, njaa na shida mbalimbali zikagusa nchi hiyo? Kuna nini na sisi Waafrika!?
 
Ndugu yangu Mazindu Msambule.. tatizo Dunia au niseme ulimwengu unaendeshwa na systems mbalimbali. Usifikiri sisi Tanzania ama Africa tuko peke yetu kwahyo kila jambo tunaweza kuamua wenyewe LA Hasha si hivyo. Kila unachojua kinagusa UN kuanzia afya, uchumi,elimu n.k.

Kwahyo system ni ileile yakimaisha kwamba mwenye nacho ndio huongezewa, ukizungumzia Waafrica walioko Marekani kwani hujui wale nindugu zetu wazazi wao walikuwa wafanyakazi wandani ama mashambani. Ila ujinga bado unatutafuna sana watu wamekwenda vidato vingi lakini hawajaelimika.

Mtu anafikiri akiwa na PHD ndio kuelimika huyo kasoma lakini anaweza asiwe na Elimu. Ndio maana yapo mambo makubwa wazee wetu walifanya bila kwenda shule.
 
Umaskini wa Bara hili unachangiwa mambo mengi sana,Kwa mtazamo wangu ukiachana na mfumo mbovu wa serikali/utawala na mgawanyo wa madaraka pamoja na mfumo wa elimu usiozingatia matakwa halisi ya mfumo wa kiuchumi,Pia kuna hili suala la utamaduni.Kwangu mimi utamaduni ndiyo chanzo cha matatizo mengine yote yanayoliandamana Bara hili. Utamaduni wa Kiafrika ndiyo unaozaa aina ya viongozi tulio nao.

Kulingana na utamaduni wa Kiafeika, Waafrika tunalelewa kuwaheshimu mno watu waliotuzidi umri. Ni ishara ya kukosa adabu na nidhamu kwa mtu kubishana au kumkosoa MTU mwingine aliyemzidi umri.

Matokeo ya makuzi ya namna hii huonekana kwenye aina za siasa tunazozifanya iwe kwenye Bunge au kwenye vyama vyetu vya siasa.Mfano halisi ni kushambuliwa kwa Lissu kuhusiana na maonu yake juu ya utawala wa mwalimu Nyerere hususan kwenye suala la Muungano.

Kwa ujumla utamaduni wa Kiafrika unatuandaa kuwa RAIA tusiotakiwa kuhoji jambo lolote maadam linafanywa na watu wenye mamlaka ya juu kuliko sisi kwenye jamii na vile vile utamaduni huu unawandaa viongozi wasuopenda kuhojiwa au kukosolewa hata kama wanafanya maamuzi yenye athari hasi kwa wanaowaongoza.

Pili,Utamaduni wa Kiafrika una-promote extended family ambao ndani ya utaratibu huu households zinaweza kuwa na mama,baba,watoto,wajomba,bibi,babu na ndugu wengine wote kwa wakati mmoja.

Pia katika extended families watoto wanaweza kukaa na wazazi wao hata wakiwa na miaka 40.Mfumo huu wa kufamilia unachangia sana Kuzalisha watu tegemezi na wasiokuwa na ari ya kufanya makubwa katika maisha yao. Watu wanaokulia katika mazingira ya namna hii huwa ni wepesi kuridhika na mafanikio madogo wayapatayo na ni tegemezi kwani mara nyingi hawaamini uwezo wao wenyewe mpaka wapewe mwongozo.

Ukija kwenye malezi yenyewe ya watoto sasa,Utakuta watoto wanakatazwa wasifanye jambo flani eti mwiko bila kuambiwa sababu ni nini,Huu ni mlolongo wa aina ya maarifa wanayopewa Waafrika maarifa ambayo yana-discourage logical thinking. Hata aina ya elimu tunayopewa ipo hivyo hivyo katika mtindo wa indoctrination lakini wanafunzi hawafundishwi critical thinking juu ya kile wanachomezeshwa.

Viongozi wa Serikali za Kiafrika kushindwa kutumia resources kujenga nchi zao ni matokeo ya kimakuzi tu.Wamelelewa kuamini katika utegemezi, kutojiamini kwamba wanaweza kufanya makubwa kama Wazungu, Kuridhika haraka na mafanikio madogo wayapatayo na kupenda kuabudiwa kama Miungu.
 
Kanuni ya msingi ya kuondoa umaskini ni kuhakikisha unalinda sana ulicho nacho au kukitumia kwa faida na pia kutafuta nyongeza kutoka kwa wengine kwa njia za kistaarabu.

Tunahitaji viongozi na wananchi wote waelewe hivyo!

Waafrika wanashindwa kulinda walicho nacho au kukitumia kwa faida. Wageni wanapora maliasili kutoka Afrika watakavyo, wanalinda walicho nacho kule kwao huku viongozi wa kiafrika wakitembeza bakuli la kuombaomba kwao. Hali hii inatokana tu na utumwa wa fikra.

Utumwa wa fikra kwa viongozi unasababisha ufisadi wa kuhamisha fedha kuficha Uswis na kwingineko huku wakiwaacha wananchi wao kwenye lindi la umasikini, mikataba mibovu, serikali zinazoongozwa kipuuzi n.k.

Waafrika tumesahau hata kutumia akili ndogo ya msingi ya wazee wetu wa kiswahili waliosema " Kila mvuta kamba huvutia kwake" Kwa utumwa wa fikra tunavutia upande mwingine!

Hata hivyo hali hii inaweza kubadilishwa na waafrika wenyewe kwa kujua kwamba suluhu ya umasikini wao iko mikononi mwao wenyewe, wapendane, walinde maliasili zao, waache kuingia mikataba ya kuwanyonya bali waingie mikataba itakayowanufaisha wao zaidi ya wengine, waache kujikomba kwa mataifa mengine, wajione huru na bora kuliko hata hao wengine katika nafasi yao waliyopewa na Mungu katika ulimwengu huu.
 
Ndugu yangu Mazindu Msambule.. tatizo Dunia au niseme ulimwengu unaendeshwa na systems mbalimbali. Usifikiri sisi Tanzania ama Africa tuko peke yetu kwahyo kila jambo tunaweza kuamua wenyewe LA Hasha si hivyo. Kila unachojua kinagusa UN kuanzia afya, uchumi,elimu n.k.
Kwahyo system ni ileile yakimaisha kwamba mwenye nacho ndio huongezewa, ukizungumzia Waafrica walioko Marekani kwani hujui wale nindugu zetu wazazi wao walikuwa wafanyakazi wandani ama mashambani. Ila ujinga bado unatutafuna sana watu wamekwenda vidato vingi lakini hawajaelimika. Mtu anafikiri akiwa na PHD ndio kuelimika huyo kasoma lakini anaweza asiwe na Elimu.
Ndio maana yapo mambo makubwa wazee wetu walifanya bila kwenda shule.


Kwa Tanzania tatizo ni CCM kwa Afrika tatizo ni watawala waliohodhi madaraka kwa muda mrefu au vyama vilivyohodhi madaraka kwa muda mrefu vikageuza nchi au wakageuza nchi kitega uchumi sababu ulizoweka ni nyongeza tu ndogondogo tatizo kuu la kwanza Afrika ni watawala. Koffi Annan Katibu mkuu wa UN akihutubia mkutano mkuu wa viongozi wa nchi za Afrika mjini Addis Ababa alisema. "Poverty, conflicts, wars and violence in Africa are the results of misguided leaderships of African leaders who are unable and unwilling to put people interest first" Koffi Annan, UN Secretary General 2002
 
Uzalendo ndio sababu kuu ya umasikini, hakuna kingine chochote.

Uzalendo wa kujali maslahi ya wananchi.

Uzalendo wa kulinda maliasili ya nchi na kuwanufaisha wananchi.

CCM wapo tayari wauze nchi ili wao wapate hela za kampeni.
 
Back
Top Bottom