Kwanini Russia ilishindwa kumtetea Saddam Hussein wa Iraq ila kwa sasa inamkingia kifua Bashar Al-Assad wa Syria ilhali nchi hizi mbili zinapakana?

Infantry Soldier

JF-Expert Member
Feb 18, 2012
8,203
2,000
Shikamooni wakubwa zangu wote wa hapa jamiiforums.

Eti ndugu zangu watanzania (wale tu mnaofuatilia siasa za kimataifa kwa muda mrefu kama mimi);

Kwanini Russia ilishindwa kumtetea Saddam Hussein wa Iraq ila kwa sasa inamkingia kifua Bashar Al-Assad wa Syria ilhali nchi hizi mbili zinapakana?

Tafadhali tazama ramani ndogo ya nchi za mashariki ya kati hapo chini;

images (65).jpg


Ndio tuseme kuna unafiki unaendelea ndani ya baraza la usalama la umoja wa mataifa (UNSC)?

Russia na China walisusia kupiga kura turufu (VETO) jambo lilipelekea wanachama wengine wa baraza la usalama la umoja huo (U.S.A, France and the United Kingdom) kuridhia kwa pamoja uvamizi dhini wa Saddam Hussein wa Iraq. Kwanini Russia hao hao hawakususia kupiga kura ya VETO dhidi ya Syria ya Assad?

images (20).jpg


NB: Ninaomba mtu asije akaongelea ama kuuliza kwanini Russia haikumtetea Muammar Gadaffi kwa maana Iraq na Libya ni mbali sana ukilinganisha Iraq na Syria.

USISAHAU: ENDELEA KUWA MZALENDO IPENDE TANZANIA. USICHAFUE TASWIRA NJEMA YA TAIFA LAKO. USTAWI WA NCHI YETU UNAANZA NA WEWE. TIMIZA WAJIBU WAKO IPASAVYO.
 

Mbimbinho

JF-Expert Member
Aug 1, 2009
7,360
2,000
Sina hakika, lakini nishawahi kusikia kuwa Russia na Syria wana mkataba wa kiulinzi na usalama ambao ulitiwa sahini kipindi cha Baba yake Assad.

Pia kimaslahi, nilisoma sehemu kuwa territory ya Syria kama akichukua kibaraka wa West inaweza kuleta shida kwenye biashara ya mafuta na gasi ya Russia.
 

Chige

JF-Expert Member
Dec 20, 2008
10,693
2,000
Short answer ni kwamba:-

George na CIA walifanikiwa kuudanganya ulimwengu kwamba Saddam anamiliki WMD to the point, hata UN Security Council ilivyokaa mwaka 2002 iliitaka Iraq iwe disarmed.

UN Security Council Permanent Members WOTE, including Russia walipiga kura in favor UN kuitaka Iraq iwe disarmed kupitia resolution ambayo ilisema wazi kwamba Iraq kutofuata resolution iliyotolewa ingekuwa ni jambo lisilokubalika na LAZIMA iwe disarmed!!!

So, ikaonekana Iraq "amegoma" kutii matakwa ya UN kumbe maskini ya Mungu hizo WMD hakuwa nazo but no one, including Russia believed Saddam!!

Na ni kutokana na hilo, ndo maana US walipoamua kuivamia Iraq kwa kigezo cha kusaka WMD, hakuna aliyekuwa tayari kumtetea!!!

Swali la msingi ni: How come taifa kama Russia nao waliamini madai ya CIA?!

Inawezekana Russia walifahamu suala la Iraq kuwa na materials zinazoweza kutengeneza WMD hasa ukizangatia hapo kabla Saddam aliwahi kutumia silaha za kemikali!

So, kutokana na hilo, Russia alikuwa na kila sababu ya kuamini inawezekana kweli Saddam alikuwa na WMD, kwahiyo akamuacha afe peke yake!!

Lakini kwa upande mwingine, Russia na Iraq hawakuwa Maswahib worth to risk kwa sababu, we all know, miaka michache tu nyuma Iraq alikuwa anapigana vita ya CIA dhidi ya Iran!
 

Carlos The Jackal

JF-Expert Member
Feb 6, 2017
16,222
2,000
Kuiruhusu Syria iwe chin ya NATO..

