Kwanini nashabikia mapinduzi ya UKAWA

Kwanini nashabikia mapinduzi ya UKAWA

Tunaopenda mabadiliko tuendelee kupiga kelele mpaka masikio ya baadhi ya watu yafunguke. Hoja za kutoipa CCM kura ziko wazi kabisa. Lakini inasikitisha kuna watu humu hata ungekesha unajenga hoja hawatakuelewa. Ni kama walevi waliopindukia. Wao ni ushabiki tu. Tukiondoka hapa jamii forum wote tunalala gizani, tunakunywa maji ya visima, tunapeleka wagonjwa kwa waganga wa kienyeji badala ya hopspitali, nk. Lakini tunapoongelea mabadiliko, utawasikia baadhi yetu hasa hawa "Mashabiki" wanaanza kupiga ramli kuhusu UKAWA, eti hawana hakika na sera zao, au viongozi wao, nk. Nchi hii itaendelea kuogelea katika lindi la umasikini kwa muda mrefu sana kama tutaendelea kuwa na kundi kubwa la watu wenye fikra hizi. Ni lazima tufike mahali kama sera za serikali tuliyoipa kura hazifanyi kazi kuondoa matatizo yetu, tuikatae serikali hiyo kwa nguvu ya kura zetu. Hiyo ndiyo njia pekee ya kuhakikisha wale tunaowapa mamlaka kupitia kura zetu wanakuwa na nidhamu na kutekeleza kwa vitendo yale wanayoahidi. La sivyo tutaendelea kuishi kwa matumaini mpaka lini?
 
Ukawa kipindi cha kina Dr Slaa na professor Lipumba ilikuwa inajulikana inaenda wapi na angalau itafanya nini. Sio hii ukawa ya mtoswa ccm

Exactly kiongozi, UKAWA ya Mbowe, Lowassa, Mbatia na Sumaye imekosa mwelekeo. Nilikuwa mfuasi wa itikadi zao hapo mwanzo. Leo hii sioni wanachofanya zaidi ya kutafuta kula...
 
Mpaka sasa sijaona kwanini niipigie kura ukawa??
Ukawa sera yenu ni nini?? Utaambiwa mabaya ya CCM tuuu!!!
Nataka kusikia ukawa mtafanya nini??

Kama hujaona kwann ipigie kura ccm, huwez ona umuhimu wa kuwa na taifa lililo imara katika misingi ya kiuchumi,afya, elimu..etc
 
Mimi kura yangu ukawa. Hivi nyie mliopigwa upofu. Ni mwaka jana tu serikali ilichakachua katiba pamoja na kugharamia mabilioni yote hayo.

Kimsingi kabisa sio kwamba naipinga kwamba haijafanya chochote CCM.

Ila Kuna mambo ya hovyo na ya hasara yanafanyika kila mwaka kwenye taifa Hili sababu ya hawa watu kulewa madaraka.

Kama kweli tuna dhamira ya utanzania na kujali maslahi ya kizazi kijacho, ni bora watanzania tuungane tufanye sub dakika hii ya themanini CCM apumzike kidogo.

Ama hakika tusipoamua sasa na kupata watu wa kuotesha misingi imara juu ya maslahi yetu ya kitaifa kama utajiri wa asili tulionao.

Hakika huko tunapoenda faida zitazidi kuwa ndogo kuliko madhara.

Ukiangalia mambo yanayotokea duniani kwa sasa ni dhahir kama taifa halitajipanga kwa miaka kumi ijayo hakika wengi watasaga meno.

Tufanye maamuzi sahihi, miaka hamsini hawa watu wametutawala lakini cost zimekuwa kubwa kuliko benefits. Hivi vilio vya kila siku sio bahati mbaya uongozi wa taifa hili haukuwahi kuwa na manufaa yoyote kwa wananchi wa kawaida.

Hata nimefanya simple research ya uchumi wetu tangu enzi za mwalimu hakika hakuna kitu.

Kuna watu wamepigwa upofu lakini watambue pale madhara yanapotokea ni wote tunahathirika.

