Nafikiri mambo ya kuulizana dini makazini, hapo zamani, yalikuwa na Mantiki ya kudhibiti utoro au ukwepaji majukumu. Ina maana kuwa, isije ukawa umeandika wewe ni mkristo, halafu Ijumaa unakwepa kwenda doria kwa kudai unaenda Masjid, au labda wewe ni Muislam, ukatae lindo Jumapili kwa kudai unaenda Kanisani. Kwa kuandikisha dini ndani ya jeshi la polisi, inawezekana kiubinadamu, kwa Mkuu kutoa ruhusa spesho kwa mtu kuhudhuria shughuli au tafrija za kidini bila kudanganyana.
Haya ni mawayo yangu tu, hayawakilishi mtazamo wa watendaji wa utumishi walioanzisha taratibu hizi.