Kwanza tuweke mambo sawa tozo ni aina ya kodi. Hivyo tusiongelee tozo kama vile sio kodi.
Mimi binafsi sijaona ubaya wowote wa serikali kuweka tozo na nina fikiri hakuna njia nyingine kwa wakati huu zaidi ya tozo na nitajaribu kuweka hoja hapa vizuri. Tanzania kama nchi inayoendelea inahitaji pesa ili iweze kuwekeza kwenye miradi mingi sana kuanzia elimu, maji, barabara, umeme, kilimo, ulinzi, n.k
Sasa vyanzo vya mapato ni hivi;
Kuna miradi tunalipia kwenye kodi kama ya maji na umeme lakini wakati wa Kikwete pesa karibu yote ilikuwa ni kulipa mishahara na matumizi ya serikali.
Sasa kama nchi tuko kwenye kipindi cha uwekezaji kwa mara ya kwanza tunaanza kuona barabara za kisasa, shule bora, hospitali na umeme hasa vijijini. Sasa tumefikaje hapa ? Ni kuwekeza kwa kodi mpya na tozo.
Umeme mfano wa vijijini umepelekwa na tozo maalamu kwenye luku za nyumbani na barabara za vijijini nyingi zinatengenezwa na tozo kwenye mafuta. Lakini ili kama nchi tuweze kuwekeza na kuongeza walipa kodi ni lazima tuwekeze kwenye kilimo.
Kilimo kitaongeza mapato kwenye kodi lakini tatizo hatuna mfumo mzuri wa kilimo kuwa na uazalishaji wa uhakika. Bashe amekuja na mpango mzuri wa kuongeza uzalishaji kwa kufanya yafuatayo (1) Serikali itatoa ruzuku kwenye mbolea (2) Serikali itawekeza kwenye umwagiliaji (3) watatoa mbegu (4) watafuta wawekezaji wa viwanda (5) kutafuta masoko.
Hii ndiyo mojawapo kubwa ya kuongeza ajira na kodi lakini mtaji wa yote haya ni karibu Trillion moja sasa mtaji unatoka wapi? Hii ndiyo sababu imeenda kwenye tozo hivyo tozo ni muhimu kwasababu ni mtaji wa uhakika wa kuongeza kodi kwa miaka ijayo. Lakini ni tukiangalia vizuri tatizo letu ni utamaduni mbovu watu wengi walizoea kukaa bila kulipa kodi wala tozo.
Mimi ni diaspora wa muda mrefu sana na naishi na kutafuta maslahi yangu jimbo la Texas. Hili jimbo letu linajulikana kwa kuwa na kodi ndogo lakini ngoja niwape data kidogo ili mgundue tonavyolipa kodi.
Kuna ambao watasema huko Ulaya na US pesa inaonekana ni kweli tuna shule kwenye kila mtaa za watoto zina mabasi na ni bure lakini tunalipa 3% kwenye thamani ya nyumba na pesa inaenda huko. Hivyo hoja ni yaanze mayai au kuku lakini kodi ni muhimu na maendeleo ni muhimu.
Ndiyo maana hoja yangu ni kwamba tozo ni muhimu kwasababu ni mtaji na utaratibu mpya wa kuongeza wigo la walipa kodi na kuweka mifumo ya kimaendeleo.
Tatizo kubwa ni mazoea ya watu wengi walikuwa wamezoea kukaa bila shughuli na kubangaiza lakini kama tunataka umeme vijijini, barabara za lami na hospitali ni lazima zitengenezwe, kuwe na pesa za matengenezo kila mara na pesa za wahudumu.
Ni lazima kuwe na mfumo wa mapato na wananchi ni lazima wazalishe ili waweze kuwa na mifumo hii. Huwezi kukaa kijijini hulipi kodi yeyote, huzalishi chochote halafu unahitaji barabara, maji, umeme ... pesa inatoka wapi? Ni lazima serikali iwekeze kwenye kilimo ili wewe mwanakijiji uweze kuchangia kodi na maendeleo na ndicho kinacho fanyika kwa sasa.

- Missada kutoka nje
- kodi na tozo
- mikopo

- Nyumba kila mwaka nalipa 3% ya thamani ya nyumba. Hivyo kwa mfano kama nyumba pale Tanzania yenye thamani ya Tsh 100,000,000 basi unatakiwa kulipa kila mwaka Tsh 3,000,000. Hakuna mjadala kwenye hili na usikolipa unapekwa mahakamani na nyumba inapigwa mnada.
- Jumuia na majiradi vilevile wana kitu kinaitwa HOA-Housing Owners Association hii ni jumuia ya makazi yako na majirani kila nyumba inalipa $350-$1000 kwa mwaka kwa usafi wa jumla kama kukata majani na kusafisha mitaro. Hii ni nje ya nyumba yako hii nayo ni lazima na kisheria wanaweza kwenda na utaratibu mpaka wakapiga mnada nyumba.
- Tuna tozo za maji na kuchukuwa taka. Kila wiki wanapita kuchukuwa taka kwenye magaloni maalumu. Hii inafanywa na manispaa huwezi kuchoma matakataka ovyo ovyo. Maji unalipa kutokana ma matumizi lakini taka utalipia unataka au hautaki jumla sio chini ya $100 kila mwezi. Ukitupa uchafu ovyo ni faini, usipoweka uchafu vizuri kwenye mifuko ni faini.
- Barabara nyingi zinajegwa kwa mikopo inayoitwa goverment bonds hivyo ni lazima ilipwe. Kila nikienda kazini kwa mfano ni lazima nipitie kwenye barabara za kulipia "toll roads" na natumia sio chini ya $5-$7 kwenda kwa siku moja na kurudi. Tena hii ni rahisi New York wanatumia $12-$15.
- Ukienda kwenye hotel na kokodi chumba karibu 35% ni kodi na tozo, kwenye simu, cable za TV au Dish hivyohivyo.
- Kwenye super market kila ukinunua kitu kuna 5% ya tozo inaenda kusaidia “Metro" ambayo ni kama mwendo kasi yetu.
- Lakini hapa kuna bima ya karibu kila kitu nyumba ni lazima uwe na bima na kwenye hizi bima kuna pesa zinaenda kusaidia idara kama zimamotto na ambulance.