Kwanini Polisi?

Kwanini Polisi?

mr qns

Senior Member
Joined
Jan 3, 2018
Posts
193
Reaction score
197
Matatizo ya polisi yamekua yakisemwa sana na RAIA hasa katika mahusiano yao ya kijamii.

polisi amekua kama adui mbele ya umma ,polisi huonekana ni mwenye jeuri,kiburi na mwenye kujivuna na madaraka yake !!

naamini si bure kutakua na jambo labda tuseme RAIA wana matatizo na hawazingatii sheria kwamana polisi kazi yake ni kulinda jamii na kuhakikisha sheria hazivunjwi ama la matukio na matendo yapolisi yatakua hayapendezi watu wengi hususani vijana!!
vijana pia huongoza kwa kuvunja sheria,utumiaji madawa ya kulevya,uhalifu,matusi nk

Lakini mbona wanajeshi hawachukiwi kama polisi kwenye jamii? maranyingi husifiwa kwa nidhamu yao na ustaarabu na ni marachache kuskia mitafaruku ya RAIA na wanajeshi?!

Historia ya matatizo ya polisi na raia au wananchi inaonekana si ya Africa tu pekee Bali dunia nzima,kumekua na matukio mengi nchini marekani ya polisi kuua na kuwanyanyasa watu weusi,polisi wanachukiwa marekani kiasi kwamba ukiwa polisi unahatarisha maisha yako pia!! wanamuziki pia wamekua na migogoro ya mda mrefu na polisi na kuna nyimbo kibao ambazo wanamuziki wanatukana polisi waziwazi!

Hali hii si tofauti sana na nchi za kiafrica kama yetu,tofauti ndogo ni kwamba nchi yetu watu wanachukia polisi lakini ni vigumu kuweka wazi hisia zao labda mitandaoni na wasanii hawawezi kuongelea wazi chuki zao kwa polisi isipokua kwa mafumbo!

tatizo kubwa linakuja inapotokea polisi kapata matatizo badala yake watu hushangilia badala ya kuhuzunika!!
polisi anasahaulika kama ni mwananchi pia wakawaida katika jamii?! kwamba anaweza kua jirani au kaka ,Dada au mzazi wako.walau watu wanaoishi na jamii za polisi karibu au kwenye kota zao huwa na uelewa na kuona kuwa hawa ni ndugu zetu pia

watu wengi husikika wakisema polisi si rafiki wakweli mana hachelewi kukugeuka!! mtaongea vizuri nyumbani lakini ukifikwa na tatizo atakuruka!! lakini polisi wao husema kuwa wanatimiza tu wajibu wakazi yao na kibaya zaidi kazi yao wao hairuhusu kuuliza maswali Bali kupokea oda!!

Lakini raia nao huuliza je polisi hapaswi kuona mambo mengine kama binadamu wa kawaida na kutumia utu?! kwamana hiyo watu wengi husema polisi hutumia madaraka yao vibaya na hawachelewi kukupakazia kesi?!

kuna watu wengine pia husema lakini kunapolisi wazuri wenye utu wanaojielewa na kutimiza wajibu wa kazi yao ipasavyo na wale wabaya wala rushwa na katili! polisi wabaya husemekana hata wakiacha kazi hutumia ujuzi wao vibaya katika shughuli za kihalifu?!

Nani alaumiwe? ! polisi kukosa maadili?! matukio yanayohusisha Vifo vya wnanchi mikonon mwa polisi ni mengi,na raia wanahasira !! na inasemekana viongozi huusisha polisi hata katika migogoro yao binafsi isiyo na tija na maana kwa jamii!

na polisi wao hawawezi kubisha sababu kazi yao ni kupokea oda!! Nini kifanyike!! elimu itumike !! mahusiano ya jamii na polisi yaboreshwe sababu polisi ni sehemu ya jamii!!
mengi yapo yakuzungumza Ila tuishie hapa.tunawapenda polisi popote walipo,tunashukuru kwa ulinzi na usalama wa maisha yetu na nchi yetu,Mungu awabariki na kuwapa ujasiri katika kazi yenu ngumu ya kulinda jamii,awape hekima na maarifa.amani!
 
Hata hao wanajeshi wakiwa wanafanya kazi za polisi watachukiwa tu.

Polisi anafanya kazi zake kila siku kuhusu raia wa kawaida kwa hiyo hawezi kupendwa na wote pia hawez kuchukiwa na wote
 
Back
Top Bottom