Kwanini Serikali isiagize Farasi tukawapandikiza katika Mbuga zetu, na wengine tukawafuga wakatusaidia katika shughuli zetu za Uchumi

Mbona polisi wanao na hawawatelekezi vipi arusha wasiwepo unajua kuwa farasa,punda na pundamilia ni jamii moja tu .whywengine wawepo wengine wasiwepo halafu hizo gharama unazotaja ni zipi?
Kama punda na farasi ni sawa mbona hatuwatumii punda kufanya kazi za farasi? Farasi kuwatunza ni shughuli pevu inasemekana. Wana diet yao ambayo huku ni ngumu kuikamilisha. Halafu kuna tofauti kubwa ya punda na farasi.
 
Kama punda na farasi ni sawa mbona hatuwatumii punda kufanya kazi za farasi? Farasi kuwatunza ni shughuli pevu inasemekana. Wana diet yao ambayo huku ni ngumu kuikamilisha. Halafu kuna tofauti kubwa ya punda na farasi.
Hiyo diet gani itaje sasa?
 
Mbona punda tunao wengi maeneo mengi nchini? Rukwa, Katavi na Songwe hata ng'ombe hutumika: wanalima, wanasafirisha mizigo na hata kuchota maji
 
Nenda shamba lipo Mbeya nadhani eneo wanaita kitulo. Wapo kule wanafugwa....ingawa tunaweza ongeza idadi....
 
Katika viitu navyovijua mnyama huyu najua kumtumia na kumuendesha vizuri tu
Najua tuko wachache sana wnye ujuzi wa kumtumia mnyama huyu...acha nijipe kongole

Ova
View attachment 1708601
Hii mbegu ndogo. Aiseee kuna farasi wameenda hewani.... Yaani akinyanyua kichwa chake ukampima urefu ngoma inasoma futi saba huko na zaidi.... Halafu ana bonge la mwili, bonge la kwato bonge la tako kama Sanchoka.
 
Mjerumani aliposhindwa vita vya pili vya Dunia(Ww2) aliwatelekeza farasi jangwani Namibia waliokuwa wanatumika katika vita hivyo. Hivi sasa wamekuwa wanyama wa mwitu na wamezaliana sana na hakuna anayewahudumia.,na ni mazingira ya jangwani.
 
Wazo la kuleta Farasi kwa wingi na kuwafuga kwa lengo la kutumika kama nguvukazi mbadala wa magari, yaliyo onekana kuwa na gharama kubwa wakati huo, liliwahi kutekelezwa na Edward Moringe Sokoine akiwa waziri mkuu kwenye awamu ya kwanza ya uongozi wa kitaifa. EMS alifanya ziara nchini Australia na kuliuza wazo lake huko na kufanikiwa kupata uungwaji mkono na hatimaye farasi kadhaa kuletwa, na kutawanywa kwenye baadhi ya mikoa.

Ninachokumbuka ni kuwa Farasi walioletwa walianza kufa kwa kasi ya ajabu na ikaelezwa kuwa wengi walikufa kwa uchovu wa safari na magonjwa. Maendeleo ya mradi huo hayakuwekwa hadharani na hivyo kupotea kimya kimya.... Lakini najiuliza tu kama kweli kuna tija kununua farasi ili wafanye kazi inayoweza kufanywa na tractor, ukizingatia kuwa bei ya farasi iko juu pengine kufikia bei ya gari dogo..... Tuchemshe bongo hapa!!. 🤔
Hata mimi nilitaka kuuliza kama wewe yaani dunia inaenda mbele halafu sisi turudi nyuma miaka 500 kwa kutumia farasi kutatua changamoto za sasa!!
 
Habari zenu wana jf.

Poleni sana na mapumziko ya weekend hii bila kusahau kuwakumbusha kuhusu suala zima la kuendelea kujichunga kwa kuchukua tahadhari dhidi ya ugonjwa wa CORONA. Hali sio nzuri.

Ndugu zangu na wazo hivi Serikali inashindwa nini kuanzisha uzao wa mnyama aina ya farasi nchini ili awe kutusaidia hasa sisi watu wa vijijini ambao usafiri huku ni shida tupu!.Huenda kungekuwa na farasi wa kutosha kila mtu angenunua wake kwa bei nzuri tukawatumia hata kusafirisha mazao kutoka mashambani ambako miundombinu ni mibovu kupindukia.

