Kwanini "Service charge" ya TANESCO ni tatizo linalohitaji utatuzi wa haraka!

Najua watu wengi wameandika kuhusu Tanesco na naomba kwa wasimamizi wa Jukwaa hili wauache uzi huu kama ulivyo ili wahusika (ambao nina hakika watausoma) wapate kujua kwa kina.

Kwanza kabisa kwa wale wanaotumia umeme wanajua kwamba tulikuwa na mfumo wa zamani ambao Tanesco walitembelea nyumba zetu na kufanya matengenezo na ukaguzi wa mambo mbalimbali ikiwamo mita za umeme. Sina hakika kama hichi ndio chanzo cha haya makato, lakini ni dhahania yangu kuwa ndizo "service" tulizolipia nyakati hizo.

Sasa ni nyakati mpya. Ukitaka LUKU unalipia, na umeme unaotumia pia unalipia. Sasa service charge ni za nini? Service ipi hasa ambayo unatozwa wakati mwingine mpaka 5000/= au zaidi kwa mwezi?

Hebu tulinganishe makato haya kuona tatizo hili jinsi lilivyo kubwa:
Ukiwa na akaunti ya kawaida benki unalipia kama 700/= kwa mwezi. Ukiwa na akaunti ya kampuni, unalipia kama 7000/= kwa mwezi. Ukiwa na LUKU unalipia kama 5000 kwa mwezi.

Nadhani hata neno LUKU halina maana hapa. Kwa sababu LUKU ni lipia kadri unavyotumia. Naomba niweke mifano miwili tu hai kuonyesha tatizo hili sio dogo kama wengi wanavyolichukulia:
Kuna watu wawili hawakuwepo nyumbani kwa miezi 6. Mmoja alinunua umeme wa elfu 60 na mwingine elfu 50. Wa elfu 60 alipata unit 0 na wa pili alipata unit zisizofika 10.

Kumbuka hawa watu hawakuwa wanatumia umeme husika kwa miezi yote sita. Iko wapi hapo concept ya Lipia Kadri unavyotumia?

Lakini katika makato hayo kuna makato ya REA. Ni makato yenye lengo jema kabisa, kusaidia kupeleka umeme vijijini ili kusukuma maendeleo. Hivi tukiwa wakweli, watu wangapi vijijini wataweza kulipia 5000/= au zaidi kwa ajili ya "service charge"?

Kabla sijamalizia naomba kuelimishwa kwa nini umeme una makato mengi hivi ilhali ndiyo primer energy kwa maendeleo yetu? Kwanza bei ya umeme wenyewe kwa unit ni mkubwa sana (295/= kwa unit). Hapo bado kuna VAT (18%), EWURA (1%), REA (3%) na service charge (5000+/= @month).

Nadhani ni wakati wa kutuondolea haya makato. Mtu anayehitaji Tanesco service na ailipie kwa wakati huo atakapoihitaji. Haya makato ya kiujumla jumla tu yanaumiza sana wananchi. Niisihi serikali iliangalie hili kama moja ya mambo yanayorudisha nyuma sana maendeleo yetu. Umeme ni nishati muhimu sana na hivyo ni vyema ikaangaliwa kwa ukaribu kabisa ili kuleta mapinduzi ya kiteknolojia.
Sichangii neno kimsingi umemaliza mi nasoma coment
 
Mkuu maandamano ya nini wakati TANESCO wanaofisi kila sehemu na wanapokea maoni.
Service charge inalipwa maramoja kila mwezi, na usipolipa mwezi uliopita mwezi huu utakatwa mara mbili, makato ya mwezi uliopita na makato ya mwezi huu.

Huwezi ukalipa service charge ya mwezi ujao, mfano hata ukinunua umeme wa 60,000 utakatwa service charge ya mwezi huu. Mwezi ujao kama bado utakuwa na umeme itakulazimu ununue umem kidogo ili kulipia service charge.

Ukishalipia service charge hata risiti yako ikipotea kabla hujaweka umeme huwezi kutozwa tena pesa. Na umeme wako utaupata ukipiga simu TANESCO watakusomea token zako(umeme) kwa maana hiyo utauweka.

Karibu kwa maswali zaidi Asante

Namba yangu ya mita ya Luku ni 01342522593
 
JE KUNA UKWELI WOWOTE AU NI UZUSHI TU KUWA WAFANYAKAZI WOTE WA TANESCO TANZANIA NZIMA WANAPEWA UMEME WA BURE KILA MWISHO WA MWEZI? NA KAMA WANAPEWA NI KIASI/UNIT NGAPI KWA KILA MWISHO WA MWEZI?
 
