Kwanini ni Prof. Ibrahim Haruna Lipumba?

CUF Habari

JF-Expert Member
Dec 12, 2019
239
234
Kwanini ni Prof Lipumba
1. Ni kwa sababu ana majibu ya kitaalam ya kutatua matatizo yanayo ikabili nchi na wananchi kwa ujumla

(i)Ana deni kwa watanzania linalotokana na kodi zao zilizotumika kumpa elimu na maarifa makubwa yaliyo na majibu ya kweli ya kutatua kero za umasikini wa wananchi walizodumu nazo kwa muda mrefu tangu kupata uhuru.

(ii)Ana deni kwa muumba wake kwa tunu aliyomjaalia ya kiwango cha juu cha ujuzi na maarifa makubwa yanayohusu majibu ya hakika ya kuondoa umasikini kwa wana nchi na Tanzania kwa ujumla wake

kwani bila urais hawezi kutatua kero hizo?
(i)Bila urais hawezi kutatua kero kutokana na mfumo wa nchi yetu, mfumo ambao mtu akiwa rais yeye ndiye mwenye maamuzi ya nini kifanyike wapi na lini.

(ii) Bila Urais hawezi kwa sababu Mifumo kama hii siyo rafiki kwa maslahi mapana ya nchi na watu wake ndio maana CUF ina sema pamoja na mambo mengine itakayofanya ni pamoja na kujenga taasisi ya urais ili ifanye kazi kwa kuzingatia miongozo ya nchi badala ya mtu mmoja kama afanyavyo mheshimiwa Rais wetu na kama walivyofanya watangulizi wake.

(iii) Kufanikisha yote hayo CUF italazimika kuunda serikali ya umoja wa kitaifa ili iweze kujenga mifumo imara ya uongozi na utawala BORA isiyokuwa ya kishabiki ila weledi.

(iv) mifumo hiyo inatarajiwa iweze kujibu kiu ya wananchi ya kuweza kusimamia nchi yao.

(V) Nchi ikiwa na taasisi ya urais itaweza kukusanya wale wote waliyotunukiwa taaluma na maarifa mbalimbali ili kuweza kutowa majibu mbalimbali ya changamoto zilizopo na zitakazojitokeza.

3. Hofu ya Prof ya kukosa majibu ya maswali atakayokutana nayo kwa mola wake ndio yanayomsukuma kuendelea kuwaonesha Wananchi kwamba kuna jambo ambalo hajafanya kwao na kwamba wasipo liona wao yeye atakuwa amefanya jitihada ambazo sisi wana wa nchi tumeziona yeye amedhihirisha na Muumba wake amezishuhudia juhudi zake hizo.

4. Prof kasaidia Nchi nyingi kujikwamua kiuchumi na ni miongoni mwa magwiji walioandaa malengo ya maendeleo ya Milenia hivyo anajua mapito sahihi ya kupita ili kufika huko kwenye MDGS (MILLENNIUM DEVELOPMENT GOALS).
 
CCM Zanzibar inatia huruma .
Mgombea Urais Wanapewa
Wabunge wanapewa
Hata wawakilishi wanapewa kutoka Dodoma.

Tukumbuke ASP+TANU =CCM
Lakini Zanzibar hawezi kutoa M/Kiti wala SG

Kuna Makamu Wenyeviti 2

Akifa M/Kiti wao wa taifa anachukua nafasia Makamu wa Bara Ccm
Kwa ufupi Ccm Zanzibar Kama Tawi la Ccm Mtwara.

Wanzazibar hamkeni.
 
Ila Safari hii sidhani kama Pro-pesa ataambulia chochote kwa Ngosha aisee.
Enzi ya Mr Smile alikokuwa anapiga mpunga wa usaliti, imepita!
 
*Kwa nini ni Prof Lipumba**....
.........
4. Prof kasaidia Nchi nyingi kujikwamua kiuchumi na ni miongoni mwa magwiji walioandaa malengo ya maendeleo ya Milenia hivyo anajua mapito sahihi ya kupita ili kufika huko kwenye MDGS( MILLENNIUM DEVELOPMENT GOALS)
Kwani aliposaidia hizo nchi nyingi(!) alikuwa rais huko?
 
Back
Top Bottom