Inasikitisha sana, tena sana! yaani mleta mada umeandika maelezo yote hayo kisa kutetea ujinga wa kupiga mkeo!!?? Lakini inasikitisha zaidi kuona kuna wengine wanathubutu kuunga mkono hoja hii ya kuwapiga wanawake?!! Ni dhahiri kwamba una tatizo kubwa la kisaikolojia na hata uwezo wako wa kufikiri umeathirika pia. Tafuta msaada bado hujachelewa. Karne hii ya sasa bado unafikiria kupiga mwanamke? Kama una tatizo na mkeo/girl friend wako, tafuta njia mbadala ya kuleta maelewano na huyo mwenzako bila kuhusisha kipigo, hata kama ni kumpiga kibao kimoja HAPANA HAIFAI. Tumia akili zako zote, fikiri, waza, wazua, mpaka utapata suluhisho na hatimaye utatatua mzozo uliopo kati yako na mpenzi wako. Kukimbilia kipigo maana yake ni kwamba aidha huna akili, au akili unayo lakini huwezi/umeshindwa kuitumia na ukakimbilia kupiga. Umeshindwa kwa hoja na kwa kuwa huna akili kimbilio lako ni kupiga. Tambua kwamba kuna nguvu za mwili na nguvu za akili. Sisi kama binadamu hasa wanaume hatupaswi kuzitumia nguvu zetu za mwili kuwapiga wanawake. Tutumie nguvu zetu za akili kuleta ustawi na maelewano na wake/wapenzi wetu na KAMWE SI KUPIGA.
Kumpiga mkeo/girl friend wako ni ushamba, ni ushenzi na ni kuonesha kiwango cha juu kabisa cha ujinga. Hayo maguvu yako unayotambia nenda kajipatie faida kwa kufanya kazi za nguvu, kabebe zege, chimba mashimo, lima shambani, beba mizigo n,k. Huko ndiko maguvu yanakotakiwa na sio katika mwili wa mkeo/girl friend wako. Unavyotetea upigaji kwa wanawake, kwa wenye akili timamu unawadhihirishia kwamba jinis gani wewe huna akili ya kutatua mzozo na huna njia nyingine zaidi ya kupiga.
KUANZIA LEO UKOME KUMPIGA MKEO/GIRL FRIEND WAKO