unahitaji msaada wa kisaikolojia.
Back to the topic baadhi ya wanaume ni kama wanyama hawana utu. Ila bora ungeomba msaada kwa marafiki wa mama yako,
Mara nyingine unaweza kujiuliza kwanini mtu kachagua ID fulani, Unaweza
kucheka, kuchukia au kubaki kawaida na maswali yako. Kwa upande wangu
nastahili kuitwa/ kujiita mcharuko. Naongea kutoka moyoni kwa sababu naamini
ni Mungu pekee ndo ananijua vizuri kwa wengine hapa jukwaani nitaendela kuwa
kivuli.
Mwk 2001 nikiwa kidato cha kwanza nilifiwa na mama yangu mzazi. Nilikuwa mtoto
wa pekee kwa baba na mama. Nikabaki na baba peke yake ambaye mara nyingi
alikuwa anasumbuliwa na maradhi ya kisukari hadialipopoteza maisha miaka miwili
baadae. Tayari maisha yalishakuwa magumu lakini baada ya kufariki baba ugumu
ulizidi.
Mara nyingi nilikuwa naenda kuomba misaada kwa marafiki wa karibu wa baba
Wengi wao walinisaidia lakini wakaanza kunitongoza. Sielewi ni kwanini wakati baba
yuko hai nilikuwa mtoto wao lakini baada ya kifo cha baba wakaanza kunifanyia
hivyo. Asilimia 90 ya wanaume niliowaomba msaada walinitongoza. Nilikuwa sina
jinsi. Wengi nilifanya nao...... lakini hawakunisaidia tena baada ya msaada wa kwanza
na wao kupata walichohitaji.
Toka Muda huo maisha yangu yamekuwa ni ya kuuza mwili wangu mpaka mwaka
2008 ambapo nilijiunga na chuo cha Elimu ya Biashara CBE. Hapo sikuwa na jinsi
ndo nikaingia kwenye biashara rasmi ya uchangudoa. Sitatokea kumpenda mwanaume
maisha yangu yote. Na hata pale nilipoleta thread kuhusu wanaume wafupi
nilikuwa nimezungumza kutokana na uzoefu nilioupata kutokana na biashara hiyo.
Najitahidi kuileta akili yangu katika hali ya kawaida ili niwapende wanaume lakini nashindwa
kwangu mwanaume ni mteja na mtu katili asiye na huruma. Nawachukia nawachukia
kutoka moyoni.
Rafiki wa karibu wa baba yangu ambao nimetembea nao mpaka sasa ni 5. Hivi
kweli kuna haja ya kuwa na imani na wanaume?