JE KUNA UKWELI WOWOTE AU NI UZUSHI TU KUWA WAFANYAKAZI WOTE WA TANESCO TANZANIA NZIMA WANAPEWA UMEME WA BURE KILA MWISHO WA MWEZI? NA KAMA WANAPEWA NI KIASI/UNIT NGAPI KWA KILA MWISHO WA MWEZI?

HAKUNA UKWELI WOWOTE NDUGU YANGU, HAKUNA MFANYAKAZI ANAYEPATA UMEME WA BURE.
 
Wanatakiwa wabuni jinsi ya kuongeza kipato siyo kuwaibia wananchi. Hili ndio tatizo la kuwa na kampuni moja ya umeme (Monopolies) na sithani kama regulator wananguvu za kutetea wananchi. Nchi kama UK wana regulator OFGEM ambaye anahakikisha fair price na fine pale umeme unapokatika katika bila sababu za msingi.
Jumamosi nilifuatilia baada ya kuona service charge hainihusu nikaambiwa service charge ni shs 5800 na hiyo ni lazima.

Nashauri wadau tuunde jumhia ya watumiaji umeme Tanzania ili mambo yetu tuyafuatilie kisheria likiwamo hili. Naomba tuuungane la sivyo TANESCO wataendelea kutunyima umeme huku wakikwapua hela zetu
 
Binafsi nakerwa sana na hiki kitu kinaitwa 'service charge'. Ukiwa na tatuzi la kiufundi unaita watu wa tannesco na bado unagharimika sasa haya makato ya kila mwezi yanayofikia hadi 5000 kila mwezi kazi yake nini?
 
Nakubaliana na wewe. Dili za watu zinabadilishwa majina na kuitwa service charges na zote anawekewa mlaji!!!
Hakuna huruma!
nchi haina mfumo maalum wa kupiga pesa, kila mmoja ananjia yake, baadhi wanaita service charge, wengine sumatra, na rea.
Sasa imetosha kama ni kuona tumeona, tuhurumien, 5,520 ya service charge ni kubwa sana, punguzeni mfanye hata 300
 
Hili ni kwamba service charge ni ajili ya kulipia gharama zote za dharula na zisizo za dharula kwa mfano unapopata tatizo lolote hutozwi gharama yeyote ile ila pesa hiyo ndiyo kazi yake, mita yako ikipata tatizo hutozwi chochote bali unabadilishiwa bure. Service charge inawahusu watu Wa tariff T1 hadi T3. Ila D1 ambao ni wateja wadogo hawalipi service charge na gharama ya unit 1 in sh 100 tuu. Na hii wamelengwa zaidi watu wanye uwezo mdogo kimaisha na wasio na matumizi yasiyozidi unit 75 kwa kila mwezi majumbani mwao.
Naomba nirekebishe uliposema unit inauzwa 295 hapana ni 298 na vyote hivi TANESCO hawapangi wao vinapangwa na EWURA kama unavyoona bei za mafuta na maji.

Nimekuelewa.
 
Binafsi nakerwa sana na hiki kitu kinaitwa 'service charge'. Ukiwa na tatuzi la kiufundi unaita watu wa tannesco na bado unagharimika sasa haya makato ya kila mwezi yanayofikia hadi 5000 kila mwezi kazi yake nini?

Sio kweli unapopata tatizo unagharamika, hautozwi gharama yoyote. Mteja anapopata tatizo kama nguzo kuanguaka, nyaya kukatika, meter kuharibika mafundi wa TANESCO wamekuwa wakitoa huduma bure kabisa kitu ambacho ingekuwa private company ingeingizwa kwenye gharama za mteja ,Service charge imesaidia hili. Service charge ni kama bima ambayo tunawekeza kwenye shirika la umeme nchini ili liweze kuhudumia wateja wote pale wanapopata hitilafu ya umeme.
 
nchi haina mfumo maalum wa kupiga pesa, kila mmoja ananjia yake, baadhi wanaita service charge, wengine sumatra, na rea.
Sasa imetosha kama ni kuona tumeona, tuhurumien, 5,520 ya service charge ni kubwa sana, punguzeni mfanye hata 300

Sio kweli unapopata tatizo unagharamika, hautozwi gharama yoyote. Mteja anapopata tatizo kama nguzo kuanguaka, nyaya kukatika, meter kuharibika mafundi wa TANESCO wamekuwa wakitoa huduma bure kabisa kitu ambacho ingekuwa private company ingeingizwa kwenye gharama za mteja ,Service charge imesaidia hili. Service charge ni kama bima ambayo tunawekeza kwenye shirika la umeme nchini ili liweze kuhudumia wateja wote pale wanapopata hitilafu ya umeme. Sio wateja wote wanaolipa service charge bali na kwa wateja wa kundi la T,Wanaotumia umeme kuanzia unit 75 mpaka 7500 kwa mwezi,Waleo wanaotumia umeme chini ya unit 75 wanalipa kwa bei ya ruzuku mimi nikiwepo mmoja wao naamini kabisa service charge inawasaidia watanzania wenzetu wa hali ya chini.
 
