Kwanini ndoa nyingi zimekuwa magereza bubu?

Kwanini ndoa nyingi zimekuwa magereza bubu?

INSONSILE

JF-Expert Member
Joined
Feb 26, 2012
Posts
1,960
Reaction score
2,945
Ni ukweli usiopingika kuwa ndoa nyingi zina migogoro mingi sana siku hizi. Mdau mmoja aliwahi kusema zimegeuka magereza bubu bila wao kujijua na bila serikali yetu tukufu kulijua. Nyingi hazitaki tuu kufunguka kwa sababu ya social image (jamii inawatazamaje). Sasa nimefikiria na kutafakari mambo yafuatayo.
  1. Sex before marriage: Siku hizi mwanaume kuoa mwanamke bikra probability inaweza kuwa 1 kati ya 100. Mpaka binti anaolewa ameshakanyagwa vya kutosha, kama ni gari imeenda mileage ya kutosha. Wanaume nao ndo usiseme, ameshavuruga akiweka list inasoma 50++, wengine hata idadi hawakumbuki. Hebu niambie hawa wanandoa wakioana watakaaje kwenye marriage wafurahiane? Kuboreka ni fasta sana na kuenda kupasha kiporo kunakuhusu. Upande wa pili fikiria wanandoa ambao hawakuwahi kujihusisha na sex before marriage. Yaani huo utamu wanaofeel hakuna pa kulinganishia. Uwezekano wa kubaki salama ni mkubwa, unless kati yao mmoja aanze kuchepuka.
  2. Utengano wa muda mrefu: Jaribu kutofautisha wazee wetu wa zamani ambao waliishi kijijini, shughuli zake zilikuwa pale palen kijijini na mama ni hivyo hivyo. Walikuwa karibu muda mwingi sana, hapakuwa na utengano wa muda mrefu. Siku hizi mume yuko Mwanza, Mke yuko Dar au mmoja yuko Mbeya mwingine yuko Arusha. Hiyo gap ya upweke mtu atavumilia kwa kiasi gani? Ukizingatia alishaonja several times kabla. Lazima akapashe kiporo.
  3. Overworking: Wanandoa wengi siku hizi kama siyo mfanyakazi mwajiriwa basi ni mfanya biashara. Hata wakiwa wanakaa pamoja kila siku wanakutana jioni au usiku tuu kila mtu amekuja yuko hoi kachoka. Au mmoja ndo anachoka sana. Fikiria mwanaume umejipanga kweli una hamu leo anakuja mkeo anasema amechoka sana, mgongo unauma, mara anasoma anakimbizana na assignments wewe unahitaji muda wa kuwa naye, mwisho wa siku utachepuka tuu.
  4. Kukosa muda wa kutosha wa wapenzi kuchunguzana: Vijana wengi wanakurupukia mapenzi na kukimbilia kuoa kabla ya kumfahamu mwenzake. Nina mifano mingi sana, lakini kuna mdada mmoja alifahamiana na mvulana wakiwa kwenye basi, na kweli wakaja kuoana ndani ya muda mfupi. Ni binti mrembo sana lakini kwa tunaomfahamu vizuri yule binti for sure hakuwa wife material. Matokeo yake wamepata mtoto hata hajajaza mwaka wameshatengana. Nafahamu visa vingi vya aina hii, mengine ni neema ya Mungu tu iingilie kati.
  5. Kukosekana kwa vision kwenye ndoa: Wanandoa wengi hususan mwanaume anapoyumba kiuchumi au akakutana na maswahibu ya maisha, wanawake wengi ni wepesi kuwakimbia waume zao na kuanza mahusiano mapya na wengine wenye kipato. Ukweli ni kwamba mwanamke wa aina hii alikuwa hajajua vizuri maana ya ndoa.
Kwa leo naishia hapa, nitakuja kuongeza mengine nikipata muda. Welcome for additional points as well as criticisms.Nimeshikwa na usingizi
 
Threads za watu waliokata tamaa kwenye mahusiano.

