Kwanini Polisi huwa hawana uchungu na matumizi mabaya ya Fedha ya Umma?

Hamatan

JF-Expert Member
Nov 10, 2020
3,183
7,645
Polisi huvalishwa na sisi wananchi, wanaishi kwenye nyumba zinazogharamiwa na sisi wananchi, wanasafirishwa kwa magari yanayogharamiwa na sisi wananchi. Hata buti na soksi zao ni sisi wananchi ndio tunaogharamia.

Matarajio ya wananchi ilikuwa ni kuona hawa wanaogharamiwa karibia kila kitu na wananchi, wanafanya kazi ya kuwalinda wananchi na mali zao kwa uadilifu mkubwa. Bahati mbaya, ni kinyume kabisa.

Yaani pesa ya mwananchi, polisi wanatumia katika harakati ovu, harakati za kubambikizia watu kesi (na hili hata Rais alilikemea) na wakati fulani kufanya matukio ambayo kwa tafsiri halisi ni utekaji.

Wananchi tulitangaziwa kuna ushahidi mzito dhidi ya Mbowe na wenzake kuhusika kwenye njama za kufanya ugaidi. Tukaambiwa kuna mashahidi na vielelezo. Tukawa na shauku kubwa ya kusikia na kuona.

Wananchi tulitarajia kuona vielelezo kama vile mabomu ambayo yangetumika kulipulia vituo vya mafuta, labda na mashine kama vile chainsew za kuangushia miti kuziba barabara, na pengine hata bunduki au zana ambazo zingetumika kuua viongozi.

Maajabu ya karne, kila shahidi anasimama mbele ya mahakama kupiga stories namna alivyosafiri kufika Moshi na kwenda Dar, alivyokula njiani, alivyobadilisha gari, alivyoingiza majina ya watu kwenye register book ya polisi! Mtu wa Tigo, tulitatajia angeleta mawasiliano ya siri ya hao magaidi waliyokuwa wanafanya katika maandalizi ya kufanya ugaidi. Cha ajabu analeta story ya kutuma muamala wa shilingi laki 5! Ujinga mkubwa! Kutuma laki 5 ndiyo ugaidi? Basi Watanzania wote ni magaidi. Maana hakuna ambaye hajawahi kutuma fedha.

Shahidi anaelezea kuwa walikuwa wanasajili namba za simu. Kusajili namba za simu ndiyo ugaidi? Kama ni ugaidi, basi sisi sote ni magaidi. Na siro, na Kingai na waendesha mashtaka wote, pamoja na jaji basi ni magaidi. Maana sote kwa wakati fulani tumesajili laini za simu.

Mpaka leo, hakuna hata mmoja aliyetoa kielelezo cha ugaidi wala maelezo yanayothibitisha ugaidi kupangwa au kutendeka.

Mahakama badala ya kusikiliza kesi halisia, inapoteza muda kusikiliza stories za akina Kingai na wenzake. Mawakili wa Serikali badala ya kufanya kazi wanazostahili kufanya, wamekuwa wachombezaji wa mashahidi ambao kwa ufahamu wa kawaida, ni dhahiri ni mashahidi wa kutengenezwa, na hawana chochote cha maana cha kuoambia mahakama. Nadala ya kuleta vielelzo vya maana, wanaleta makaratasi waliyoyaandika wenyewe, na kuwalazimisha wqtuhumiwa kusaini. Ni ujinga wa hali ya juu.

Pesa yetu inateketea bila sababu kwa vile tu polisi hawana uchungu na pesa yetu. Tunawavalisha, tunawasafirisha, tunawalisha na kuwatibu ili wawalinde raia na mali zao, na siyo hii michezo isiyo na vichwa wala miguu. Inasikitisha sana. Taifa hili hatutakuja kupiga hatua kwa sababu pesa yetu kidogo inayopatikana, tunaitumia kwa mambo ya hovyo, tukiacha mambo ya msingi.

Wananchi tupaze sauti kuwataka polisi wafanye kazi wanazostahili kifanya, au la Jeshi la polisi liundwe upya, na hawa polisi wachafuzi wafukuzwe.
 
Ogopa askari hasa akikuta na mali.

Ogopa askari wale wa patrol wenye maplate number ya ajabu ajabu mara NHZ 5487 halafu hawana sare ni hatari wanakuua na kukupora mali na ikiwezekana wanaweza kukuzika pasipo kujulikana si unaona wanatembea na koleo na bendera nyekundu muda wote?
 
Yaani wale ni zaidi ya majambazi. Siku wananchi tutakapouvaa ujasiri, wale wakionekana, wanastahili kuteketezwa maana wapo kwaajili ya kuutumikia uovu. Mwovu hastahili kuwa rafiki wa yeyote labda mwovu aombaye toba.