Jumamosi nilifuatilia baada ya kuona service charge hainihusu nikaambiwa service charge ni shs 5800 na hiyo ni lazima.

Nashauri wadau tuunde jumhia ya watumiaji umeme Tanzania ili mambo yetu tuyafuatilie kisheria likiwamo hili. Naomba tuuungane la sivyo TANESCO wataendelea kutunyima umeme huku wakikwapua hela zetu

Sio kweli unachokisema Service Charge bila vat ni Tsh. 5520, ukiweka VAT inakuwa Tsh. 6734.4, na pia sio wateja wote wanaolipa service charge bali ni kwa wateja wa kundi la T,Wanaotumia umeme kuanzia unit 75 mpaka 7500 kwa mwezi,Waleo wanaotumia umeme chini ya unit 75 wanalipa kwa bei ya ruzuku mimi nikiwepo mmoja wao naamini kabisa service charge inawasaidia watanzania wenzetu wa hali ya chini.

Naomba mita namba yako tuangalie matumizi yako ya miezi sita nyuma kama haikuhusu, wateja wengi wamekuwa wakisema hivyo ukija kuangalia matumizi yake unakuta inamhusu, na kama utawekwa tariff 4, ambayo hautalipia service chaji matumizi yako yakizidi unit 75 unit zilizo zidi utanunua kwa gharama ya Tsh. 350 badala ya Tsh 100.

Sio swala la kukimbilia tu inabidi kujiridhisha vya kutosha.
 
Sorry Ni 013 425 225 03

Tumeangalia Mkuu matumizi yako kwa muda wa miezi 3, mwezi wa kumi (10) unit 36.5, mwezi wa kumi na moja (11) unit 68, mwezi wa kumi na mbili (12) unit 47.7.

Ni inbox namba yako ya simu ili niweze kukuunganisha na wahusika waweze kukusaidia.
 
Kwangu bila kushughulikia matatizo ya makato kibao ya tanesco na hizo sijui ndo service charge.... service yenyewe hatuion.Bila kushughulikiwa sijauona ubora wa JPM, wazir husika utusaidie.... ilisemekana bei ingepungua baada ya matumizi ya ges lkn hakuna lolote

What is service charge?

A type of fee charged to cover services related to the primary product or service being purchased. For example, a concert venue may charge a service fee in addition to the initial price of a ticket in order to cover the cost of security or for allowing electronic purchases. Another example would be a fee for using the ATM of a competing bank.
Mimi nadhani Service charge ni muhimu kwa shirika hili la umma kwa sababu zifuatazo

  1. Gharama kubwa za uwekezaji kuanzia kuzalisha,kusafirisha na kusambaza umeme, Gharama hizi kubwa zinapelekea wawekezaji kuona kuwa kuwekeza kwenye umeme kunachelewa sana kulipa (Long payback period), Hivyo shirika hili la umma limejitahidi kufikisha umeme hata maeneo yasiyo na faida hivyo kulichangia service charge ni kulipa nguvu Zaidi
  2. Mteja anapopata tatizo kama nguzo kuanguaka, nyaya kukatika, meter kuharibika mafundi wa TANESCO wamekuwa wakitoa huduma bure kabisa kitu ambacho ingekuwa private company ingeingizwa kwenye gharama za mteja, Service charge imesaidia hili
  3. Service charge mimi naiona kama bima ambayo tunawekeza kwenye shirika la umeme nchini ili liweze kuhudumia wateja wote pale wanapopata hitilafu ya umeme.
  4. Sio wateja wote wanaolipa service charge bali na kwa wateja wa kundi la T,Wanaotumia umeme kuanzia unit 75 mpaka 7500 kwa mwezi,Waleo wanaotumia umeme chini ya unit 75 wanalipa kwa bei ya ruzuku elfu ishirini na saba ( 27000) naamini kabisa service charge inawasaidia watanzania wenzetu wa hali ya chini.
Tuiisadie TANESCO kuweza kutuhudumia vizuri Zaidi,
 
