Mr pianoman
JF-Expert Member
- May 22, 2019
- 2,549
- 6,097
Watu wengi wamekuwa wakiuliza swali: "Kwanini ndege za abiria wasiweke miamvuli {#parachutes} ili kila mtu aweze kuruka inapotokea dharura"
Ni swali zuri, lakini kiuhalisia haiwezekani kwasababu zifuatazo:
1. Urukaji kwa kutumia mwamvuli {parachute} unahitaji mafunzo ya saa 4 hadi 5 kwa darasani ikifuatia vitendo akiwemo mwalimu mmoja au wawili.
Utuaji unahitaji akili na ustadi mkubwa kuepuka kutengua miguu au kiuno. Hivyo ndege za abiria 100 hadi 500 ni vigumu kutoa mafunzo, gharama na muda.
2. Urukaji kutumia mwamvuli kawaida ndege haitakiwi kuzidi kasi ya 200km/saa na umbali usiozidi futi 13,000 kwa warukaji waliobobea, futi 3,500 warukaji wa kawaida.
Ndege kama #Boeing787 {#Dreamliner} kawaida hupaa futi 35,000 hadi 43,000 kwa kasi inayofika hadi 900km/saa. Kuruka katika kasi hiyo unaweza kuvunjwa na kusambaratishwa na upepo ikiwa si kujipigiza katika mbawa au mkia wa ndege.
Urukaji wa mwamvuli unaozidi futi 13,000 unahitaji kifaa maalumu cha kukufahamisha kimo ulichopo, '#musk' na mtungi wa '#oxygen' kwasababu kimo zaidi ya hapo hakuna oksijeni ya kutosha vinginevyo unaweza kuzimia {#hypoxia} kabla ya kufika kimo sahihi cha kufungua mwamvuli wako.
3. Mwamvuli mmoja na vifaa vyake unaweza kugharimu kati ya milioni 15 hadi 20.
4. Mafunzo yanahitaji kufahamu kuendesha mwamvuli huo pamoja na ishara za mikono kama njia ya mawasiliano.
5. Mwamvuli mmoja una kilogramu zaidi ya 20, mara idadi ya abiria wote ni uzito mkubwa sana ambao utaathiri mafuta na uzito wa ndege.
6. Urukaji wa mwamvuli unahitaji kupeana nafasi hadi futi 500 au nusu dakika kwa watu wa kawaida ili kuepuka kuvaana angani.
Hii si rahisi kwa abiria walio'panic kwenye dharura.
7. Takwimu zinaonesha ndege nyingi asilimia 80% hupata dharura wakati wa kutua au kupaa.
Hivyo hakuna muda na kimo cha kutosha abiria kuweza kuruka.
8. Ndege chache zipatazo dharura katika kimo cha mbali husababishwa na hali mbaya ya hewa kama wingu la mawe na radi {#thunderstorm} hivyo ni vigumu kuruka na mwamvuli katika hali hiyo.
9. Dharura nyingi zikutazo ndege zinahitaji ufunge mkanda kuepuka kurushwa au kuelea ndani ya ndege.
Hivyo ni vigumu kuvaa mwamvuli na kutembea kufikia mlango.
10. Ndege zipaazo kimo cha mbali huwa zinatengeneza mkandamizo wa hewa ndani {cabin_pressure} ili upate mazingira yanayofanana na ardhini kuepusha damu isijae gesi na kuchemka povu {#blood_boiling_bubbles} kwasababu ya pressure ndogo.
Ndege ni salama zaidi hata kwa dharura.
Credit by
#Aviation_Media_Tanzania