Watu wanakula raha kwenye ndoa wewe unatuambia zimekuwa magereza bubu!
 
Threads za watu waliokata tamaa kwenye mahusiano.

Watu wanakula raha kwenye ndoa wewe unatuambia zimekuwa magereza bubu!

Mtu kupost mada yenye kutafakarisha haimaanishi yeye anaishi uhusika. Inaweza ikawa ndiyo, au siyo. Lengo ni kuelimishana kijamii, ukipata cha kujifunza fine take it, ukiona hakuna pia unaruhusiwa kupita kimya kimya.
Hoja yako nyepesi haiondoi ukweli kuwa kuna tatizo katika jamii yetu ya sasa. Lakini zingatia pia sijasema zote, nimeandika "nyingi". Unaweza kujihisi unafaidi raha ya ndoa wakati huo huo kuna mwingine anafaidi hapo hapo. Siku ukigundua sijui utafanyaje
 
Uoe malaya utegemee ndoa idumu?

Wewe fuata taratibu zote kabla ya kuoa uone ndoa ilivyotamu. Wewe unatumika na shetani kuwatisha watu wasioane waendelee kuzini.

Ndege kila siku zinafanya safari na kutua salama hutangaziwi ila ikitokea ndege moja ikaanguka ikaua abiria 200 itatangazwa wiki nzima dunia yote.

Vivyo hivyo kwenye ndoa.
 
Threads za watu waliokata tamaa kwenye mahusiano.

Watu wanakula raha kwenye ndoa wewe unatuambia zimekuwa magereza bubu!
umeona mkuu.. ndoa raha tupu
 
Sababu ulizo taja hapo juu ongeza na hizi

Kutokua na utayar wa kuingia kwenye ndoa, unakuta mtu anaolewa au kuoa sababu tu flani kaoa, au anashinikizwa huko kwao, pengine amekaa muda mrefu anapata presha ya ndoa anaona yoyote ajaye sawa tu anaenda utategemea vipi watu hawa wadum??

Kutokua na wenza wenye sifa zinazoishi, inafahamika kwamba kila mtu ana zile sifa anazotaka kwa yule mwenza wake, japo huwez kuta amekamailika na kua na sifa zote lakini anazo zile muhim, sifa zinazoishi n kumpendea mtu labda ukarim wake ucha Mungu wake, akili yake wengi huoa au kuolewa na watu ambao hawana hizo sifa unakuta mtu anaolewa sababu tu jamaa ana pesa anasahau kuna siku zitakosekana ina mana mapenzi ndani yatakosekana, mwanamke anaolewa sababu ya uzur wake tunasahau uzuri unakongoroka shape inapotea kabisa oa mtu sababu ya tabia, akili hata ucha Mungu wake kwamba atakua anaishi kwa kua n mwenye kuabudu na unaona kabisa akili yake ina waza maendeleo mtafika mbali

Ndoa nyingi huvunjika sababu kumekua na usiri sana ndani ya nyumba, mnapoana hakuna siri tena, mnalala kitanda kimoja mnajifunika shuka moja, mtu ana mambo ake anafanya chini chini, kuna mambo muhim lazima kama mume na mke mkae mshirikishane sio anatokea mtu alikotoka anaaamua tu nafanya mawazo yenu yawe kitu kimoja na mkubaliane,

Tamaa, hii ndio baba lao kwa pande zote mbili, ndoa nyingi zknavurugika sababu ya tamaa pia, unakuta mtu anajua mumewe hana uwezo wa kile anachotaka kutaka mambo makubwa yaliyokua nje ya uwezo wake na wa mwenzie mwishoe anaona akachepuke tu atimize azma zake za siku moja, muhim kusema na tamaa zetu muhim kuridhika na kile unachopewa

Ukweli na uwazi, wanandoa wengi hawana hii desturi ya kuambiana ukweli na kuwekana sawa, tunafaham ukwel unauma kama umekereka na jambo n heri ukalisema kabla hujalala, kaeni chini ambianeni umekosea hapa umenikera hapa jirekebishe hivo unamjenga mtu kua bora zaid, siku hizi tunaamua kupotezea tu hata mambo ya muhim ndio inakuja baadae kuteteresha ndoa,
 
