Kwanini ni Bunge la 11?

Kwanini ni Bunge la 11?

Chadema subilini sisi Tulioanzisha TANU tuwape ufafanuzi wa kina, msikurupuke kwa hoja zisizo na ukweli, kazi yenu kupotosha, msidhani kila hoja inalazimishwa Tatizo lenu hamuendi Library kujisomea mnakalia kujadili ujinga ujinga hapa, SASA mtulie tuwape majibu sahihi, msije mkaanza fujo na MAANDAMANO.

Mkuu hili siyo Bunge la CHADEMA ,CCM, CUF ,NCCR ,TADEA wala TLP bali ni la Wananchi wa Tanzania.
Hivyo tafadhali mambo yako ya Uchama peleka baharini.
 
Uongo. Sina majibu sahihi lakini liwe la 10 au 11 litakua linauhusiano na vipindi vya Marais. Sasa je, kama Mwinyi, Mkapa na Kikwete wamevunja bunge mara mbili mbili na kufanya tuwe na jumla ya mabunge sijui mangapi? Je Mwalimu alivunja mara ngapi? Mi nadhani kuna uhusiano na Uwaziri mkuu, kwamba kabla ya kuteuliwa kila waziri mkuu Bunge huvunjwa na kuundwa upya. Samahani lakini

uko mbali na ukweli sababu unaukataa,je,wakati sokoine alipofariki bunge lilivunjwa au wakati lowasa alipojiudhulu bunge nalo lilivunjwa? Rais ndiye anayemteua waziri mkuu na kuidhinishwa na bunge,anaweza kutengua uteuzi au bunge likapiga kura ya kutokuwa na imani na waziri mkuu huo ukawa mwisho wake.
 
Waheshimiwa JF,

Kwanza niwapongeze mleta mada na wote waliojaribu kujibu swali hili kwa kadiri ya uwezo wao. haya ndiyo maswali yanaoijengea heshima JF na kupafanya paitwe ThinkTanker. Hongera mleta swali na hongera mliojibu.

Sasa nije kwenye swali lenyewe. Ukweli ni kwamba pamoja na jitihada za majibu yote niliyoona, swali hili halijajibiwa kikamilifu, kibaya zaidi ni kwamba hayo majibu yasiyokamilifu na yasiyo sahihi, yamepata approval (LIKE) kana kwamba yameridhisha.

Mimi ninatoa jibu sahihi lakini kwanza ninagawanya post yangu katika sehemu mbili A na B, yaani sehemu ya kwanza nitajadili MAJIBU YA WANA-JF na sehemu ya pili nitaeleza JIBU SAHIHI.

A: MAJIBU YA WANA-JF

1: Jagarld:

Jagarld kwenye Post Namba 3 amejibu akisema kuwa bunge la Jamhuri linahesabiwa kuanzia Uhuru. Kwa kiasi fulani si sahihi, kumbuka Tanganyika ilipata Dec. 09, 1961 na Zanzibar ilipata uhuru Dec 10, 1963 na ikapindua Serikali Jan. 12, 1964. Hivyo huwezi kuhesabu idadi ya mabunge kwa kuanzia siku ya uhuru.

Sasa utaona kwamba pamoja na jibu hili finyu bado kuna mtu kalishukuru kwenye Post Namba 4 akishukuru kwa jibu murua.

Kwa sababu JF ni kisima cha kufiri where people dare talk unaona kwamba Joseph Isaack japo hana jibu na yeye lakini haliamini hilo kwenye Post Namba 6

2: Charminglady

Charminglady, yeye kwenye Post Namba 7 amekuja kwa kujiamini kabisa na akatoa mchanganuo unaoonyesha kuanzoa 1961 hadi 2015. Utaona kwamba hata yeye ana makosa mawili, la kwanza nilishalisema kuwa huwezi kuhesabu kuanzia 1961 kwa sababu halikuwa bunge la Muungano bali la Tanganyika. Na hata kama Charminglady angekuwa yuko sahihi kwamba Muungano ungefanyika 1961, bado lake halingekuwa jibu sahihi maana kwa hesabu yake bunge letu hili la Anne Makinda lingekuwa bunge la 11 na si la 10 kama ukweli ulivyo sasa. Lakini naona na yeye kapata LIKE toka kwa Mimibaba and UCHAGUZI kwamba wameridhika na jibu hilo!

3: Msendekwa

Msendekwa
amejitahidi kwa kiasi chake kwenye Post Namba 9. Ingekuwa ni maksi ningempa 75%, kwa sababu anasema Bunge la kwanza la MUUNGANO lilianza mwaka 1965. Na kwa dhana yake ukiangalia utaona yuko sahihi kwani ukihesabu kila miaka mitano, ni kweli kama la kwanza lilikuwa hilo la 1965-70 basi ni kweli sasa hivi la Anne Makinda 2010-15 ni la 10.

Lakini Msendekwa na wanaoafikiana naye hayuko sahihi kwa kiasi kile kwamba Bunge la Muungano lilianza mwaka 1965. Ukisoma kitabu cha Masimulizi ya Thabiti Kombo, ukurasa wa 143, kuna kopi ya barua ya Rais wa Tanzania akimu-appoint Thabiti Kombo kuwa mbunge wa Bunge la Muungano. Barua hiyo imesainiwa na Julius Nyerere May 11, 1964.


Hivyo, bunge la Muungano lilianza May 1964 na miezi mitano baadaye yaani October 28, 1964 bunge hili la Jamhuri lilipitisha jina la Muungano liwe TANZANIA.

