#COVID19 Kwanini Rais ameamua kujificha nyuma ya kamati ya Corona? Anaogopa nini kuwambia Watanzania wajiandae na AstraZeneca? Anaogopa nini?

Leak

JF-Expert Member
Feb 22, 2012
52,211
42,074
Wasalaam wana jamvi!

Nimeshangazwa sana na Mh Rais kusema ataunda kamati kuhusu swala la Corona ili baadae tuwe na msimamo kuhusu Corona!

Mimi kwenye hili nimejiuliza maswali hivi ni kweli Tanzania hatukuwa na msimamo kuhusu Corona? Huyu Rais si alikuwa Makamu wa Rais na Rais wake alishasema wazi kuwa Tanzania hakuna Corona na kama ipo ni ndogo sana?

Hii kamati anayounda anataka imwambie nini kipya asichokijua? Anataka aanze kutoa takwimu za Corona sasa anataka kamati imshauri?

Anataka aweke watu Lockdown sasa anataka kamati imshauri?

Anataka kulazimisha watu kuvaa barakoa sasa anataka kama imshauri?

Anataka kupokea chanjo ya Astrazeneca sasa anataka kamati imshauri?

Rais anaogopa nini kusema alikuwa hakubaliani na jinsi mtangulizi wake alivyo kuwa anaikabili Corona? Rais anaogopa nini kusema wamejiandaa kupokea chanjo ya AstraZeneca hivi karibuni?

Sidhani kama Rais anatakiwa kujificha nyuma ya kamati kwenye swala kama hili ambalo liko wazi!

Kuna kitu gani hajui ambacho anataka kamati imwambie?

Kwanini anajificha nyuma ya kamati anashindwa nini kuwambia watanzania wajiandae kudungwa Astrazeneca?

Kama Tanzania hatuna msimamo kwanini yeye havai barakoa? Hajui huo nao ni msimamo? Anataka ashauriwe nini?

Kwanini Tusiamini ana ajenda zake mkononi anataka azipitishe nyuma ya kamati ili watanzania waamini ni msimamo wa kamati kumbe ni msimamo wake?

Wasalaam!
 
Kwenye suala la Corona lazima tukubali Magufuli alichemka big time.

Hakuna mtu mwenye akili timamu angekubaliana na Magufuli kwa jinsi alivyoishughulikia korona.

Huwezi kuwa dogma ukajifanya Tanzania haina korona wakati Dunia nzima ina korona eti mungu ametusaidia, huyo mungu alishindwa nini kumsaidia korona isimuue?

Nakubaliana na mama, shughulika na korona kitaalam.
 
Kwenye swala la korona lazima tukubali Magufuli alichemka big time.

Hakuna mtu mwenye akili timamu angekubaliana na Magufuli kwa jinsi alivyoishughulikia korona.

Huwezi kua dogma ukajifanya Tanzania haina korona wakati Dunia nzima ina korona eti mungu ametusaidia, huyo mungu alishindwa nini kumsaidia korona isimuue?

Nakubaliana na mama, shughulika na korona kitaalam.
Unataka tuweke lock down, huo ndio utaalam unaotaka, hao wenye lock down wanakufa wengi zaidi ya Tz sasa nini faida ya lockdown ? SSH ana tatizo, tena ni KUBWA.
 
Kwenye swala la korona lazima tukubali Magufuli alichemka big time.

Hakuna mtu mwenye akili timamu angekubaliana na Magufuli kwa jinsi alivyoishughulikia korona.

Huwezi kua dogma ukajifanya Tanzania haina korona wakati Dunia nzima ina korona eti mungu ametusaidia, huyo mungu alishindwa nini kumsaidia korona isimuue?

Nakubaliana na mama, shughulika na korona kitaalam.
Unayeandika hivi, usikute hujawahi hata kuambukizwa hiyo Corona, na pengine unaposema Magufuli hakuwa Sawa katika kushughurikia Corona ukilinganisha na nchi gani ambao kwao wameshughurikia vizuri na Corona kwao haipo mpaka Leo ni Nani na nchi gani??
 
Kenya wanaofuata COVID19 protocols wako wapi?
Je hamsikii hosptali na mfumo wa afya ulivyozidiwa?
Mbona bongo tunaishi na vizuri tu na maisha yanaendelea kama kawaida?
Tunataka maisha gani zaidi?
 
Kumekucha!

Yupo sahihi kabisa kwa sababu ile kamati ya mwanzo iliongozwa na PM Majaliwa na Ummy Mwalimu ilikuwa ni ya kisiasa siyo ya kitaalamu na haijawahi kuvunjwa!

Ndio maana ukaona Jaffo amejiingiza na nyungu zake.
Licha ya kuwepo mapungufu kupambana na covid lkn nchi hakuiweka
Lockdown,magufuli ni kama alikuwa anataka
Watanzania tuishi nayo tu

Ova
 
Back
Top Bottom