Kwanini Rais Magufuli lazima aombewe ....

Huu mwezi wa rozari kwa sie wakatoliki, kila mtu ajiombee na aombee familia yake.
 
Kama Mungu hayupo? (nadhani unanielewa kwa swali langu)... inawezekana Mungu hayupo hivyo kupoteza muda.
 
watu wanasahau kuwa yupo kwenye office mpaka 2020,

kuwa bitter kwa sasa hivi haisaidii,

badala ya chuki,tumuombee kweli atufikishe 2020 salama,
 
Maombi yote tangu issue ya Lissu yanaratibiwa na polisi.Pengine utuambie km yamesharuhusiwa tena.
 
Maombi bila imani ni bure wenzenu wanaomba Lissu anapona nyie mnaomba vyuma vinakaza si mutubu dhambi msimfanyie dhihaka Mungu?
 
Kwann wale wakiong'oa nati kweny gari la lemma wasingo'oe kwa marais madikteta
 
Bora nikae kimya maana hasira zangu nazijua. Nisije fanya sala akageuka mawe
 
Nchi yetu haina dini ndo maana lissu alizuiwa kuombea hata mkuu harusiwi kuombewa kama Mungu ameruhusu Tanzania ipitie magumu sawa,lakini mambo yanavyoendelea nchini yanasikitisha
 
Ni yupi muhimu wa kuombewa ni Lissu ambaye kapigwa risasi na kutokana na umahututi wake hana hata uwezo wa kuinua kinywa chake kuomba maombi ili apone,au ni huyu mtu mzima mwenye uwezo wa kutumia nguvu zake kuviamuru vyombo vya dola kuwazuia na kuwakamata wananchi wanaopanga kumuombea Lissu?.
 
Anataka aombewe kwa "mungu" anayeruhusu wengine wauawe sio Mungu wetu huyu
 
Kila mtu apambane nahali yake
 
Hivi tumuombee aendelee kuwa n'a hekima ? Au apate hekima.
 
Duh!...kushauriwa hataki, kukosolewa hakubali, hata kupangiwa hapendi, serikali take imepiga marufuku kumuombea Lisu lakini yeye tumuombee!.........bado natafakari..
 
Hivi tumuombee aendelee kuwa n'a hekima ? Au apate hekima.

Mkuu katika wote wewe ndiye uliyemwelewa sana mtoa thread.

In fact, Magufuli mwenyewe anaposema naomba mniombee anamaanisha watu wamowombee asije akadhuliwa na watu anaosema anapambana nao. Lakini hilo sio muhimu tena. Umuhimu wa kumwombea Magufuli hauko katika kuomba awe salama, bali asizidi kufanya maamuzi ya kuumiza wanyonge au kuonea watu au kufanya ukandamizaji katika uongozi wake, au hata kuua demokrasia nchini!

Kwa mantiki hii, maombi kwa ajili ya Tundu Lissu ni muhimu kama kwa ajili ya Magufuli!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…