Hivyo, huo ndiyo upande wa usahihi na makosa ya mkuu Msendekwa.

B: JIBU SAHIHI

Baada ya kuchabua majibu ya wana-JF yaliyoelekea kushawishi forum, sasa ni kazi yangu kutoa jibu sahihi. Jibu sahihi ni lipi.

Ukweli ni kwamba na nimesema Bunge la kwanza la Muungano lilianza May 1964, hilo waliloteuliwa akina Thabiti Kombo. Hili lilidumu hadi October 1965 ulipofanyika uchaguzi wa wabunge kwa upande wa Tanganyika. Zanzibar haikuwa na uchaguzi maana Karume I, aliapa, alisema na aliandika kwamba hakutakuwa na uchaguzi Zanzibar hadi mwaka kesho yaani 2014!

Hivyo, hili Bunge la Kwanza la Muungano lililoanza May 1964 hadi October 1965 lilikaa kwa takriban miezi 18 tu. Na kama lilivunjwa kabla ya uchaguzi maana yake ni chini ya hapo ikibidi lilidumu kwa miezi 15 tu kama lilidunu hadi June 1965.

Hivyo, kwa uhai huo wa miezi 15 au 18 ambao ni chini ya miaka miwili, lilitakiwa liende hadi May 1969 bila kuvunjika ili liitwe Bunge kamili kwa mujibu wa namba hizi za Bunge. Lakini liliishia miezi 18 ambayo ni 27% ya uhai wa bunge la miaka mitano.

Hivyo, hili bunge la Muungano, halikupaswa kuitwa Bunge kamili kwa maana ya hizi namba za sasa, na kutokamilika huko ndiko kulifanya lisihesabiwe katika mabunge yaliyomaliza miaka mitano.

Hivyo, kwa hesabu ya mabunge yaliyomaliza miaka mitano tunalazimika kuanza na lile lililongia baada ya uchaguzi wa October 1965. Hivyo hili ndilo linaesabika kama bunge la kwanza yaani yamba yake ni 1. Hii ndiyo hesabu inayotueleta leo kwamba Bunge la Samwel Sitta lilikuwa la tisa na hili la Anne Makinda ni la kumi.

Naamini ufafanuzi huu hauna mashaka na unaeleweka.

Asanteni, This JF where we dare talk openly.

Cc: Dr Emma John, Mtoto halali na hela, Kimbunga, masagwa, Bagenisb, Uchaguzi, Paw, ZumbeMkuu, SDG KHOI
 
Jf bwana! Juzi baada ya lecture nilimwuliza jamaa yangu akasema hajui! Sasa napata ufahamu kwa bei nafuu! Mungu tubariki ccm itoke ili tupate habari kwa uhuru. Maana hii kuficha majina ni sababu yao! Wasituue.
 
Jf bwana! Juzi baada ya lecture nilimwuliza jamaa yangu akasema hajui! Sasa napata ufahamu kwa bei nafuu! Mungu tubariki ccm itoke ili tupate habari kwa uhuru. Maana hii kuficha majina ni sababu yao! Wasituue.

JF ni lecturer of lecturers. Wanakuja mawaziri ambao ni maprofessa humu, tena kwa kujileta wala hatuwafuati kwa sababu haijapita miaka mingi walipoisusia kwamba JF ni ya Chadema.

Viva JF. JF ni kama hospitali, ni mtakuja.
 
Umedanganya mkuu. Kwanza hakuna cha bunge la kumi wala la sita bali kuna mkutano wa kumi kikao cha 3 nk. Sababu ni kama ulivyoeleza kwenye bandiko lako la hapo juu. Ndani ya miaka mitano bunge linatakiwa likae mikutano let say 20. Lakini mkutano mmoja unaweza kuwa na vikao 50. Kwa mfano sasa kuna mkutano wa bajeti. Sjafuatilia kujua ni mkutano wa ngapi tangu bunge liapishwe 2010, sasa kila siku waliyokaa bungeni ndio kikao chenyewe.Kama ijumaa ya last week ilikuwa ni kikao cha 20 inamaana wakikaa jumatatu kitakuwa kikao cha 21 wakikaa jumanne kikao 22 wakikaa j5 kikao 23 nk. So ni mkutano wa....kikao cha....
Umekosea! Unachosema si sahihi. Kila Bunge linapochaguliwa kwa kipindi cha miaka mitano linajulikana kwa namba yake, la kwanza, la pili.....la kumi n.k. Katika hilo bunge ndiyo kunakuwa na vikao ambavyo pia upewa namba cha kwanza kikiwa kile kinachofanyika mara baada ya uchaguzi ambapo uapishwa.
 
Safi sana Nikupataje,
JF ni Jungu kuu,--
Ila tu angalia tena pale kwenye bandiko lako sehemu A inayosema hivi
´´Hivyo,bunge la Muungano lilianza May 1965´ikiwezekana rekebisha mkuu.
 
Hili ni bunge la 10, la kwanza la Muungano liliaanza 1965, kisha 70, 75, 80, 85, 90, 95, 2000, 2005,2010.
Na ni mkutano wa 11 wa bunge hili la 10, yaani,
nov 2010 lilipokutana baada ya uchaguzi, ndo mkutano wa kwanza. Kisha 2011 Feb, April, Jun, Nov, ikawa mi5, then 2012 mara 4, ikawa 9, kisha 2013 imekuwa miwili(feb na Apr) jumla 11.
Halafu vyama vingi vimerejeshwa 1992, sio 96.

Umesomeka mkuu, ubarikiwe kwa maelezo yako!
 
Back
Top Bottom