Kwanini Serikali inaonea Wafanyabishara Kahama?

Mzee

JF-Expert Member
Joined
Feb 2, 2011
Posts
13,620
Reaction score
5,863
Habari za hapa Jukwaani.

Serikali ya Halmashauri Manispaa ya Kahama wanaendesha zoezi la kukagua bidhaa zilizoExpire pamoja na bidhaa ambazo haziruhusiwi kuuzwa. Ni jambo jema sana.

Ijumaa walipita dukani, wakakuta soda 6 za aina tofauti katika freezer pamoja na Blue band kopo 1 zikiwa zimeexpire, kila moja wakanipiga faini ya laki 1, Jumla ya faini Laki 7 i.e 700,000/=.

#1 Ni jambo jema sana kuzungukia na kuona mazingira tunayofanya kazi, lakini wanapokuta kosa wanapiga faini za kuumiza ili kuruhusu Mazingira ya Rushwa?

Je, Serikali yetu ni katili namna hii?

#2 Nilijarbu kurepoti tukio langu siku hiyo hoyo kupitia Portal ya Serikali ya kutoa malalamiko lakini hakuna majibu mpaka leo, na wanaendelea kupiga faini za kuumiza ili kujenga Mazingira ya Rushwa.

#3 Hakuna mtu anataka kuuza bidhaa iliyoexpire maana hata sisi hatupendi kununua bidhaa zilizoexpire. Mnapokuta makosa jaribu kupiga faini ambazo zitatoa elimu lakini sio kumaliza Biashara. Unapiga faini ya laki 7, unataka nifunge Biashara?

NB: Endeleni kuja na kiburi chenu, kuna siku tutawavizia. Haiwezekani mtuonee namna hii.

Nawasilisha.
 
Kwa nchi za wenzetu ukiuza product ilio expire ni Death penalt inakungoja, faini tu wakati wewe ni sawa na muuaji?
 
Ilishanikuta hii, mm nilifungua duka sehemu kwa mara ya kwanza na wauzaji wa blue band wakapita nikanunua mzugi wa kutosha pasipokuangalia expiry date yake. Ebwaaana! Baafa ya miezi mitatu kuja kuchungulia kumbe ishaexpai, nilipata hasara kubwa sana. Na hawa wauzaji wakikuona mgeni wanakubambika makusudi kabisa
 
Daaah kiongozi nani atawatetea walaji kwa kuuza vitu vibovu tayri.
 
Mmuuaji Sanaa wewe,uuze vilivyoexpire afu unakuja kututangazia hapaaa.Yaan wangekuweka serooo uuumwe mbuu week 3, bila kuingiza ata bukuuu daadek.
 
Na ww kwann huuze vitu vilivyo isha muda wa matumizi huoni ya kwamba unahatarisha maisha ya watu?
Si bora hata Tz umepingwa faini , nchi nyingine kosa Kama hilo unaenda jera miaka isiyo pungua kumi.
 
Back
Top Bottom