Kwanini siku hizi maeneo haya ya Kitajiri jijini Dar es Salaam hizi mboga zinauzika na kuisha haraka?

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Jul 13, 2013
56,742
109,178
Zifuatazo ni Mboga ambazo kiukweli siku hizi zinauzika na zinaenda kwa kasi sana kuliko ilivyokuwa huko nyuma ambazo kwa haya maeneo ya ' Kitajiri ' nakumbuka hizi mboga zilikuwa zikinunuliwa na kupewa sana Mbwa, Paka, Sungura, Mbuzi na Ng'ombe ila kwa sasa imegundulika ' Binadamu / Watu ' wa hayo maeneo ndiyo wanazitumia sana katika milo yao ya kila siku.

Maeneo hayo ni:

  1. Mbezi Beach kwa ' Washua '
  2. Kawe Beach kwa ' Washua '
  3. Bahari Beach kwa ' Washua '
  4. Kunduchi Beach kwa ' Washua '
  5. Mikocheni Uznguni acha hii yetu ya Uswahilini
  6. Masaki na Oysterbay
  7. Kijitonyama na Makumbusho mitaa ile ya ' Washua '.
Na hizo ' mboga ' zilizotukuka kabisa ambazo kwa sasa zinauzika na zinaenda kwa haraka / kasi sana hayo maeneo tajwa hapo juu ( ya ushuani / ya wenye pesa ) ni zifuatazo:
  1. Dagaa
  2. Mnafu
  3. Matembele
Najua na nina uhakika kabisa kwamba humu Jamvini JF kuna Watu / Members wengi sana waishio hayo maeneo tajwa na wachache wetu kama akina GENTAMYCINE ndiyo tunaishi huku Kwetu Tandale Uswahilini kwa Mama Paka hivyo watajitokeza kutoa ushirikiano wao juu ya hii ' kitu ' tujue kwamba labda ina ukweli wowote au ni Watu tu wanawachafua.

Nawasilisha.
 
Nadhani wengi wamekuja kugundua pizza,nyama,kuku wa kizungu nk havina virutubisho.Pia magonjwa yamekuwa mengi siku hizi.

Wamekuja kugundua kuanzia mwishoni mwa mwaka 2015 hadi 2017 Mkuu? Kwahiyo miaka ya 2005 hadi 2015 hawakuligundua hilo tatizo / hayo matatizo?
 
Matajiri wamegundua kuwa wataongeza siku zao za kuishi kwa kula mboga hizo na kupunguza ulaji wa nyama hasa nyama nyekundu

Huo ' Ugunduzi ' wao mbona umeanzia tu mwishoni mwa 2015 hadi sasa 2017 lakini huko nyuma kwa mfano kati ya mwaka 2005 hadi October 2015 hawakugundua? Je tatizo lilikuwa ni nini / lipi labda?
 
Hapo kwenye dagaa umeongopa!

Dagaa wa maeneo hayo tajwa ya ' ushuani ' miaka ile ya kati ya 2005 hadi October 2015 ilikuwa ni Mbuzi, Kuku na Samaki tena wale wa kule Kwetu Ziwa Victoria Sangara na Sato Mkuu isipokuwa hawa ' Dagaa ' wa kwelikweli walikuwa wakichanganywa katika ama Chakula cha Paka au Mbwa ila kwa sasa hata ' Binadamu ' wa hayo maeneo ya ' Washua / Kishaua ' wanatiririka na kuserereka nao katika milo yao ya 24/7.
 
Hayo maeneo kutokana na ulaji wao mbovu walikuwa waathirika wakubwa sana wa magonjwa kama shinikizo la damu, kisukari, uzito mkubwa nk nadhani wameamua kureview menu jambo ambalo ni jema na halitegemei unaanza lini ili mradi tu unaijali afya yako na kwa namna hiyo fedha walizokuwa wakizipeleka india kwa ajili ya matibabu (maana sidhani walikuwa wanatibiwa hapa nchini) wanaziinvest hapa nchini na kama hivyo ulivyosema hao wauzaji wamepata soko pia, ni jambo la kuwapongeza sana
 
Huo ' Ugunduzi ' wao mbona umeanzia tu mwishoni mwa 2015 hadi sasa 2017 lakini huko nyuma kwa mfano kati ya mwaka 2005 hadi October 2015 hawakugundua? Je tatizo lilikuwa ni nini / lipi labda?
Hii research methodology mbona inaonekana probability of the answer is already known by a researcher.
Anayway jirani yangu wa huku kwetu Kwamtogole anafanya kazi za ndani huko ushuani anasema sikuhizi anaambiwa aongeze mchele kwenye chakula cha jioni ili kibaki kipolo cha kunywea chai
 
hata uchumi udondoke vipi... matajiri wa ukweli hawawezi kukosa hela ya kula...

watakosa hela za kujengea au kununua magari... lakini sio chakula
 
Back
Top Bottom