Kwanini ndoa nyingi leo zimejaa migogoro?

Kwanini ndoa nyingi leo zimejaa migogoro?

Tamalisa

JF-Expert Member
Joined
Feb 3, 2015
Posts
2,542
Reaction score
907
Habari,

Katika soma soma yangu mtandaoni, nimekutana na hii makala, kwa yule ambaye hajawahi kuiona na kuisoma inaweza kuwa msaada kwake kwa namna fulani.

Kwanini ndoa nyingi leo zimejaa migogoro?

Ndoa katika jamii za kikristo zilikusudiwa kudumu na kuwa mfano wa kuigwa na ndoa za watu wengine katika jamii. Lakini cha kushangaza ndoa nyingi leo za kikristo zinavunjika kwa kasi ya kushtusha. Hii inashtusha na kushangaza kwa sababu sisi kama wakristo tumeacha kutembea katika mpango kamili wa Mungu. Kwanini hali hii inatokea? Kuna sababu nyingi kwanini ndoa zinakuwa na migogoro isiyoisha na ningine kutawanyika. Kuna sababu ndogo ndogo na zingine ni kubwa na za msingi.

Zifuatazo ni baadhi ya sababu kwanini ndoa nyingi siku za leo zimejaa migogoro, malumbano na kuvunjika.

USIOE AU KUOLEWA KWASABABU YA KUMSAIDIA MTU FULANI AU KUMUONEA HURUMA

1. Kuoa au kuolewa na mtu kwasababu ya kumuonea huruma

  • Kuoa au kuolewa na mtu kwa sababu ya kumuonea huruma ni moja kati ya sababu zisizo sahihi. Na inaonekana kuwa ni sababu moja ya kijinga pia.
  • Ndoa zianazo oana kwa misingi ya kumsaidia mtu au kumwonea mtu huruma huwa hazina maisha.

2. Huruma ya kujiona kuwa ni wewe ndio unawajibika

  • Kumhurumia mtu na kujiona kuwa una wajibu wa kumsaidia ni vizuri, lakini kuolewa naye kwa sababu hiyo ni wazi kuwa ni jambo lisilo la hekima kabisa.

3. Ndoa niyathamani Kuliko Huruma ya Mahusiano

  • Ndoa ni kitu cha thamani zaidi kuliko mahusiano ambayo yamejijenga katika huruma.
Chukulia kwamba kama mhusika ana masaa sita tu kuishi baada ya ndoa. Kwa hiyo utaishi katika ujinga huo kwa masaa sita tu maana kinyume na hapo utaishi maisha yako yote ukiwa unajihisi mjinga zaidi na mwenye huzuni.
  • Hiyo itakuwa ni sabau ya kuvunjika kwa ndoa hiyo kwa sababu utaonekana mbaya zaidi ya kabla hujaingia.

4. Kuoa au kuolewa kwajili ya kumsaidia mtu anayeteseka

  • Usioe au kuolewa na mtu eti kwasababu unaamua kumsaidia kutokana na shida Fulani
· Mfano kuna baadhi ya watu utakuta mwanaume anaamua kumuoa msichana fulani eti kwasababu kule anakoishi wanamnyanyasa na kumtesa so anaamua amsaidie amuoe ili aishi naye.
  • Hii ni sawa na ile ya ujinga wa kufikiri kwamba utaoa au kuolewa na mtu kwa matumaini kwamba utambadilisha mtu baada ya kuolewa au kumuoa ili afanane na wewe, dini yako au tamaduni zako.
  • Kumbuka kwamba, kuwa na jitihada za kukubaliana sio kubadilika, sababu suala ndoa halina haja ya kuweka mabadiliko kwa mtu yeyote.
  • Ukitaka kumbadilisha mwenzi wako usisubiri kwenda kumbadilishia ndani fanya hayo mabadiliko kabla ya kuingia ndani.

Na Mchungaji Peter Mitimingi
 
sawa kabisa, ila kibaya zaidi vijana wamekuwa sio wenye imani na dini tena.... hawana uoga kwa mungu!
 
tatizo kuu ni kwamba wanawake wanahamasishwa kuwa wana haki sawa na waume zao, kwaiyo ni kama vile tu ambavyo fahari wawili hawawezi kuishi zizi moja. Huu utamaduni wa kizungu wenyewe unawashinda na ndio maana wana ndoa za mikataba na wakifikisha miaka mitano wana fanya annivesary kubwa sana kusherekea.,

zamani ndoa hazikuwa na migogogro coz women were submissive to their husbs kwa kila spect. ukweli ndio huo
 
Wasichana wa siku hizi hawafundishwi na wazazi wao jinsi ya kuishi ndoani.
Wengi wao wanaishi maisha ya kuiga kwenye movie.
Mtu anavaa kama kahaba afu anategemea siku akiolewa atabadilika.
Mtu anaongea maneno machafu kama mdomo huo hautumiki kuingiza chakula tumboni afu anategemea kuolewa.
Mtu hamchi Mungu hana upande haijulikani kama yuko kwa Shetani au Kwa Mungu
 
Hihihiiii
 
Ni kweli mkuu ila sasa mabadiliko ndio mtihani
 
...kwa Wakristu; Biblia inamafundisho mazuri kuhusu maisha ya ndoa takatifu! Lakini wanadamu wa siku hizi' wakizazi cha .COM hawana mpango wa kuisoma biblia na kuielewa!
 
Japo nahisi shetani ameniteka kwa muda wakati naandika hii comment.
Mimi nadhani ndoa zimekuwa out dated tunahitaji ustarabu mwingine.
 
Wasichana wa siku hizi hawafundishwi na wazazi wao jinsi ya kuishi ndoani.
Wengi wao wanaishi maisha ya kuiga kwenye movie.
Mtu anavaa kama kahaba afu anategemea siku akiolewa atabadilika.
Mtu anaongea maneno machafu kama mdomo huo hautumiki kuingiza chakula tumboni afu anategemea kuolewa.
Mtu hamchi Mungu hana upande haijulikani kama yuko kwa Shetani au Kwa Mungu

Ndoa haibebwi na wasichana tu ndoa ni ya watu wawili mme na mke. Vijana wa kiume wa siku hizi nani anawafunda? Zaidi ya kudanganyana vijiweni? Au unazungumzia ndoa za jinsia moja ya ke? Fundeni vijana wenu wakike kwa wakiume wajue majukumu yao
 
mhmm ila kweli....
 
Back
Top Bottom