Maana yake ni kufuta kabisa biashara ya Mafuta ya Urusi kutokea mashariki ya kati kwenda Ulaya.( ukumbuke NATO ilianxisha hii vita, kwa sababu Bashar Assad alikataa kuruhusu Bomba la Mafuta kupita nchin kwake kwenda Ulaya).

Ni Kuiondoa Urusi katika Mizani ya wenye Dunia.

Kuendelea kuizunguka Urusi Kijeshi.

Syria kimkakati ipo mahali pazuri...Urusi anaweza kuipiga Ulaya kirahisi kutokea Syria .

Urusi anauwezo wa kujua Kashikashi za Angani za Ulaya kutokea Syria kirahisi sanaaaa

Na Kubwaaaa sana. KUA NA KITU CHA MAKUBALIANO ,LINAPOKUJA SUALA LA ISRAEL.
 

Lucas Mobutu

JF-Expert Member
Jul 29, 2017
14,160
2,000
Saddam alikuwa na tuhuma nyingi ikiwemo kuna siku alipita kijiji fulani akashambuliwa hapo na waasi,ilikuwa kidogo auwawe akakimbia kwa mguu,kilichofuata alituma wajeda wa kila aina vifaru vikawa vinapita vinabomoa nyumba na inadaiwa alitumia chemicals kuwauwa raia.hovo basi huenda hii ni moja ya sababu hakutetewq
 

Infantry Soldier

JF-Expert Member
Feb 18, 2012
8,203
2,000
Hoja ya msingi sio kushambulia wananchi bali UN Resolution ambapo UN iliamini Saddam anamiliki WMD na kwahiyo LAZIMA iwe disarmed!!
Mkuu, kumbuka kwamba UN Resolution ilipitishwa baada ya ushahidi mzito kuletwa mbele ya baraza la usalama (UNSC) juu ya Saddam Hussein kushambulia wananchi (The Halabja chemical attack)...
 

AggerFirminho

JF-Expert Member
Sep 17, 2019
828
1,000
Iraq inapaka na Syria lakini haipakani na Urusi.
Urusi haitaki marekani aweke makao kwenye nchi zinazopakana na Yeye ndo sababu ya kumkingia kifua Syria.
Kama ambavyo China wanamkingia kifua North Korea.
 

Infantry Soldier

JF-Expert Member
Feb 18, 2012
8,203
2,000
Short answer ni kwamba:-

George na CIA walifanikiwa kuudanganya ulimwengu kwamba Saddam anamiliki WMD to the point, hata UN Security Council ilivyokaa mwaka 2002 iliitaka Iraq iwe disarmed.
Mbona Obama aliudanganya ulimwengu kuhusu Assad kumiliki WMD lakini Russia akaweka kifua mbele kumkinga huyu Rais wa Syria?...
 

Infantry Soldier

JF-Expert Member
Feb 18, 2012
8,203
2,000
UN Security Council Permanent Members WOTE, including Russia walipiga kura in favor UN kuitaka Iraq iwe disarmed kupitia resolution ambayo ilisema wazi kwamba Iraq kutofuata resolution iliyotolewa ingekuwa ni jambo lisilokubalika na LAZIMA iwe disarmed!!!
Katika sakata la WMDs za Assad Russia hakupiga kura ya ndio ila members wengine wote waliobaki walikubali Assad avamiwe kwa nguvu za kijeshi. Kwanini?...
 

Infantry Soldier

JF-Expert Member
Feb 18, 2012
8,203
2,000
Inawezekana Russia walifahamu suala la Iraq kuwa na materials zinazoweza kutengeneza WMD hasa ukizangatia hapo kabla Saddam aliwahi kutumia silaha za kemikali!
Baada ya lile shambulizi, Russia walikuwa na uhakika kuwa Assad anazo silaha za sumu na wakaongoza juhudi za UN za kuwapokonya kwa njia za kistaarabu...
 

Infantry Soldier

JF-Expert Member
Feb 18, 2012
8,203
2,000
Lakini kwa upande mwingine, Russia na Iraq hawakuwa Maswahib worth to risk kwa sababu, we all know, miaka michache tu nyuma Iraq alikuwa anapigana vita ya CIA dhidi ya Iran!
Kwa point hii ninaweza kukuamini kwa mbaaaaaaaaaaaali kidogo.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom