Bornventure
JF-Expert Member
- Jan 29, 2017
- 529
- 523
http://www.jamiiforums.com/mobile-gallery/312e13567a8e79e7565b0948959c70a0.jpg[/IMG
Nimeambatisha copy ya form ukiangalia heading yake inajieleza wazi.
Mimi ni mmojawapo wa wahanga wa kuchukuliwa kwa ardhi yangu kutokana na mradi wa ujenzi wa barabara kutoka Matema (Kyela , ziwa Nyasa) to Kyela njia panda ya Ipinda.
Tumefanyiwa tathmini nyiingi sana na tukajazishwa form za mkataba wa fidia ya mali zetu ikiwemo miti ya kokoa ambayo ndiyo nguzo ya uchumi huku kwetu, nyumba na ardhi.
Baadaye viongozi wa mkoa, wakaja na kutusihi turuhusu ujenzi uanze bila fidia ili tusicheleweshe mradi halafu malipo yatafuata . Tukakubali.
Cha kushangaza majuzi amekuja Mkuu wa Wilaya na kututangazia kwamba hakuna malipo. Mara Sijui wengine walifata barabara na wengine iliwafuata.
Kwa Kweli nimekosa imani saana na serikali hii. Tafadhali msaada jamani tusaidieni wana Kyela kutupazia sauti tunataka kudhulumwa. Tumerudishwa nyuma sana kimaendeleo halafu tudhulumiwe!!?
Nina mengi Ila kifupi ni haya.