Hakika hii chance tukipoteza hawa hawa viongozi watu ipo watatuambia si ni wasengerema

mapinduzi ya ukawa ni mapinduzi ya kumuondoa Dr. slaa na kumweka Lowassa
 
Ujue Ukawa Mnapata Nguvu Na Kujinasibu Kutokana Maneno Ya Nyerere Ya" Watanzania Wanahtaj Mabadiliko Na Wasipopata Ndan Ya Ccm Watayatafuta Nje Ya Ccm"na Watz wachache walivo connect na matatizo yao wakaamin ukawa ndo solution lakin wakasahau Nyerere Huyohuyo Alisema "mabadiliko Ya Kwel Yatapatikana Ndan Ya Ccm"na Wakat Huo Ndo Sasa...Ukawa Ni Kwel Inataka Kuleta Mabadiliko Lakin Hayatakua Ya Kwel,hata Sis Tumejionea Kama Mtu M1 Anaweza kuja na Kuparanganya Mising Yote Ya Chama Si Zaid Wakichukua Nchi,watakua Wanasimamia Lip Kama Mising Yao Wenyewe Wameshndwa Kuisimamia?
 
Hao ukawa ndo hamna kitu kabisa. Hamna watakacho kifanya zaid ya kuanza kukwapua na kulipa visasi ambavyo havitakuwa na tija yoyote kwa nchi kama nchi.

# UKAWA na chadema mmekosa demokrasia ya kweli ndani ya chama, kama mlishindwa kuteua mgombea uraisi kwa kufuata misingi ya kidemokrasia ndani ya UKAWA, mnathubutu vipi kuja kwangu kuniomba kura? Kwa sababu hii siwezi kuwapa kura yangu. Kama alliance imekosa demokrasia, sidhani kuwa mnaweza kuongoza nchi kidemokrasia.
# Kile mlichokuwa mnaimba kila siku majukwaani, mkiongozwa na Dr. Slaa, Lissu, Mnyika na wengine kuhusu ufisadi ambao limekuwa kero kwa wananchi walio wengi, huku mkiaminisha umma kuwa baadhi ya viongozi ndani ya CCM ni mafisafi papaa, leo hamuwezi tena kuwasema, bali mmeungana nao. Hilo ni dhahiri kuwa mpo kimaslahi na sio kulipigania taifa. Ndio wale wale tu hakuna tofauti. Sioni sababu ya kuwapa kura yangu.
# UKAWA haina sera, zaidi ya kuongea kuitoa CCM madarakani, sioni sera wala mkijinadi kwa sera. We need to know what you'll do to the people of this nation, tuna kero nyingi...hatutaki hadidhi za kuuchukia umasikini huku hamna strategies za kuuondoa umasikini.
# Nina wasiwasi na afya ya mgombea wa UKAWA, Mimi sio Mungu lakini ni dhahiri kuwa kiafya Lowassa hayuko sawa, haruwezi kuweka mtu ambaye afya yake ni tatizo, nchi inagitani kiongozi mwenye afya imara ili atumie nguvu, busara, uwezo na ajili zake zote kutuongoza. Kwa sababu hiyo pia, siwezi kumpa kura yangu.

tatizo hapo si UKAWA bali mtu waliomuweka kupeperusha bendera ya ukawa. ccm A kwa ccm B bora ya ccm A.

Yawezekana mme ni quote kwamba mimi ni kada wa upinzani. Hapana mimi sio kada.

Ila mimi ni raia wa kawaida tu ambaye nimejiridhisha beyond no doubt kwamba raia tunahitaji mabadiliko ya kisiasa na fikra nje ya system msonge ya CCM.

System ambayo kwa miaka 50 imetengeneza bomu la mparanganyiko na maovu katika jamii yenu kitanzania.

System iliyotengeneza viongozi wabinafsi na wala rushwa wa wazi wazi.

System ya viongozi wenye ahadi za uongo kwa jamii yao na kudanyanya waziwazi.

System iliyoleta uduni katika elimu na kufanya watu wawe vipofu wakujua hasa taifa linaelekea wapi.

System iliyoshindwa kutumia potentiality ya utajiri tulionao kama nchi kuwa na sound economic growth.

We unafikir ukiwa mwana ukawa tu ndo unaweza kuona mambo kama haya. Yeyote anaweza kuona kama ukikaa chini na kufikiri kwa dhati hata ukiwa huko CCM.

Ni kwamba waweza baki na chama chako kiwe CCM au whatever Ila unatakiwa kujua kwamba nchi inahitaji mabadiliko na inahitaji watu wenye maono. Over
 
Back
Top Bottom