Kwanini Serukamba hakutolewa bungeni?!

Kwanini Serukamba hakutolewa bungeni?!

Tulimumu

JF-Expert Member
Joined
Mar 11, 2013
Posts
14,395
Reaction score
13,266
Nyerere: "waswahili wana mambo ya ajabu. mambo ya kijinga jinga yakisemwa kwa kiingereza, wanashangilia kana kwamba ni mambo mema"

Hayo ni baadhi ya maneno aliyoyasema baba wa taifa Mwl Julius K. Nyerere katika moja ya hotuba zake.
Tusi alilolitoa Serukamba ndio tusi kubwa kuliko yote yaliyowahi kutolewa bungeni mpaka sasa. Tofauti na mengine yeye lake amelitoa kwa kiingereza kiasi kwamba naibu spika ameliona ni jema hivyo kutomchukulia hatua yoyote.

Hata majadiliano yanayoendelea sasa miongoni mwa wananchi na viongozi ni kuhusu "utovu wa nidhamu" wa Tundu Lissu wa kuomba miongozo na taarifa kila mara hivyo kutimuliwa bungeni na wenzake waliokuwa wakipinga kitendo cha naibu spika kumtoa nje. Hili la Serukamba halizungumzwi kama ni tusi kuu bungeni.

Tatizo ni kama alivyosema Nyerere, katukana kwa kiingereza hivyo spika na naibu wake hawaoni kuwa ni tusi. Waziri mkuu haoni kuwa ni tusi. Aibu!
 
...Huwezi Jua...Labda Mheshimiwa Naibu haelewi maana ya 'F**k You', maana lilipotolewa hakuonekana hata kushituka angalau kwa kumuangalia tu Mropokaji!
 
Jamani mimi kidogo kiingereza kinanipiga chenga, sasa naomba mnisaidie tafsiri sahihi ya KISWAHILI katika maneno haya ambayo yote nimeyasikia kutoka mjengoni Dodoma

1. FAKI YU
2. IMPOTENTI

Nawasilisha
 
Jamani mimi kidogo kiingereza kinanipiga chenga, sasa naomba mnisaidie tafsiri sahihi ya KISWAHILI katika maneno haya ambayo yote nimeyasikia kutoka mjengoni Dodoma

1. FAKI YU
2. IMPOTENTI

Nawasilisha
Impotent ilishaelezewa humu mara kibao.

Kwa umri ulionao humu jamvini natarajia matumizi ya google hayatakuwa tatizo kwako.
 
Lol! inabidi nicheke hata kabla ya kukoment!! JF hebu naomba tuelezwe maana ya na matumizi Ya Fak u? nahisi wakati mwingine hakuna tofauti na jinsi ilivyotafsiliwa neno '''Impotenti'' Angalizo ni sentensi kama hizi ambayo neno 'Fak u' limetumika! I dont give a f**k or dont F**k with me!!!! au ndo mnagoma na kung'ang'ania maana moja ya tafsili ya hilo neno kiswahili kama CCM wanavyolalamika?........ Ila jamaa ilimtoka KAVU KAVU.... nadani ya KIJIWE aka bunge!!! nomaaaa!
 
Ukosefu wa busara wa hali ya juu kabisa,watu wazima wenye heshima zao maneno ya hovyo hovyo tu yanawatoka pasipo ata na staha.
 
wajameni na Mh.Serukamba alimaanisha ivi- "go to hell."Aksante
Nyerere: "waswahili wana mambo ya ajabu. mambo ya kijinga jinga yakisemwa kwa kiingereza, wanashangilia kana kwamba ni mambo mema"

Hayo ni baadhi ya maneno aliyoyasema baba wa taifa Mwl Julius K. Nyerere katika moja ya hotuba zake.
Tusi alilolitoa Serukamba ndio tusi kubwa kuliko yote yaliyowahi kutolewa bungeni mpaka sasa. Tofauti na mengine yeye lake amelitoa kwa kiingereza kiasi kwamba naibu spika ameliona ni jema hivyo kutomchukulia hatua yoyote.