Kuna mazingira mengine, ni aheri polisi wasingekuwepo, mbakie na vibaka wenu mtaani mjue namna ya kuwadhibiti, maana madhara ya polisi dhidi ya watu wasio na hatia, kuna wakati yanakuwa nafuu madhara yanayosababishwa na jambazi sugu.
 
Yaani wale ni zaidi ya majambazi. Siku wananchi tutakapouvaa ujasiri, wale wakionekana, wanastahili kuteketezwa maana wapo kwaajili ya kuutumikia uovu. Mwovu hastahili kuwa rafiki wa yeyote labda mwovu aombaye toba.

Kabisa ni zaidi ya majambazi ,ukiwaona wametega sehemu sio kwamba wanaangalia usalama wa raia na mali zao lahasha wanasikilizia gari zenye mizigo ili wawapore au wagawane pasu kwa pasu....wale ni certified street gang.
 
Unakosea unapowalaumu polisi kwenye hayo matumizi mabaya, chanzo cha yote ni CCM na serikali yake, hao ndio mabosi wa polisi na huwatuma polisi popote wakafanye uhalifu wowote bila kuhofia gharama unazozingumzia.

Wamezoea kuwatuma polisi kwenye mambo mabaya wakafanye kwa manufaa yao, mwishowe ndio na polisi nao wamejiongeza kwa kuwaumiza wananchi kuwawekea vipande vya meno ya tembo ili wagawane pesa na wananchi wasio na hatia.
 
Nchi haina uongozi ndugu zangu na raia wenyewe ndio hivyo kila kitu hewalah!! Sijui lini tutaamka na kuwa kama raia wa nchi zingine wanaojitambua.
 
watanzania huwa walalamishi saaana, ukiwaambia wachukue hatua juu ya hilo wanalolalamikia wote wanaingia mitini...

Nigeria walipokuwa wanasumbuliwa na wale SARS, raia waliingia barabarani mpaka wenye mamlaka wakasikia...wabongo sasa makelele mitandaoni kimyaaa...
 
Polisi huvalishwa na sisi wananchi, wanaishi kwenye nyumba zinazogharamiwa na sisi wananchi, wanasafirishwa kwa magari yanayogharamiwa na sisi wananchi. Hata buti na soksi zao ni sisi wananchi ndio tunaogharamia.

Matarajio ya wananchi ilikuwa ni kuona hawa wanaogharamiwa karibia kila kitu na wananchi, wanafanya kazi ya kuwalinda wananchi na mali zao kwa uadilifu mkubwa. Bahati mbaya, ni kinyume kabisa.

Yaani pesa ya mwananchi, polisi wanatumia katika harakati ovu, harakati za kubambikizia watu kesi (na hili hata Rais alilikemea) na wakati fulani kufanya matukio ambayo kwa tafsiri halisi ni utekaji.

Wananchi tulitangaziwa kuna ushahidi mzito dhidi ya Mbowe na wenzake kuhusika kwenye njama za kufanya ugaidi. Tukaambiwa kuna mashahidi na vielelezo. Tukawa na shauku kubwa ya kusikia na kuona.

Wananchi tulitarajia kuona vielelezo kama vile mabomu ambayo yangetumika kulipulia vituo vya mafuta, labda na mashine kama vile chainsew za kuangushia miti kuziba barabara, na pengine hata bunduki au zana ambazo zingetumika kuua viongozi.

Maajabu ya karne, kila shahidi anasimama mbele ya mahakama kupiga stories namna alivyosafiri kufika Moshi na kwenda Dar, alivyokula njiani, alivyobadilisha gari, alivyoingiza majina ya watu kwenye register book ya polisi! Mtu wa Tigo, tulitatajia angeleta mawasiliano ya siri ya hao magaidi waliyokuwa wanafanya katika maandalizi ya kufanya ugaidi. Cha ajabu analeta story ya kutuma muamala wa shilingi laki 5! Ujinga mkubwa! Kutuma laki 5 ndiyo ugaidi? Basi Watanzania wote ni magaidi. Maana hakuna ambaye hajawahi kutuma fedha.

Shahidi anaelezea kuwa walikuwa wanasajili namba za simu. Kusajili namba za simu ndiyo ugaidi? Kama ni ugaidi, basi sisi sote ni magaidi. Na siro, na Kingai na waendesha mashtaka wote, pamoja na jaji basi ni magaidi. Maana sote kwa wakati fulani tumesajili laini za simu.

Mpaka leo, hakuna hata mmoja aliyetoa kielelezo cha ugaidi wala maelezo yanayothibitisha ugaidi kupangwa au kutendeka.

