Kwanini Pasco haipendi serikali ya Magufuli?

Huyu aliwahi jitia unajimu kwa kusema uchaguzi huu atashinda Lowassa iwe isiwe...sasa haikuwa akaamua idisds mazima CCM na serikali ya JPM
 
wekeni ushahidi basi tujue kama kweli alibadili gia angani. Walau amejitahidi kuwa neutral ktk mabandiko yake mengi tu.
 
Pasco si lolote si chochote ni kama wewe, japo na mchambuzi na mwandishi mahili, hivyo unavyojijengea dhana ya fulan akipenda jambo ndo inakuwa safi uo ni utumwa wa fikra, pasco ni member tu kama wewe hapo , na ana haki ya kupenda au kutopenda serikali ya magufuli,
Kwani ni watanzania wote wanaipenda serikali ya magufuli isipokuwa pasco? Hapana wapo wengi tena wenye kishindo kikubwa wakitamka msimamo wao
 
Kwenye haya maisha..
1. Ukiona unatumia muda mwingi kwenye kujitetea kwa sehemu kubwa ya mambo uyafanyayo JIKAGUE KWENYE KAULI NA MATENDO YAKO
2. Ukijiona unatumia mida mwingi sana kumtetea mtu kwa almost kwa kila anachokifanya.. Jikague na ukague matendo na maneno ya unayemtetea..
3. Ukijiona kila kauli unayoitoa inaleta mijadala isiyo na tija kwako na kwa wanaokuzunguka ... JIKAGUE
4. Ukijiona kila kitu ili kitendwe vile unavyotaka ni LAZIMA UTUMIE UKALI, KAULI NGUMU NA VITISHO..jikague..
5. Ukijiona unawazawaza kuongeza wanaokulinda... JIANGALIE
6. Ukijiona kila anayekuzunguka ni wa NDIYO MZEE jiangalie maana wanakudanganya kuwa unakubalika.. OGOPA SANA KUZUNGUKWA NA WATU WANAOTENDA NA KUYASEMA UNAYOYAPENDA TU BILA KUKUHOJI WALA KUCHANGIA MAWAZO ILI KUBORESHA
 
Unajikontradikti mkuu... mara si lolote wala chochote mara mchambuzi na mwandishi mahili... HAPO PANATOSHA
 
Huamini nini wakati Magufuli kipenzi chako?
Nimependa hapo tuu uliposema kipenzi chako.

P
 
Wanabodi,

Mie nashangaa sana kwanini huyu anayejiita Pasco hapendi chochote kinachofanywa na serikali ya Magufuli.
Leo Machi 17 ambayo ni Magufuli Day, nadurusu baadhi ya mabandiko yangu humu kumhusu JPM huku nikitafakari, if I was right or I was wrong.
Kwa vile kila zama na zama zake, Pumzika kwa Amani Magufuli wetu huko ulipo.
RIP JPM
Paskali.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…