Hata majadiliano yanayoendelea sasa miongoni mwa wananchi na viongozi ni kuhusu "utovu wa nidhamu" wa Tundu Lissu wa kuomba miongozo na taarifa kila mara hivyo kutimuliwa bungeni na wenzake waliokuwa wakipinga kitendo cha naibu spika kumtoa nje. Hili la Serukamba halizungumzwi kama ni tusi kuu bungeni.

Tatizo ni kama alivyosema Nyerere, katukana kwa kiingereza hivyo spika na naibu wake hawaoni kuwa ni tusi. Waziri mkuu haoni kuwa ni tusi. Aibu!
 
Naibu Spika ni Afisa wanyamapori kiprofesheni, hivyo tusimlaumu sana wajameni. Kitendo cha mnyama mmoja aliyesimama kumnyea mnyama mwingine aliyekaa au aliyejilaza ni kawaida sana tu kule mbugani na zizini.
 
ukitukana kwa lugha ngeni aliyetukanwa anaweza akadhani hujatukanwa. Nyerere alishawahi kusema kuwa kuna waswahili jambo likisemwa kwa kkingereza basi wanaona ni la maana sana
 
Hivi Ndugai si alikuwa mesenja tu mle bungeni,kutumwa vikaratasi na kina Mzindakaya,ubunge aliupatapataje?!
 
Naibu Spika ni Afisa wanyamapori kiprofesheni, hivyo tusimlaumu sana wajameni. Kitendo cha mnyama mmoja aliyesimama kumnyea mnyama mwingine aliyekaa au aliyejilaza ni kawaida sana tu kule mbugani na zizini.
Ili uwe Mbunge au Spika unatakiwa uwe na sifa gani?
Hakuna sehemu inayotaka uwe na sifa km za TUNTEMEKE SANGA (R.I.P.}
Hakuna sehemu inayotaka uwe na umri mkubwa
Unachotakiwa uwe na Umri wa miaka 18 na Elimu ya Msingi
sasa sijui Ndugai ana tofauti ipi au mnalazimisha tu?
Hakuna Mbunge yeyote ila serukamba tu ndiye aliyeomba Radhi kwa neno lilomtoka la Tusi kati ya Wabunge wote waliotamka Matusi ndani ya Ukumbi kwa hiyo sionoi haja ya kushupalia mtu aliyekiri alipotoka licha ya kuwa kuna mtu alimsababishia hasira hizo
(Star Tv Naibu Spika kakiri humo Ukumbini huwa kuna matusi mengi sana amabayo vinasa sauti viakuwa mbali kunasa)
quote_icon.png
By saronga
Jamani naomba tafsiri sahihi ya KISWAHILI katika maneno haya ambayo yote nimeyasikia kutoka mjengoni Dodoma
1. FAKI YU ------------------- Maana yake unakandamizwa
2. IMPOTENTI -------------------- Maana yake Huwezi kukandamiza
 
  • Thanks
Reactions: smz
Hakutolewa kwa sababu ni mbuge wa CCM, chama dola! Ukiwa CDM ukiomba mwongozo mara nyingi-out!
 
Hivi Ndugai si alikuwa mesenja tu mle bungeni,kutumwa vikaratasi na kina Mzindakaya,ubunge aliupatapataje?!
Ndugu yangu, wapo watu wengine walipewa tu ubunge hata hawahusiki wala hawakustahili kivile. Cheki waliomo:-
- Wapo pia waimba kwaya tu,
- wamo waganga wa kienyeji tu,
- wamo watukanaji wazuri tu kama huyu,
- wapo wazinzi (kumbuka kule Ziba - Igunga walikofumaniana),
- wapo majambazi wanaohutubia mikutano ya hadhara na silaha nje nje viunoni mwao,
- wapo wezi wa mataulo ya gesti,
- wamo makahaba na wezi wa wake/waume za watu,
- wapo wala rushwa bila aibu (tena hawa ni wengi tu),
- wamo wasinziaji wazuri tu, naskia wanalala bila kukoroma mjengoni. Ukikoroma unakuwa umevunja kanuni!
Kwa mchanyanto huu, hatuwezi kujadili issue serious za kitaifa. Wao kazi yao ni kukuondoeni kwenye mjadala wa issue nzito kwa kuchomeka jambo linaloudhi tu.
 
