Kwanini Serikali isilipe fidia simu feki?

Mpalakugenda

JF-Expert Member
Jun 2, 2015
3,839
4,065
Kufuatia kutangazwa kwa kuzimwa kwa simu feki,na hasara moja kwa moja kumkuta mwananchi,

Je serikali kwa nini isiwajibike kurudishia gharama wote watakao athirika na zoezi hilo. Sababu
1. Serikali ndio ilikuwa na jukumu la kudhibiti bidhaa hizo, lakini ilishindwa hivyo wananchi wake tayari wameathirika kiafya.

2. Wameshakusanya kodi ya hizo simu.
 
Nilipoona Title nikajua tayari serikali imekubali kulipa fidia, nikajisemea moyoni kesho nitaenda kununua feki ili wanilipe. Kufungua, kumbe unauliza swali!!!
 
Wale wapuuzi wanaouza simu fake eti wanalalamika kwa kusema serikali ingewaongezea muda ili stock yao iishe halafu hizo gharama za simu zikizimwa maumivu ayapate mtanzania? Na pia je inakuwaje serikali inakiri kuna simu fake wakati tuna taasisi ya FCC ambayo moja ya kazi zake ni kuzibiti huduma kwa mtumiaji ili asidhurike kwa kupata kitu substandard.Zamani airport FCC walikuwa wanakagua na kutetekeza bidhaa fake sasa sijui nini kimetokea masimu fake kila kona sasa.
 
Hiyo heading yako ongeza na alama hii???????? Nilifikiri watoa taarifa kuwa visimu vyetu havitazimwa kumbe mchewww
 
Hapo nimekupenda ghafla.
wewe unadhani kila mtanzania ana uwezo wa kujua simu feki?a vyombo vyote vinvyohusika kzi yao ni ipi. tunalipa kodi watulinde. nashuri serikali kwa kutokulinda watu wakuziwa vitu feki wangewka utaratibu wa kuhakiki simu zinazoingizwa na hizo wlizouziwa feki hazitachukua muda kwani zinkufaga zenyewe baada ya muda mfupi.kwa hiyo wasizifungie. waendelee kupata kodi yao kwa matumizi ya hizo simu.
 
TFDA wanapita na kukagua bidhaa feki na kuziharibu ili zisifike kwa mlaji na kula sumu kwani ni wajibu wao.
Sasa inakuwaje TBS wanakiri kuwa kuna simu fake na hawachukui hatua wakatizimezagaa
 
Mtanzania wa kawaida anapata hela yake kwa tabuu anaenda mjini tena dukani anauliza bei ya simu anapewa simu risiti na warranty leo unasemaje kuna simu feki inhali hukuzuia wala kutoa elimu tcra ni zaidi ya jipu
 
TFDA wanapita na kukagua bidhaa feki na kuziharibu ili zisifike kwa mlaji na kula sumu kwani ni wajibu wao.
Sasa inakuwaje TBS wanakiri kuwa kuna simu fake na hawachukui hatua wakatizimezagaa

mteja amenunua simu kihalali na akapewa risiti.
leo mteja huyohuyo azimiwe simu inakuwa uonevu... kwa nn na mfanyabiashara asichukuliwe hatua kwa kuuza vitu feki?.
 
Kufuatia kutangazwa kwa kuzimwa kwa simu feki,na hasara moja kwa moja kumkuta mwananchi,

Je serikali kwa nini isiwajibike kurudishia gharama wote watakao athirika na zoezi hilo. Sababu
1. Serikali ndio ilikuwa na jukumu la kudhibiti bidhaa hizo, lakini ilishindwa hivyo wananchi wake tayari wameathirika kiafya.

2. Wameshakusanya kodi ya hizo simu.
Hii ni Serikali ya Awamu ya Tano. Watafute serikali awamu ya nne uwapelekee haya malalamiko.
 
TFDA wanapita na kukagua bidhaa feki na kuziharibu ili zisifike kwa mlaji na kula sumu kwani ni wajibu wao.
Sasa inakuwaje TBS wanakiri kuwa kuna simu fake na hawachukui hatua wakatizimezagaa

Endelea kununua simu fake eti TBA wapo!! Anyway waandikie Barua za malalamiko
 
Endelea kununua simu fake eti TBA wapo!! Anyway waandikie Barua za malalamiko
Majibu ya kitoto haya. Bidhaa zote kutoka nje zinapoingia vipo vyombo vya serikali vyenye utaalam kuchunguza ubora wake na kuhakikisha kodi inalipwa. Jee ina maana serikali kumbe inakusanya kodi hata kwa bidhaa fake ili kupata mapato bila kuangalia madhara kwa mlaji? Hao wanaonunua simu fake wanajikuta wanazinunua kutoka katika maduka yanayotambuliwa na bidhaa hizo wanaamini zimekaguliwa ubora wake.
Mbona kwenye madawa, vipodozi na vyakula wako makini?au ni kwa vile kuna kuooteza maisha?
Siku nyingine usijibu kama unetoka usingizini
 
Hutakiwi kununua simu feki,hiyo lni loss ya wenya maduka na wateja wao
 
Hivi leo hii J5 tutasikia nani kafukuzwa kazi...ziara ya kushtukiza wapi....jipu gani limetumbuliwa....malalamiko gani toka serikalini...waziri gani wazamani anachunguzwa.....Tubadilishe style.....Sasa hatutaki Reasons tunataka Results.
 
Back
Top Bottom