Kwanini Profesa Kabudi anaandamwa?

Kumekuwepo na utitiri Wa watu kumuandama na kumkashifu Prof. Palamagamba Mwaliko Aidan Kabudi hasa katika mjadala huu Wa Sakata la DP WORLD. Kwanini imekuwa hivi!?

Mwanasiasa ni binadamu anayefanyakazi kwa kutazama kiongozi Wa nchi anataka nini. Hii ni nidhamu ya kutawala ambayo imekuwepo tangu Enzi za utawala Wa Roma. Ndio maana WANACCM Leo hawawezi kumpinga mheshimiwa Rais kwa lolote mpaka atakapomaliza utawala wake.

Mwanasiasa yeyote atakupa Tia sifa kama unapenda kutukuzwa, atakupa hisani kama unapenda hisani, atawajibika kama unapenda uwajibikaji.

Kabudi Enzi Magufuli aliwajibika kwenye mikataba ya madini, kwenye shares za serekali katika makampuni mbalimbali nk kwasababu uelekeo Wa Serekali ulikuwa kupambana na mikataba yote ya hovyo na hawakuona aibu wala muhali kuwa Piga mkwara wawekezaji wote wenye mikataba ya kinyonyoji. Alikuwa ni mtu mwenye nguvu serekalini kwasababu alionekana kama nembo na alama ya uzalendo katika utawala Wa JPM.

Kwasasa Ndani ya serekali Hana nguvu wala ushawishi tena, meza imepinduka na wenye nguvu kwasasa ni Akina January Makamba, Nape Nnauye na Mwigulu. Hawa ndio alama na Icon Ndani ya serekali. Uelekeo Wa wanasiasa kwasasa ni kuwapa sapoti Hawa, kwenda kinyume nao ni kupunguza vema ya kisiasa Ndani ya Chama na serekali.

Ni dhahiri kuwa Prof. Kabudi Leo ukimfuata hadharani ukamuuliza jambo lolote la Enzi za utawala Wa JPM hawezi kulisifia hadharani kwasababu watu Hawa ambao ndio nembo ya utawala kwasasa they were not in good terms with Late JPM. Ili kuepuka kukera yuko tayari kusema kuwa mchakato Wa Makinikia na Mirabaha ya madini ilikuwa bisheni, Suala la shares za serekali. Pale Airtel nk halikuwa na maana, ununuzi Wa ndege ulikuwa uamuzi Wa hovyo, ujenzi Wa SGR ulikosa dira nk. Why? Kanuni ya kuwa msaidizi Wa kisiasa ni kucheza na binti la. Muziki.

Professor Kabudi aachwe apumzike, alifanya kazi nzuri Sana, kwasasa analinds heshima yake na heshima ya serekali. Hataendelea kutoa maoni yake kulingana na falsafa ya mtawala husika.

Inshort alikuwa ameshikiwa akili wakati wa dhalimu. Hakuna cha nini wala nini. Hilo zee lilikuwa linajipendekeza hadi linatia kinyaa. Na si ajabu ww mleta uzi ndio Kabudi mwenyewe.
 
Ni wajinga pekee ndio wataomuandama Prof. Kabudi, haiwezekani mtu atoe bandari kwa wajomba zake, lawama apelekewe Kabudi.
Kabudi hataki kuingilia mambo ya kifamilia ya mtu na Wajomba zake.
 
Kama yeye ni mwanaume kweli ajiuzulu kama Nyalalandu alivyojiuzulu enzi za mwendazake
Nyalandu alijirekodi ujumbe wa kujiuzulu akiwa mpakani, na baada ya kurusha Ile clip, akatokomea,

Ndo uanaume huo?

Mwamakula ndo jembe, Yeye aliandamana mwenyewe wakati CHADEMA wamekubali yaishe.
 
Nyalandu alijirekodi ujumbe wa kujiuzulu akiwa mpakani, na baada ya kurusha Ile clip, akatokomea,

Ndo uanaume huo?

Mwamakula ndo jembe, Yeye aliandamana mwenyewe wakati CHADEMA wamekubali yaishe.
Nyalandu aliondoka CCM akajiunga Chadema na akawa anashiriki kikamilifu siasa za Chadema.

Kabudi hawezi kutoka CCM, hana ujasiri huo
 
Back
Top Bottom