Mahakama badala ya kusikiliza kesi halisia, inapoteza muda kusikiliza stories za akina Kingai na wenzake. Mawakili wa Serikali badala ya kufanya kazi wanazostahili kufanya, wamekuwa wachombezaji wa mashahidi ambao kwa ufahamu wa kawaida, ni dhahiri ni mashahidi wa kutengenezwa, na hawana chochote cha maana cha kuoambia mahakama. Nadala ya kuleta vielelzo vya maana, wanaleta makaratasi waliyoyaandika wenyewe, na kuwalazimisha wqtuhumiwa kusaini. Ni ujinga wa hali ya juu.

Pesa yetu inateketea bila sababu kwa vile tu polisi hawana uchungu na pesa yetu. Tunawavalisha, tunawasafirisha, tunawalisha na kuwatibu ili wawalinde raia na mali zao, na siyo hii michezo isiyo na vichwa wala miguu. Inasikitisha sana. Taifa hili hatutakuja kupiga hatua kwa sababu pesa yetu kidogo inayopatikana, tunaitumia kwa mambo ya hovyo, tukiacha mambo ya msingi.

Wananchi tupaze sauti kuwataka polisi wafanye kazi wanazostahili kifanya, au la Jeshi la polisi liundwe upya, na hawa polisi wachafuzi wafukuzwe.
Sheria ilio anzisha jeshi la polisi tangu enzi za ukoloni hijabadirishwa. Standing order ya jeshi la polisi ni kulinda viongozi na mali zao. Kulinda raia na mali zao ni slogan ya kisiasa. Ukiona polisi wanafanya doria ni kuhakikisha kuna amani ndani yenu, ili viongozi wasibughudhiwe.
 
Unajua mimi kipindi cha nyuma nilifikiri hizi story za kulaumu polisi sio za kweli.
Lakini niliogopa sana hawa watu hasa pale ndugu yangu alipopata kisanga bar..
Walikamatwa usiku wakawekwa lockup kwa kuleta fujo bar..
Lakini kule ndani ya kituo anasikia askari anasema huyu tusimpe bangi.. Ongea na flani anayo funguo ya stoo leta CHUMA moja hapa mezani kisha tumkabidhi na maandishi juu ameitoa wapi..
Jamaa hakuelewa wanamaanisha nini.. Akashangaa libunduki likubwa mezani anaambiwa wewe itakufaa kesi ya ujambazi.. Tuambie hii bunduki umeitoa wapi..
Machozi yalimtoka.. Tafuta ndugu jichange sana.. Hela ya kutosha akapona na kesi ya ujambazi.. Wewe waone tu polisi.. Wakikuamulia unakula mvua 30 kimchezo mchezo
 
Kuna kipindi pale Kakola Polisi waliokuwa wakifanya uhalifu walitiwa kibano na Sungusungu mpaka wakakimbilia Nyakagwe Hehee.

Sijui Sungusungu waliishiaga wapi.
 
Yaani ni uharamia wa hali ya juu. Na hii nadhani ndiyo maana huwa uzeeni wanakuwa watu wa maisha ya majuto. Wamelaanika.
 
Kwa ujumla ni aheri utendaji wa sungusungu unazingatia haki kuliko ubaradhuli wa polisi.
 
Kenya wanajitahidi.. Camera vituo vya polisi.. Hata ukihojiwa unawekewa camera.. Kupunguza uhuni kama huu
Polisi akisema amekukamata na silaha inakuwa vigumu kwa mahakama kukataa na hivyo unaenda na maji.
 
Kwa ujumla ni aheri utendaji wa sungusungu unazingatia haki kuliko ubaradhuli wa polisi.
Kuna siku nimekutana na very friendly Traffic Police, akanipiga Warning tu.

Sasa huyo ninaimani anaijua hata PGO ila hawa wanaokesha Bar Wananchi wengi wanawalalamikia.
 
Kuna polisi wana utu wapo wengi. Yaani hata akipelekewa kesi anaichunguza kwa haki bila upendeleo.
Ila wapo hawa wa chini nafikiri maslai sio mazuri hivyo akipata mtuhumiwa kwake moyoni anaona ni fursa ya hela..
Wengi wa wananchi wanajikuta wameangukia kwa hawa ambao maslai ni madogo.. Hafikirii hata warning au hili niliache au hili linahitaji uchunguzi.. Yeye anafikiria kuvuna pesa..
 
Kuna wakati haswa wa usiku unakuta Cruiser imepaki Bar unawakuta Wamelewa huwa najiuliza maswali mengi sana.
 
Back
Top Bottom