Kwanini Rais anaogopa mikutano ya vyama vya siasa?

Kwanini Rais anaogopa mikutano ya vyama vya siasa?

Kutokana na uwezo wetu wa kufikiri namna ulivyo mambo mengine rais anatusaidia sana, hatuna uwezo wa kuyakataa.

Kwa mfano mtanzania wa kawaida hawezi kutenga muda wake wa kufanya siasa na kufanya kazi.

Unaweza mfanya asifanye kazi kwa mwaka mzima kisa siasa tu.

Ila taratibu tutafikia viwango hivyo vya kuweza kutenga muda wa siasa na kufanya shughuli za maendeleo.
aliyeelewa haya mashudu anisaidie😵
 
Hana ubavu wa kupambana na hoja nzito za upinzani,hata mashuleni ukiona Mwl anaingia darasani mkali ujue hajui kufundisha,Hivyo ukali ni self defence yake ili asiulizwe maswali na wanafunzi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mbowe juzi aliongea kwenye mkutano ndani ya kanisa kuhusu kanisa au!?

Acheni udaku mnapenda kutangaza uongo mtupu.
 
Sikukatazi kuamini uaminicho au upendacho kumjaji magufuli,ninahakika nawe vivyohivyo kwa yeyote,ila ukweli utabaki palepale, yupo madarakani kimabavu,kiwizi na kiukandamizaji demokrasia na zaidi ya hapo hapendeki na wengi.pia kauli zake zinadhihisha kukomoa watu hata kama hamkunichagua,mshahara mdogo nimeamua,hutaki acha kazi !. Tuna njaa nikawapikie,ukimwi nyie tetemeko nyie Zanzibar usiseme !.Haya maneno yanaonyesha Niko madarakani mtanifanya nini ? Wa njaa kufeni,wa kazi acheni,wa ukimwi na tetemeko kufeni !. Utawala huu hatakama unaleta maendeleo,unamletea nani ? Watuwako unawaona kama mbwa?hata mbwa nafuu utamtupia kiporo !.katawala kwa nguvu ya risasi,bado anadharau watu na kuwaona si Mali kitu ! kwani angekua tu kawaida angepungua nn?bashite anadunda ila walio wapa wapinzani kura wanasota jela nakupoteza kazi.siwatetei,ila kwanini bashite ?na haigusi wanasiasa,mawaziri na waliokarbu na magufuli ? au huoni ombwe kubwa la kupoteza amani na furaha,lililo ikumba nchi ? Asante pia hata kwa kuona nilicho andika barikiwa sana.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom