Kwanini sio Tanganyika? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kwanini sio Tanganyika?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Swahilian, Oct 24, 2010.

 1. Swahilian

  Swahilian JF-Expert Member

  #1
  Oct 24, 2010
  Joined: Apr 28, 2009
  Messages: 558
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Habari zenu Watanzania wenzangu na poleni na majukumu ya ujenzi wa Taifa letu hili changa.

  Baada ya salamu kwenu nimeona si vibaya nikapata ujuzi na uelewa zaidi juu ya masuala mbalimbali ya Taifa hili ili niondoke katika utata katika masuala kadhaa yanayoniumiza kichwa.

  Kwanza ningependa kujua au ninavyofahamu mie ni kwamba Visiwa vya Zanzibar/Pemba viliungana na Tanganyika kuunda nchi moja inayoitwa Tanzania, lakini katika kipindi cha karibuni tumeweza kuona mabadiliko mengi na hasa kila anayeunga au kupinga hoja hizi za muungano kutetea maslahi ya Taifa lake hapa namaanisha Wazanzibar, Wapemba na kiasi kidogo kwa Watanganyika.

  Tumeweza kuyaona hayo bungeni na katika baraza la wawakilishi na kwa kiasi kikubwa hoja ya Mafuta kuwa ni suala la Muungano au la Visiwani Pekee.

  Katika kipindi hiki tumeona mabadiliko mbalimbali kwa upande wa Visiwani mfano, Bendera ya Zanzibar, Vitambulisho vya Mzanzibar mkazi, kura zilizopigwa hivi karibuni (SERIKALI MSETO) na Mengineyo mengi yanayoamsha maswali na fikra za hali ya juu.

  Nimeona nijadili nanyi haya ili nijue nanyi mnadhani kipi kifuate? Nasi twahitaji vitambulisho vya Mtanzania mkazi au siyo? Serikali zetu zi ngapi? Na bendera yetu ya Bara ni ipi na Ya Tanzania, nafikiri haya ni muhimu kuyajua na kuyafanyia kazi kwa maslahi ya ustawi wa Taifa letu.

  Ufike wakati sie wote tujue kama tuko na serikali tatu, nne au tano na Muungano.

  MOLA ATUBARIKIE

  UCHAGUZI WA FANAKA
   
 2. Swahilian

  Swahilian JF-Expert Member

  #2
  Oct 25, 2010
  Joined: Apr 28, 2009
  Messages: 558
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Jamani mwenye macho haambiwi ona! Na ajuae lugha niandikayo hashindwi kusoma, sasa ni vipi? Au haionekani? NAombeni Mchango Wenu nami nipone na donda hili...
   
 3. Mtu wa Pwani

  Mtu wa Pwani JF-Expert Member

  #3
  Oct 25, 2010
  Joined: Dec 26, 2006
  Messages: 4,096
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  anza na kujisafisha moyo wako
   
Loading...