Matusi ndani ya ukumbi wa Bunge ni mali halali ya CCM.
Tabia mbaya zote ni mali ya CCM
Mwana CCM hawezi kutolewa ukumbini kwa kuwa matusi ni mali yao, hata akitolewa ukumbini ataenda kutukana nje kama alivyofanya Living Stone Lusinde kule Arumeru
 
Ili uwe Mbunge au Spika unatakiwa uwe na sifa gani?
Hakuna sehemu inayotaka uwe na sifa km za TUNTEMEKE SANGA (R.I.P.}
Hakuna sehemu inayotaka uwe na umri mkubwa
Unachotakiwa uwe na Umri wa miaka 18 na Elimu ya Msingi
sasa sijui Ndugai ana tofauti ipi au mnalazimisha tu?
Hakuna Mbunge yeyote ila serukamba tu ndiye aliyeomba Radhi kwa neno lilomtoka la Tusi kati ya Wabunge wote waliotamka Matusi ndani ya Ukumbi kwa hiyo sionoi haja ya kushupalia mtu aliyekiri alipotoka licha ya kuwa kuna mtu alimsababishia hasira hizo
(Star Tv Naibu Spika kakiri humo Ukumbini huwa kuna matusi mengi sana amabayo vinasa sauti viakuwa mbali kunasa)
quote_icon.png
By saronga
Jamani naomba tafsiri sahihi ya KISWAHILI katika maneno haya ambayo yote nimeyasikia kutoka mjengoni Dodoma
1. FAKI YU ------------------- Maana yake unakandamizwa
2. IMPOTENTI -------------------- Maana yake Huwezi kukandamiza
Nilichojadili sio sifa ya kuwa Mbunge. Mjadala ni busara ya mtu. Kama Naibu Spika busara yake ilimtuma kutokereka na neno F*#@ YOU lililo nje ya kanuni ambalo alilisikia vizuri tu wala asishituke, badala yake akakereka dhidi ya mtu anayeomba mwongozo kwa mujibu wa kanuni, nadhani busara yake inaweza kuonekana kirahisi.
Halafu unayemsema aliomba radhi kwa kusema F*#@ YOU, alifanya hivyo lini?
By the way, Ukiomba radhi ndio unakuwa hukusema F*#@ YOU?
 
Mr Presedent You can't believe him!!! SERUKAMBA ni GAMBA mwenzao wamfukuze iliweje? kwa mtazamo wao hawatajki kujiabisha,ila wamesahau kwa kufanya vile ndio wanajimboa vyakutosha,UJUMBE WA MUHIMU KWAKO MIMI NITAKUSHANGAA KAMA NAWE BADO UNAIPENDA CCM KWA JINSI HIO TAYARI UTAKUWA NI MZOGA.
 
Wabunge wa CCM ni masikini wa hoja lakini wanautajiri wa matusi si wabunge tu bali hata Rais wao ni mtukanaji mzuri,ninacho shangazwa mm ni uzandiki wa (ana makinda) kwa kulala mika kuwa ametukanwa mwembe Yanga ili hali matusi ameyazoea,CDM hatuto rudishwa nyuma na matusi au kupindishwa kwa kanuni ndani ya bunge "Ni bora vita yenye kusaka haki kuliko amani yenye kunyonya,kuua, kuteka nyara na kunyimana haki ya kidemokrasia ndani ya bunge" DR. slaa is unforgetable.
 
wabunge wa ccm hawana elimu na pia sheria hawaijui vizuri kwa hiyo wamefika bungeni kwa uswaiba wa viongozi wa juu
 
Back
Top Bottom