Sio kweli unapopata tatizo unagharamika, hautozwi gharama yoyote. Mteja anapopata tatizo kama nguzo kuanguaka, nyaya kukatika, meter kuharibika mafundi wa TANESCO wamekuwa wakitoa huduma bure kabisa kitu ambacho ingekuwa private company ingeingizwa kwenye gharama za mteja ,Service charge imesaidia hili. Service charge ni kama bima ambayo tunawekeza kwenye shirika la umeme nchini ili liweze kuhudumia wateja wote pale wanapopata hitilafu ya umeme. Sio wateja wote wanaolipa service charge bali na kwa wateja wa kundi la T,Wanaotumia umeme kuanzia unit 75 mpaka 7500 kwa mwezi,Waleo wanaotumia umeme chini ya unit 75 wanalipa kwa bei ya ruzuku mimi nikiwepo mmoja wao naamini kabisa service charge inawasaidia watanzania wenzetu wa hali ya chini.
Koleba/Leadd, inawezekana kwa kuwa wewe ni mfanyakazi wa TANESCO huwezi kukubari kuwa wateja wanagharimika kwa namna moja au nyingine. TANESCO ni kijipu ndugu yangu. Binafsi mwishoni mwa mwaka jana nilipatwa na tatizo la umeme nyumbani kwangu,umeme ulianza tu kwa kuwaka na kuzima kila wakati na baadae kuzima kabisa,ilikuwa majira ya saa 1.00 jioni, nilipiga simu ya huduma kwa wateja na kujibiwa tunawaataarifu mafundi. Nikapiga tena simu saa tatu na nusu usiku kuulizia nikajibiwa mafundi wako njiani, saa sita usiku nikaambiwa mafundi walishakuja wako maeneo yako watafika muda si mrefu! Nikawa mkali kidogo nikaauliza hivi wanatumia usafiri gani tokea saa tatu hawajafika umbali wa kilomita 8? N akwetu ( Mwanza) hakuna hata foleni. Sikuona mafundi mpaka kesho yake ikabidi nitumie mtu anaefahamiana na bosi mmoja wa mafundi nikaeleza scenerio yote ndo akaagiza mafundi wakaenda! Sasa ingekuwa nyumba inawaka moto kwa huduma hizo halafu tunaambiwa ukiwa na tatizo hakuna ghalama ambazo mteja anaingia,hivi kiuchumi ghalama ni pesa tu?
Bado hujaja na point ya kunishawishi kuwa hiyo service charge ni halali. Tujibu na uhalali wa EWURA na REA pia, pamoja na kwamba vilipitishwa na bunge lakini ni halali kweli?
Mtanzania kwa nini ananyonywa mno?
Niulize kitu kingine unisaidie, hivi na Mining companies mnawalipisha haya madude, Service charge,EWURA na REA au wenyewe ni VAT tu?

Asante.
 
Mkuu Kandawe, wateja hawagharamikii chochote, pia inawezekana kunavikwazo vidogo vidogo vinavyotekea katika huduma kwa wateja.

Kitu kikubwa ambacho tuongelee ni namna ya kuboresha huduma kwa wateja, na TANESCO inajitahidi kuboresha kitengo cha Huduma kwa wateja pamoja na cha dharura, pia zilitolewa namba za simu za mameneja wa Wilaya, Mikoa na Kanda iwapo umetoa taarifa na kushindwa kupata huduma kwa wakati unaweza kuwasiliana nao.

Pia ukipiga simu na kutoa taarifa ya tatizo unatakiwa kupewa TB namba ambayo ni kama reference number hii itakusaidia hata unapoenda ngazi ya juu kutoa taarifa inakuwa rahisi sana kuwabana wahusika.