Ndoa inatakiwa iwe na lengo moja,ndoa za leo kila mtu ana malengo yake na aliingia ndoani kwa sababu zake
 
Kwanza, kama jamii tufike stage tukubali kwamba ndoa siyo kitu cha muhimu wala siyo mafanikio kwenye maisha
Wengi (hasa wanawake) wanaingia kwenye ndoa ambazo hazikuwa machaguo yao ili tuu nao waonekane wamo humo. Kwenye kudai talaka wanakuwa ndio wa kwanza.

Pili, kwa wote mlio kwenye ndoa, wengi wenu bado mnaishi kama mko single, na mna behave hivo. Kizazi kijacho kitakuwa kinadhani ndoa ni sehemu ya utani na wao wataendelea kuishi hivo. Yajayo haya furahishi kwenye sekta hii.

Tatu,Naamini katika ndoa, naamini katika upendo,naamini katika kushea malengo, naamini kuwa sifa ya kwanza ya kudumu kwenye ndoa ni UVUMILIVU (wenye mipaka lakini). Naamini nikioa stakuwa perfect ila kila siku nikiamka nitakuwa naweka mawazo yangu na akili yangu kufanya ndoa niliyo nayo inadumu.
 
Biblia inasema wanaume ndio waliambiwa waishi na wake zao kwa akili. Labda mkianza kuishi kwa akili na wenza wenu itasaidia kufanya ndoa kurudisha maana yake iliyokusudiwa? Nimesema labda. [emoji41]
Chanzo cha yote ni maelekezo ya wakina mama kwa mabinti zao na hasahasa hii kauli "nenda kaishi na mume wako kwa akili"
 
Ndoa bora haiji kwa miujiza bali nimatokeo ya mipango.

Mke mume watumiapo busara na hekima kupanga kua na ndoa nzuri bila shaka watakua na ndoa bora.
 
Kuchepuka is a must kwa sababu ki wastani watu wakiwa katika ndoa zaidi ya miaka 5 au zaidi tayari watakuwa wameshaboreka haswa wakishazaa. Mwanamme anafikiri kutoka na house girl au jirani huku mwanamke anaweka penzi zaidi kwa watoto na hujisahau mpaka anakuwa na mtambi shinda kalio lake. Mwanamme gani atakaa na mwanamke asiyejitunza/kujipenda?
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
Threads za watu waliokata tamaa kwenye mahusiano.

Watu wanakula raha kwenye ndoa wewe unatuambia zimekuwa magereza bubu!
 
Nilitegemea mwisho wa post yako uje na suluhisho la kuondokana na hayo uliyoorodhesha.

Asante kwa story.
 
Kwanza, kama jamii tufike stage tukubali kwamba ndoa siyo kitu cha muhimu wala siyo mafanikio kwenye maisha
Wengi (hasa wanawake) wanaingia kwenye ndoa ambazo hazikuwa machaguo yao ili tuu nao waonekane wamo humo. Kwenye kudai talaka wanakuwa ndio wa kwanza.

Pili, kwa wote mlio kwenye ndoa, wengi wenu bado mnaishi kama mko single, na mna behave hivo. Kizazi kijacho kitakuwa kinadhani ndoa ni sehemu ya utani na wao wataendelea kuishi hivo. Yajayo haya furahishi kwenye sekta hii.

Tatu,Naamini katika ndoa, naamini katika upendo,naamini katika kushea malengo, naamini kuwa sifa ya kwanza ya kudumu kwenye ndoa ni UVUMILIVU (wenye mipaka lakini). Naamini nikioa stakuwa perfect ila kila siku nikiamka nitakuwa naweka mawazo yangu na akili yangu kufanya ndoa niliyo nayo inadumu.
Thumbs up Shem...[emoji6]
 
Back
Top Bottom