pakaywatek
JF-Expert Member
- Dec 28, 2014
- 4,710
- 6,372
Mwanzo alijinasibu kuwa mikutano hiyo inawapotezea wananchi mda wa kufanya kazi, wakati huohuo anazunguka na sijawahi kumsikia akiwakataza hao wananchi wasihudhurie kwenye hiyo mikutano yake kwani watapoteza mda wa kufanya kazi.
Pia alidai hataki siasa hadi 2020 wakati huo yeye anafanya siasa katika mikutano yake kwa kuwaponda wapinzani wake ambao yeye amewazuia wasifanye siasa wakati wao ni wana siasa.
Kama anatekeleza ilani ya CCM na anaitangaza anavyoitekeleza kwa nini anazuia mikutano wakati yeye anajinasibu serikali yake (kama anavyodai) inawatumikia wananchi?
Si aache wana siasa wafanye mikutano na kama wakimkosoa si wananchi watawapuuza tu?
Anaogopa nini wapinzani wanapofanya mikutano?