Kwanini Shule ya Sheria iko Dar pekee?

Brigedia Chan-ocha

JF-Expert Member
Mar 7, 2014
1,353
2,846
Kwanini watendaji wetu wasiwe wabunifu na akili zao zifanye kazi 24 hours?

Hivi kuna umuhimu gani wa wanafunzi wanaotaka kusomea Uwakili katika shule ya sheria, au school of Law wasifungue Branch mikoani, yaani watu wote lazima waende Dar?

Nadhani Waziri wa Elimu Mh. Ndalichako litazame hili kwa kina, haiwezekani kila mtu akaja Dar, kusomea hiyo kozi, fungueni Branch mikoani mfano, Mbeya, Mwanza, Arusha au Tanga.

Au kama hamtaki basi mruhusu kila chuo kinachotoa shahada ya sheria kiruhusiwe kutoa na kozi hiyo katika chuo husika, mnaweza kubadili sheria mkaruhusu hili, ila usimamizi, ubora nk. ndo uachwe kwa "Shule kuu ya sheria"

Hakuna haja ya kila mtu kuja dar. kisa kusomea kozi hiyo.
 
Ni kweli kabisa, hata Mimi sioni umuhimu wa Law school kuwa Dar. pekee bila kuwa na branch...

inabidi Waziri Joyce Ndalichako alitazame hili kwa kina.
 
Haiwezekani Nchi nzima ikawa na Law school moja tu,

Tena hilo wazo la kila Chuo kuwa na Law school yake. ni muhimu sana, Sheria ibadilishwe ili Shule juu ya sasa yenyewe ibaki na "Usimamizi, ubora, na ufuatiliaji.

Au kama vipi, basi Law school ifungue branch zake Mikoani,

Sasa dar. na msongamano wa watu ulivyo, gharama kubwa ya maisha, na wengine hawana pa kufikia baada ya kufika hapa....
 
Kwanza nikukosoe kidogo, shule ya sheria haipo chini ya wizara ya elimu ipo chini ya wizara ya katiba na sheria so Ndalichako hahusiki chochote hapo.
Sheria inayoanzisha shule ya sheria inaruhusu kuanzishwa kwa matawi maeneo mengine ya nchi so nadhani ni suala la muda tu kutegemea na mahitaji yatakavyokuwa japo ni kweli sasa niuda muafaka wa kufanya hivyo.
 
Asante kwa kusahihisha, Ni kweli kwamba kumekuwa na usumbufu mkubwa sana, yaan kila mtu Dar? kisa "Law school"?

Mwakyembe fanya faster bhana Hili tawi kuu lifungue Branch mikoani.
 
Sio huko tu serikali iliyo seriously pia itupie jicho kwa chuo cha usafirishaji pia yaani NIT found only mabibo dsm tunashindwa wa mikoani kujiendeleza
 
Mi binafsi law school kuwa moja imeweza kufanya wanasheria wote kuwa kitu kimoja, ukitaka uwe kile mkoa it means haitawafanya wanasheria kufanana hapo itatengeneza matabaka kama ya vyuo. We mwenyewe umeona watu wanavyodharauriwa kufuatana ma chuo alichotoka. Mi binafsi nimependa kilivyo kimoja ukisema tuwe kama cpa kila fani ina utaratibu wake, kuhusu gharama hata udsm pia muombe ihamie mbeya, lingine law school watu wanapata mkopo kama undergraduate, ukisema gharama popote ni gharama kwa sababu unatoka mazingira ya kwenu lazima gharama iwepo hata mkoani. Ila cha kuomba ni kwamba tujengewe hostel maana vyumba ni gharama hilo ndo la muhimu. Mtu alipie tuu hostel ili kupunguza hizo gharama
 
in fact school of law ilipokuwa moja pale UD Taaluma ilikuwa respected walipoacha kuimonopolize vikaibuka vyuo vinafundisha hata miaka mitatu na tunaona kawaida, vyuo vingine vinahonga honga tuu vibinti hata actus reus havijui vina GPA kubwa hatari... in fact kama taaluma zenu zimeharibiwa muiache hii law iwe kama ilivyo ibaki law school moja ichambue wanao toka sehemu mbali mbali. Pia kwani huko dar unapenda uende peke yako tuu? yaani wengine wanapokuja unajisikia vibayaaaaaa so uungwana muheshimiwa
 
Law School haipo chini ya wizara ya elimu ipo chini ya wizara ya katiba na sheria,it is right where it is suppoed to be ikianza kuwekwa mikoani itachakachuliwa na mawakili feki ambao hawajui kitu watakua mtaani. System iliyopo inaumiza wengi lakini there is no way ni bora ukomalie kitu ukikipata ujue thamani yake sio kukipata bure bure tu.
 
Mi bin

Mi binafsi nimependa ilipo sasa ajabu utakuta mtu wa sociology analalamika ungejua kile ni chungu kinachopika chakula kikaiva ni kile, kwanza tusilalamike kwa kila jambo serikari imejitahidi kwa kweli imejenga vizuri, mazingira mazuri, walimu usiseme, mitihani yao ndo kabisaa ukitoka pale hata bila muhuri unakuwa umeiva, yaani nashindwa kuelezea umuhimu wa eneo lile, pia mtoa maada unazijua gharama za kusimamia na kujenga mazingira kama yale, ningekuona una akili ungeomba kujengewa hostel lkn sio kukutenganisha. Nani asiependwa kufundishwa na manguli waliobobea, majaji, wataalamu wa kila eneo la sheria wanaiitwa ili mradi tuu tuelewe, mkoani utasaidia ilo fungu wewe, hiyo hela ya kujenga law school si ingesaidia kununua dawa hospitalini, madawati ya watoto, hata trekta kwa wakulima
 
in fact school of law ilipokuwa moja pale UD Taaluma ilikuwa respected walipoacha kuimonopolize vikaibuka vyuo vinafundisha hata miaka mitatu na tunaona kawaida, vyuo vingine vinahonga honga tuu vibinti hata actus reus havijui vina GPA kubwa hatari... in fact kama taaluma zenu zimeharibiwa muiache hii law iwe kama ilivyo ibaki law school moja ichambue wanao toka sehemu mbali mbali. Pia kwani huko dar unapenda uende peke yako tuu? yaani wengine wanapokuja unajisikia vibayaaaaaa so uungwana muheshimiwa
actus reus: criminal act.........
 
kibaki hapo hapo ili ubora wa elimu uendelee, maana kwa sasa kinatoa mwanafunzi aliye na uwezo mzuri
 
Law School ni kakichaka flani hivi ka uraji kwa baadhi ya watu,ni "wahujumu uchumi "...na wadidimizi wa utawala bora wa kisheria,kwa kua kikwazo cha idadi ya kuzalishwa mawakili kwa njia ya kuwa na chuo kimoja tu na pasipo kutoa mwanya wa vyuo vingine kufungua course hiyo ya miezi takribani nane...kama haitoshi walianza na grant,baade wakaona inaongeza idadi ya waombaji na wasomaji..sasa wameitoa..wakidai wanaleta mkopo..mkopo hakuna..mtoto wa masikini asomi...lengo lao wasome watoto wa big fishes wakatete maslahi ya wazazi wao!
 
Mi binafsi law school kuwa moja imeweza kufanya wanasheria wote kuwa kitu kimoja, ukitaka uwe kile mkoa it means haitawafanya wanasheria kufanana hapo itatengeneza matabaka kama ya vyuo. We mwenyewe umeona watu wanavyodharauriwa kufuatana ma chuo alichotoka. Mi binafsi nimependa kilivyo kimoja ukisema tuwe kama cpa kila fani ina utaratibu wake, kuhusu gharama hata udsm pia muombe ihamie mbeya, lingine law school watu wanapata mkopo kama undergraduate, ukisema gharama popote ni gharama kwa sababu unatoka mazingira ya kwenu lazima gharama iwepo hata mkoani. Ila cha kuomba ni kwamba tujengewe hostel maana vyumba ni gharama hilo ndo la muhimu. Mtu alipie tuu hostel ili kupunguza hizo gharama

Serious can you raise this argument to dend the reality?ni kibaraka sio bure..! If an advocate of any common law legal system anaweza fanya katika nchi yoyote yenye mfumo huo,itashindikana vipi aliyesoma tanga au mwanza?!!
 
in fact school of law ilipokuwa moja pale UD Taaluma ilikuwa respected walipoacha kuimonopolize vikaibuka vyuo vinafundisha hata miaka mitatu na tunaona kawaida, vyuo vingine vinahonga honga tuu vibinti hata actus reus havijui vina GPA kubwa hatari... in fact kama taaluma zenu zimeharibiwa muiache hii law iwe kama ilivyo ibaki law school moja ichambue wanao toka sehemu mbali mbali. Pia kwani huko dar unapenda uende peke yako tuu? yaani wengine wanapokuja unajisikia vibayaaaaaa so uungwana muheshimiwa
You are confuse the two..law was monopilised with the few and now even individuals from poor families possess the bacherol and you are worried that the influx is too high to defeat your interests or to loose the battle in court...hawa hawa vijana waleo wanawendesha mahakamani.

Degree za kupeeana ata mlimanj zipo nyingi tu
 
Mi napita tu!!! BTW sioni hata umuhimu wa hiyo law school cheki huko zanzibar sakata la uchaguzi mawakili mnaojiita wasomi mko wapi??? Wafungwa wangapi wamefungwa bila hatia mawakili mko wapi??? Watu wangapi wako na matatizo na nyie mpo tuuu hata hamueleweki kazi mnakaa na kujiita learned lawyers sijui brothers uji.nga tu!!
 
Kabla ya kuropoka..jaribu pia kujiuliza kwa nini ndio uje kujenga hoja;

Kunakitu kinaitwa Locus Stand,iwe uwe wakili au nani unayejua sheria au uji..huwezi kwenda mahakamani bila kuwa na locus stand.
 
Back
Top Bottom