Kwanini serikali inamhofia ''Nyoka wa makengeza''

Kwanini serikali inamhofia ''Nyoka wa makengeza''

bwana eeh ayo ayazungumziki,nashindwa ata cha kuongea let me pass as a housfly in da fire
 
Afanye hivi utawala huu, ntaamini kweli ni untouchable

Hata akifanya leo hakuna mwenye ubavu wa kumgusa usidhani serikali ya leo imejitenga na ya jana mkuu,hata akiamua kuyazungumza ya awamu ya tatu basi serikali hii nayo haitokua salama kwa kifupi JOKA LA MAKENGEZA ni la kuliangalia tu kwa mfumo wa chama kikongwe ni UNTOUCHABLE.
 
Wakimwagia ugali na yeye "nyoka wa makengeza" atawamwagia mboga zao na atatoboa sufiria hakitopikwa kitu.

Hapo lazima aogopwe...
 
Jamaa liliweka pingamizi la kutohojiwa na tume ya maadili!Hapo nikajua basi,mchezo umeisha
Na baada ya pingamizi lake kutupiliwa mbali sijui nini kilifuata!!
 
Huu ndiyo ukweli usiopingika. Huyu fisadi anawajua mafisadi wote ndani ya chama cha mafisadi. Atakayemgusa tu kuhusu ufisadi wake wowote ule naye atalala naye mbele kwa kuanika maovu yake. Hivyo wanamuhofia sana.

kwa sababu anaujua wizi wote wa magamba,wakimwaga mboga anamwaga ugali...too late to balali him.
 
Chenji ya escrow yupo, Tibaijuka kawajibishwa, Chenji ya Rada yupo akasema vijisenti. Mikataba mingi ya ovyo, I PTL mfano mmoja. Leo ni mwenyekigoda wa chombo cha kutunga sheria, wabunge kwa wengi wao wakamhofia. Naomba kujua nguvu hiyo anatoa wapi? Nyuma yake kuna nini? Maana naona Mbele ya serikali ye ni kama chatu, Mbwa anafyata mkia. Team LUMUMBA BOOK 7PROJECT MJE NA HOJA SIO JAZBA. Cc:Jingalao, Simiyu Yetu, Ritz, Lizaboni, Shindu Namwaka.,Lotima.
Labda umesahau kuwa huyu na Lowassa walikuwa kapu moja
 
Watu wengi tunaowaongelea ufisadi Mkubwa huenda tuhuma dhidi yao si za kweli, au they played it so smart that kuwakamatia chini ni vigumu. Kwa nini wametajwa miaka nenda rudi na hamna wafanywalo?
 
Back
Top Bottom