NAMBA ZA SIMU ZA MAMENEJA WA MIKOAKWA KILA KANDA

Namba za simu zilizoko hapa chini ni za Mameneja wa Mikoa mbalimbali. Simu hizi zitatumiwa na wateja kuwasiliana na Meneja husika wa Mkoa pale ambapo tatizo lake halikuweza kutatuliwa na wafanyakazi wa ngazi za chini kupitia dawati la dharura (Emergency Office).
Namba
KANDA YA DSM NA PWANI
1 ILALA Eng. Athanasius Nangali 0689 877 735
2 KINONDONI KASKAZINI Eng. Raymond Seya0689 638 266
3 KINONDONI KUSINI Eng. Henryfrid Byabato 0684 889 884
4 TEMEKE Eng. Jahulula M. Jahulula 0782 926 200
5 PWANI Eng. Martin Madulu 0786 300 139
KANDA YAKASKAZINI
6 ARUSHA Eng. Gaspar Msigwa 0684 885 270
7 TANGA Eng. Richard Mallamia 0786 864 411
8. KILIMANJARO Eng. Maclean Mbonile 0787 365 678
9. MANYARA Eng. Gerson Manase 0788 108 800
KANDA YA ZIWA
10 MWANZA Eng. Sarah Assey 0784902345
11 KAGERA Eng. Hassan Said 0786899998
12 MARA Eng. Obey Sigala 0784418283
13 GEITA Eng. Joachim Ruweta 0787622842
14 SIMIYU Eng. Rehema Mashinji 0784411790
KANDA YA NYANDA ZA JUU KUSINI
15 MBEYA Eng. Francis Maze 0785392312
16 IRINGA Eng. Seraphin Lyimo 0787180143
17 RUKWA Eng. Herini Mhina 0683119480
18 NJOMBE Eng. Julius Sabu 0687230833
KANDA YA KATI
19 DODOMA Eng. Zakayo Temu 0782190080
20 MOROGORO Eng. John Bandiye 0786214499
21 SINGIDA Eng. Gamba Mauggira 0784902383
KANDA YA MAGHARIBI
22 TABORA Eng.Mohammed Abdallah 0789586820
23 SHINYANGA Eng. Mathias Salongo 0786456205
24 KIGOMA Eng. Masigija Lugata 0786405085
25 KATAVI Eng.Emmanuel Kachewa 0784300352
KANDA YA KUSINI
26 MTWARA Eng.Aziz Salum 0687296584
27 LINDI Eng. Johnson Mwigune 0782222997
28 RUVUMA Eng. Patrick Lwesya 0784551944

NAMBA ZA SIMU ZA MAMENEJA WAANDAMIZI WA KANDA
Mameneja Waandamizi wa Kanda watahusika katika kutatua matatizo ya wateja ambayo yameshindikana kutatuliwa Mkoani.
1. Kanda yaKusini
(Mtwara, Lindi & Ruvuma)Bi. Joyce Ngahyoma
0784275936
2. Kanda yaNyandazaJuuKusini
(Mbeya, Iringa, Rukwa&Mjombe) Bi. Salome Nkondola 0787286 599
3 Kanda ya Dar es Salaam naPwani
(KinondoniKaskazininaKusini, Temeke, Ilala &Pwani) Eng. Mahende Mugaya 0784277953
4 Kanda yaKaskazini
(Tanga, Arusha, Kilimanjaro & Manyara) Eng. Stella Hiza
0784902346
5. Kanda yaZiwa
(Mwanza, Kagera, Mara, Simiyu &Geita) Eng. Amos Maganga
0784902324
6. Kanda ya Kati
(Dodoma, Morogoro & Singida) Eng. Deogratius Ndamugoba
0687848400
7. Kanda yaMagharibi
(Tabora, Shinyanga, Katavi & Kigoma) Eng. Engelbert Makoye
0786454611
 
Koleba leadd
hivi huu ujamaa wa kusaidiana kulipa madeni i wa nini? Kila mtu alipe huduma anapoita Tanesco. Kama hawezi kuilipia basi aidha Tanesco watoe msaada au la asubiri mpaka apate uwezo wa kulipia.
Ada hatusaidiani japo kuna watoto wanafukuzwa shule
Nauli hatusaidiani japo kuna watu wanatembea kwa miguu karibu kila siku
Kodi ya nyumba hatusaidiani japo kuna vijana wanalala vibarazani
Pesa ya chakula hatusaidiani japo kuna watu wanalala njaa
..... the list goes on

sasa huu ujamaa wa kwenye service charges msingi wake ni upi? Bahati mbaya swali langu hili mnaliruka na hamtaki kuliaddress maishia kutuambia habari za ujamaa. Ujamaa wa kweli ulishaisha na Nyerere. Enzi hizi kila mtu anakula kwa urefu wa kamba yake!
 
Stefano Mtangoo,
Service charge sio mpaka tatizo likuguse direct nyumbani kwako mfano maeneo unayoishi nguzo kuanguaka na nyaya kukatika, mafundi wa TANESCO wamekuwa wakitoa huduma bure kabisa kitu ambacho ingekuwa private company ingeingizwa kwenye gharama za mteja ,Service charge imesaidia hili
 
Back
Top Bottom