Kwanini Semina za kuwa 'tajiri ndani ya wiki mbili' zimekuwa nyingi lakini watu bado hawatajiriki?

Mwanga Lutila

JF-Expert Member
Nov 10, 2016
4,137
13,824
Habari,

Kila kukicha kuna Semina, Watu na Vijarida/Vitabu vikielezea jinsi ya kuwa tajiri ndani wiki mbili, Vyote hivyo havitolewi bure kama ni semina utalipia na kama kitabu utanunua. Lakini kwanini bado watu hao 'wahudhuriaji wa hizo semina' hawatajiriki?

Je hawa watoa semina ni matapeli tu walioamua kufuta umaskini wao kwa kuhubiri utajiri? au wapewa elimu hiyo hawana elimu ya ziada na hawa tambui kuwa ili uwe tajiri ni 'mchakato' na wala sio blaa blaa za kuhubiriwa na 'wahamasishaji'?
 
Cha kushangaza hizo semina zina kiingilio,utasikia kiingilio ni 100,000/= sasa unashindwa kuelewa kama kweli wanataka watu wawe matajiri kwanini wasiwaite wakawapa elimu jinsi ya kuitumia hiyo pesa kama mtaji na kupanda kuwa matajiri?nadhani wao ndiyo wanaojifunza kuwa matajiri kuona kwamba tukikusanya kiwango hiki tutafikia wapi.
 
Mwenye nacho ataongezewa ila asiyenacho atanyang'anywa hata kile kidogo alicho nacho.

Watu wanaangalia fursa tu sasa hivi kwa sababu kupitia hizo semina wao wenyewe wanaongeza vipato vyao kwa kuuza hazo brochures na viiingilio vya waalikwa.
 
Wajinga ndio waliwao, wenyewe wameshindwa kujitajirisha. Wanataka hivyo viingilio wakale na familia zao.
Utajiri au mafanikio hayana Formula kuwa uki-apply unakuwa tajiri...Ingekuwa ni hivyo ningenunua formular ya Mengi au Bahresa niwe tajiri..

Watu hawaelewi utapeli huu....Unatoa 20,000 yako kuhudhuria Semina ya kuwa tajiri..WTF....Hiyo 20,000 wanaenda kutajirika na kuneemesha familia zao
 
mmoja alinifuata nikamwambia nipe hints ya semina halafu hicho kiingilio iwe kama mtaji analininunia na msuti wake huku mimi nikishusha kawine kangu kabaridi na tabasamu kwa mbali kimoyo moyo najisemea na utalipia hii wine .... nalailipa akaondoka sitaki ujinga
Haha hapo ulimuweza aise
 
Ukiwa na akili nzuri utakuwa tajiri bila kufundishwa ukiwa na tamaa ya utajiri utasindikiza maisha mpaka unaingia geto la haki

Ukijitambua unaweza kuwa tajiri

Zile semina ni zuri kwa waendeshaji maana unaingia kwa kiingilio na ndo yeye anapo ondokana na umasikini huku wewe ukibaki mchangiaji was utajiri wake
 
Back
Top Bottom