Kwanini Ngoswe alikuwa maarufu kuliko Edwin Semzaba?

Jospina

JF-Expert Member
Apr 19, 2013
2,421
1,387
Ukweli ni kwamba "NGOSWE" ambaye ni "Mtu wa Kufikirika" NI MAARUFU KULIKO "Edwin Semzaba" aliyetunga habari za huyo Ngoswe...
Bendi nyingi zimeimba "...mambo ya Ngoswe muachie Ngoswe mwenyewe..." na umekua ni msemo maarufu.
Jina "EDWIN SEMZABA" LINATAJWA sana baada ya kufariki.
kwanini waandishi wetu hawa hawavumi na kupewa sifa stahiki kama kazi zao?
R.I.P Edwin Semzaba
 
Kweli watanzania hatuelewi jinsi ya kuwakuza waandishi wetu, kama wenzetu. fikiria akina Ngungi wa thiong'o, chinua achebe nk
 
Characters ndo wanavuma ukiniuliza nani kaandika Hawa the bus driver simjui,ila namjua mhusika Hawa,vilevile Baraka na Neema,Okonkwo,Manenge na Mandawa,Bwana Bugonoka na Bibi Muyombekele,Unyoya wa kipanga Azizi,etc nadhani ni rahisi sana kuwakumbuka characters kuliko authors,
 
Ha ha ha kina Ngoswe wengi ila huyu bwazna December nadhani anafaa zaidi kuwawakilisha wenzie!
 
Back
Top Bottom