Kwanini Serikali isiagize Farasi tukawapandikiza katika Mbuga zetu, na wengine tukawafuga wakatusaidia katika shughuli zetu za Uchumi

Mbona polisi wanao na hawawatelekezi vipi arusha wasiwepo unajua kuwa farasa,punda na pundamilia ni jamii moja tu .whywengine wawepo wengine wasiwepo halafu hizo gharama unazotaja ni zipi?
Kama punda na farasi ni sawa mbona hatuwatumii punda kufanya kazi za farasi? Farasi kuwatunza ni shughuli pevu inasemekana. Wana diet yao ambayo huku ni ngumu kuikamilisha. Halafu kuna tofauti kubwa ya punda na farasi.
 
Hiyo diet gani itaje sasa?
 
Mbona punda tunao wengi maeneo mengi nchini? Rukwa, Katavi na Songwe hata ng'ombe hutumika: wanalima, wanasafirisha mizigo na hata kuchota maji
 
Nenda shamba lipo Mbeya nadhani eneo wanaita kitulo. Wapo kule wanafugwa....ingawa tunaweza ongeza idadi....
 
Katika viitu navyovijua mnyama huyu najua kumtumia na kumuendesha vizuri tu
Najua tuko wachache sana wnye ujuzi wa kumtumia mnyama huyu...acha nijipe kongole

Ova
View attachment 1708601
Hii mbegu ndogo. Aiseee kuna farasi wameenda hewani.... Yaani akinyanyua kichwa chake ukampima urefu ngoma inasoma futi saba huko na zaidi.... Halafu ana bonge la mwili, bonge la kwato bonge la tako kama Sanchoka.
 
Mjerumani aliposhindwa vita vya pili vya Dunia(Ww2) aliwatelekeza farasi jangwani Namibia waliokuwa wanatumika katika vita hivyo. Hivi sasa wamekuwa wanyama wa mwitu na wamezaliana sana na hakuna anayewahudumia.,na ni mazingira ya jangwani.
 
Hata mimi nilitaka kuuliza kama wewe yaani dunia inaenda mbele halafu sisi turudi nyuma miaka 500 kwa kutumia farasi kutatua changamoto za sasa!!
 
Ufugaji wa farasi Africa haiwezekani sababu tropical climate ina vectors wa maradhi ambayo farasi hawezi vumilia ,kwenye tropical climate kuna mbung'o (tse tse flies) wanaosababisha ugonjwa wa Trypanosomiasis ,ugonjwa hatari kabisa kwa farasi ,

Sio kwamba haijwahi jaribiwa kufuga farasi Africa ,hawezi kuishi huku , anaishi maeneo ya baridi ,maeneo ya baridi huwezi kukuta mbu wala mbung'o hawawezi zaliana huko.

Kadiri unavyotoka ikweta kwenda kaskazini na kusini ndivyo Hali ya hewa inavyobadilika na kuwa baridi,na ndivyo uwezekano wa kuwepo mbu na mbung'o unapungua KWA hiyo farasi wanaweza kufugika south africa (wanafugwa) na north africa huko morocco (wanafugwa)
 
Nyuzi kama hizi mods muwe mnazifuta maana zinaweza zikaonwa na yule msemakweli wa Chato akasitisha SGR ili anunue farasi

Utamsikia na ili sauti yake "I prefer horses over SGR & BOMBARDIER"
 
Wakoloni walishamtoa farasi afrika kwasababu moja ni chanzo cha usafiri kama mpka leo farasi wangekuwa wengi afrika basi vyombo vya usafiri vingekuwa vichache na mabeberu wasingeuza magari,baskeli, na pikipiki
 
Nyuzi kama hizi mods muwe mnazifuta maana zinaweza zikaonwa na yule msemakweli wa Chato akasitisha SGR ili anunue farasi

Utamsikia na ili sauti yake "I prefer horses over SGR & BOMBARDIER"
Hahahahahha
 
Nenda hata hapo Iringa kwa mzungu mmoja anaitwa Philips, anao pale mkuu.
 
Mbona polisi wanao na hawawatelekezi vipi arusha wasiwepo unajua kuwa farasa,punda na pundamilia ni jamii moja tu .whywengine wawepo wengine wasiwepo halafu hizo gharama unazotaja ni zipi?
Kama huwezi kununua pikipiki, basi sahau habari ya farasi. Bei yake sawa na pikipiki 3-4
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…