Kwanini serikali haitoi vibali vya kuingiza sukari na mahindi ndani ya nchi?

mwenda wazimu

JF-Expert Member
Feb 20, 2017
819
1,278
Habari,

Nimekuja kwenye jukwaa hili nikiamini kuna wataalamu wa kutosha na wenye uzoefu na mambo ya uchumi, kwa sasa serikali yetu aitoi vibali kwa watanzania kuingiza mahindi/sukari ndani ya nchi, kwa sasa ukiingiza mahindi au sukari ni kama umeingiza bangi mwisho wako utakuwa ni mbaya.

Nachotaka kufahamu hapa ni nini au kitu gani serikali inakwepa au itapata kupitia katazo kama hili kwasababu najaribu kujiuliza. Taratibu za kuingiza kitu ndani ya nchi zina husisha taasisi tofauti tofauti kama TRA, TBS, TFDA, TPA, lakini zinakuja kuingia baadhi ya wizara kutokana na nuture ya mzigo kwa mfano maindi wizara ya kilimo lazima iingie hapa ili kutoa kibali cha kuingiza ndani ya nchi kisha wafate TFDA ili wapime maindi yenyewe kama yanafaa kwa binadamu kisha waje TRA ili ulipe ushuru wa unacho ingiza kisha bandari na mteja kwenda kufanya biashara.

Lakini serikali haitaki watu waingize mahindi hapa nchini, licha ya kwamba wafanya biashara watalipa ushuru kwa serikali bado hawataki, ni nini wanacholinda kwenye makatazo haya ndo ninalotaka kujua kwasababu contena moja ya mahindi inayo ingizwa hapa inalipiwa si chini ya milioni 8 kama serikali inapata mapato kwenye hilo kwannini wanazuia?

WATALAAMU NISAIDIENI, KIUCHUMI KINALINDWA NINI HAPA.
 
Unapaswa kuagiza bidhaa ambazo upatikanaji wake hapa nchini ni mdogo au haupo. Ukitaka bidhaa zote hata zinazozalishwa hapa hapa nchini ziwe imported unavuruga kabisa uchumi na kuporomosha thamani ya shilingi. Kadri mnavyofanya manunuzi nje ya nchi ndivyo thamani yenu inavyozidi kuporomoka
 
Ni sawa kuhusu manunuzi lakini vip kuhusu mahindi tunayo ya kutosha kiasi hicho mbona unga sasa imakuwa shida?
 
Ni sawa kuhusu manunuzi lakini vip kuhusu mahindi tunayo ya kutosha kiasi hicho mbona unga sasa imakuwa shida?
Nani kakuambia hivyo. Mahindi yapo ila sema tu hakuna uwiano wa usambazi wa mahindi nchini. Kuna ukame ulisababisha upungufu baadhi ya mikoa lakini si kweli kwamba kuna upungufu nchi nzima. Hata maghala ya serikali NFRA bado yamejaa mahindi
 
Back
Top Bottom