Kwanini ndoa nyingi zinavunjika

Nzega

New Member
Jun 28, 2011
4
0
Katika kipindi cha miaka mitano wilaya ya Songea pekee ndoa 500 zimevunjika kwanini idadi ya ndoa zinavunjika ni kubwa na inatisha hatujui sehemu nyingine hali ikoje
 
Ndoa nyingi zinavunjika kwa sababu wanaume tulo wengi hatupitia mafunzo yale ya unyago,hivyo wengi ni malimbukeni na hawajui maana ya kuishi na mwanamke na hwajui mwanamke ni nani?anataka nini nk.tumetawaliwa na mfumo dume wa kujiona sisi ndio sisi tunajua kila kitu hata pale tulipokosea hatutaki kukosolewa,Kwa upande wa akina dada ndo ni kama kuondoa Gundu kwa sababu ya umri au kwa sababu fulani kaolewa lakini kiukweli hawajakamilika katika maisha ya ndoa,kitchen party za siku hizi hakuna lolote zaidi ya kutumika kama sehemu ya kupatia vyombo.
 
simu za mkononi, upungufu wa nguvu za kiume, wanawake wengi wanaolewa wakiwa hawana sifa za kuwa wake.

Sababu hizi huenda zina mashiko. Cha kuuliza - je jamii ifanyeje kuhakikisha:
1. Simu za mkononi hazitumiwi kama silaha ya maangamizi dhidi ya ndoa
2. Kuongeza nguvu zaa kiume - nini kipimo sahihi kuona kama mwanaume ana nguvu?
3.Sifa za kuwa mke- (naongeza na mume)- hivi inawezekana kutengeneza hadidu za rejea kama ilivyo katika michakato mingine ( wabunge, wataalamu mbalimbali nk)
 
Katika kipindi cha miaka mitano wilaya ya Songea pekee ndoa 500 zimevunjika kwanini idadi ya ndoa zinavunjika ni kubwa na inatisha hatujui sehemu nyingine hali ikoje

Kadri hali ya uchumi inavyokuwa ngumu na wengi kukosa hela ndio majaribu katika ndoa za kweli yanavyoongeza..kile kiapo cha dhiki na raha kinakuwa karaha na hivyo wapenzi wababaishaji wanaishia njiani na kupandisha chati ya kuvunjika kwa ndoa..
 
Ndoa nyingi zinavunjika kwa kuwa wanandoa wengi hawajapata mafunzo namna ya kuishi maisha ya ndoa; hivyo kupelekea ndoa hiyo kuvunjika muda mfupi.
 
Nionavyo mimi, ndoa nyingi zinavunjika kwa sababu wasichana/wanawake wengi wanakosa uvumilivu. Na hii ni kwa sababu wengi wao hawajui maana halisi ya kuolewa - wanafikiri ni kupata sehemu ya kusaidiwa matatizo yake. Sasa akiona matatizo yake hayajasovia haoni umuhimu wa kuwa kwenye hiyo ndoa tena. Na akishakuwa na uwezo wa kuyasovu mwenyewe pia haoni umuhimu wa kuwa kwenye ndoa hiyo.
 
Back
Top Bottom