Binafsi mimi si mtaalamu wa wanyama kama farasi ila nimekuwa nikiwaona kwenye tv na documentary kibao wakitumika ktk shughuli mbalimbali za uzalishaji hasa nchi za Ulaya na Amerika sijajua tatizo liko wapo sisi tunashindwa kupandikiza wanyama hawa hapa kwetu ilhali tuna eneo kubwa lenye ardhi yenye rutuba ya kitosha na hali ya hewa tofauti .

Mara ya kwanza nilijua shida labda hawawezi kuishi kwenye maeneo ya joto watakufa lakini nashangaa mbona Polisi pale Makao Makuu Kurasini wanao na wanawatumia ktk doria mbalimbali. Kwa uelewa wangu farasi ni jamii ya punda ambao huku vijijini pia wapo japo kwa kiai kidogo kutokana na mchina kuleta mambo ya kuwachinja ila wanaishi safi tu.

Wakati mwingine nikajua labda madawa yake ni ghali lakini mbona mifugo karibia yote madawa yake ni ya kawaida tu naamini hata wao wanatumia madawa kama haya haya tunayotumia kutibu mifugo mingine.

Nikajua labda ni ghali sana kununua hao farasi lakini Serikali ikinunua wachache then ikawapadikiza ktk kila mbuga si watazaliana na watakuwa wengi na wananchi watauziwa watusaidie kutubebea mizigo miaka nenda rudi Mzungu anatumia farasi hadi leo kubebea mizigo na usaifiri katika maeneo korofi .

Nikajua labda hula majani tofauti na yalipo Tanzania lakini kama ishu ni majani si tunachukua Ulaya tunakuja kuyalima hapa tunakuwa tunawalishia

Wito wangu kwa Serikali; Kamwe haitotokea imalize changamoto ya miundombinu vijijini na hii imepelekea wakati mwingine wakulima kupata hasara kwa mazao yao kuharibikia mashambani na kurudisha kipato cha mkulima na uchumi kwa ujumla

Ushauri wangu ni bora kutumia mbinu hii ya kuanzisha uzao wa farasi wananchi wauziwe watusaidie kurahisha maisha watu tunateseka kwakweli. Bei za magari na mapikipiki hazishikiki kwa watu wakipato cha chini

Au mnaonaje wadau karibuni tuchangie.

ASANTE.
Ufugaji wa farasi Africa haiwezekani sababu tropical climate ina vectors wa maradhi ambayo farasi hawezi vumilia ,kwenye tropical climate kuna mbung'o (tse tse flies) wanaosababisha ugonjwa wa Trypanosomiasis ,ugonjwa hatari kabisa kwa farasi ,

Sio kwamba haijwahi jaribiwa kufuga farasi Africa ,hawezi kuishi huku , anaishi maeneo ya baridi ,maeneo ya baridi huwezi kukuta mbu wala mbung'o hawawezi zaliana huko.

Kadiri unavyotoka ikweta kwenda kaskazini na kusini ndivyo Hali ya hewa inavyobadilika na kuwa baridi,na ndivyo uwezekano wa kuwepo mbu na mbung'o unapungua KWA hiyo farasi wanaweza kufugika south africa (wanafugwa) na north africa huko morocco (wanafugwa)
 
Nyuzi kama hizi mods muwe mnazifuta maana zinaweza zikaonwa na yule msemakweli wa Chato akasitisha SGR ili anunue farasi

Utamsikia na ili sauti yake "I prefer horses over SGR & BOMBARDIER"
 
Wakoloni walishamtoa farasi afrika kwasababu moja ni chanzo cha usafiri kama mpka leo farasi wangekuwa wengi afrika basi vyombo vya usafiri vingekuwa vichache na mabeberu wasingeuza magari,baskeli, na pikipiki
 
Nyuzi kama hizi mods muwe mnazifuta maana zinaweza zikaonwa na yule msemakweli wa Chato akasitisha SGR ili anunue farasi

Utamsikia na ili sauti yake "I prefer horses over SGR & BOMBARDIER"
Hahahahahha
 
Mbona polisi wanao na hawawatelekezi vipi arusha wasiwepo unajua kuwa farasa,punda na pundamilia ni jamii moja tu .whywengine wawepo wengine wasiwepo halafu hizo gharama unazotaja ni zipi?
Kama huwezi kununua pikipiki, basi sahau habari ya farasi. Bei yake sawa na pikipiki 3-4
 
4 Reactions
Reply
Back
Top Bottom