Kwanini sigara zinaruhusiwa kutangazwa kwenye vyombo vya habari?

FRANCIS DA DON

JF-Expert Member
Sep 4, 2013
36,465
41,438
Nilikuwa nadhani ni vyema matangazo yote ya bidhaa za tumbaku yapigwe marufuku, hata zile promotion za sigara kwenye mabaa zipigwe marufuku kabisa.

Hii inatokana na ukweli kwamba wavuta sigara hawahitaji kutangaziwa kwani wakipatwa na kiu ya sigara wataifuta popote ilipo.

Hivyo basi matangazo na promosheni za sigara zina lengo ovu la kuwaingiza uraibuni wale ambao hawavuti sigara, huu ni uovu unafanywa na ni lazima upigwe vita.

Pia packet za sigara zisiweke rangi ya aina yoyote ile, cha zaidi iwekwe picha za watu wenye kansa zitokanazo na sigara ili kuelezea matumizi yake.
 
Kuna wengine sisi sio walevi ila wavutaji wazuri tu!, unataka na sisi tuombe mzuiwe matangazo ya pombe. Kuna mlevi asiyejua bar/pub/kilinge cha pombe za bei chee eneo lake?

UVUTAJI SIGARA NI HATARI KWA AFYA YAKO.
 
Achana na starehe za watu wewe, sigara zinakuhusu nini? Hayo matangazo yanakukera na nini?
 
Usihangaike waache wajimalize..Maana haina tofauti na kuambiwa hii ni sumu, alafu unaichukua unaweka kwenye chai ya maziwa unakunywa.
 
Chombo gani cha habari kinatangaza sigara?
Naona vipeperushi vingi sana vinabandikwa kwenye maduka ambayo hata watoto wadogo huenda hapo, kuna tangazo moja limebandikwa dukani ni la master kama sikosei, linasema eti 'Tumbaku, fahari ya nchi yetu', just imagine! Mtoto atachukuliaje huo ujumbe?
 
Nimeona nitie neno katika hili.

Ndugu yangu,sigara zilizuiwa kutangazwa kwenye radio, tv na magazeti tangu mwaka 2000.

Zamani tulikuwa tukisikia matangazo ya sigara radion au kwenye magazeti.


Hiyo claim kuwa sigara zinatangazwakwnye vyombo vya habari, kifupi ni uwongo, hakuna sigara inayotangazwa kwenye vyombo vya habari.

Sambamba na kutangaza sheria ilitaka mvuta sigara awe katika eneo lililotengwa kwa ajili yake smoking zone/area
 
Back
Top Bottom