kalulukalunde
JF-Expert Member
- May 27, 2016
- 1,056
- 1,086
WAKATI mwingine huwa nastaajabu mambo ya Watanzania. Sidhani kama kuna mtu atapiga hatua yoyote kimaendeleo hapa nchini, endapo atakuwa anawasikiliza Watanzania.
Ipo mifano mingi ya kueleza tabia hii ya ajabu ya Watanzania. Kwa mfano, wakati wa utawala wa Rais Jakaya Kikwete, wapo waliolalamika kwamba alikuwa mpole sana. Leo amekuja Rais John Magufuli, wapo Watanzania wanaolalama kwamba ni mkali sana. Haohao ndiyo walikuwa wakisema ili iendelee Tanzania inahitaji kiongozi mkali.
Nimekumbuka haya baada ya kusoma katika mitandao mbalimbali ya kijamii wiki iliyopita, ambapo watu mbalimbali wanalaumu hatua ya kuwekwa rumande kwa mfanyabiashara maarufu hapa nchini, Yusuf Manji, kwa maelezo kuwa kuna athari kwa uchumi wa taifa.
Manji anaandikwa kwa sababu ya umaarufu wake lakini yeye ni mmoja tu wa wafanyabiashara wengi wakubwa hapa nchini ambao serikali ikifanya kazi yake sawasawa, inaweza kujikuta ikikusanya mapato zaidi.
Badala ya serikali kuogopa kushindana na wafanyabiashara, nadhani pona yetu kama taifa ni kuhakikisha kuwa kila mtu anakuwa na haki na wajibu sawa mbele ya sheria. Hili liwe kwa wote, hasahasa kwa matajiri ambao mchango wao kwa uchumi wetu ni mkubwa.
Tukubaliane jambo moja kwamba hali yetu kiuchumi bado ni mbaya. Pamoja na juhudi zote ambazo serikali ya Rais Magufuli imefanya, bado kuna mianya inaweza kuzibwa na kutuongezea fedha nyingi zaidi.
Ripoti ya karibuni zaidi ya Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imeonyesha kwamba matarajio yake ya ukusanyaji kodi kwa mwaka 2016/2017 hayakufikiwa na kwamba inahitaji kutafuta takribani shilingi trilioni mbili zaidi katika mwaka ujao wa fedha.
Nakisi hii katika makusanyo imefikiwa wakati serikali imefanya juhudi za aina mbalimbali katika kuongeza mapato na kupunguza matumizi yasiyo ya lazima na kupunguza wizi na rushwa.
Kwa mfano, serikali imepunguza wafanyakazi hewa waliokuwa mzigo mkubwa serikalini kiasi kwamba hadi sasa imeokoa zaidi ya shilingi bilioni 25 kwa eneo hilo moja pekee.
Katika kuzimua uchumi wa nchi, serikali pia imefanya mambo mazuri kama vile kutoa msamaha wa Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) kwa bidhaa za uzalishaji na zile ambazo zinapita tu hapa nchini lakini hazitumiwi.
Serikali hii pia imeongeza ukusanyaji wake wa mapato kutoka shilingi bilioni 800 kwa mwezi ilizokuwa ikikusanya miaka miwili iliyopita hadi wastani wa shilingi trilioni 1.2 hivi sasa.
Pia, katika hatua inayoelezwa kuwa ya ubunifu wa kipekee, serikali ya Rais Magufuli iliondoa gharama za leseni ya matumizi ya barabara na badala yake kuiweka katika bei ya mafuta ili kukuza wigo wa mapato na pia kupunguza matumizi.
Pamoja na jitihada zote hizo za serikali, bado kuna nakisi na ndiyo maana ni muhimu kwa serikali kutafuta kila namna ili kuziba pengo hilo na ni wazi wafanyabiashara wakubwa wa ndani wana sehemu kubwa katika hilo.
Labda kuna watu wanamfahamu Manji kwa nafasi yake ya Uenyekiti wa klabu ya Yanga lakini huyu ni mmoja wa wafanyabiashara wakubwa zaidi waliopo hapa nchini.
Kushadadia hoja yangu hii, ni muhimu nikaweka baadhi ya takwimu halali za mwaka 2013 zinazoonyesha namna makampuni ya Manji yalivyofaidika na biashara mbalimbali hapa nchini.
Katika mwaka huo pekee (2013) makampuni yaliyokuwa yakimilikiwa na Manji yalishinda zabuni zifuatazo za kibiashara. Makampuni hayo na thamani ya zabuni walizoshinda kwenye mabano ni Golden Globe International Services Ltd (USD 44,816,255.07- shilingi bilioni 90), Quality Trade and Distribution Ltd (USD 5,572,947.45 – shilingi bilioni 10), Quality Motors Ltd – EUR 38,835.37 na TZS 24,376,600- takribani shilingi milioni 150) na Intertrade Commercial Services ( USD 19,978,706.46- shilingi bilioni 40).
Kuna maswali kadhaa ambayo yanahitaji kuhojiwa kutokana na namna makampuni ya tajiri huyu mmoja (ambaye ni mfano wa matajiri wengine) yalivyoweza kushinda zabuni hizi.
Kwa mfano, hakuna mtu yeyote –vikiwamo vyombo vya habari maarufu hapa nchini, ambavyo viliwahi kuhoji endapo kiasi hicho cha fedha kilichopitishwa ndicho hicho kilichotumika katika matumizi yaliyopangwa.
Hadi sasa, hata wale ambao wanalaumu wakati wafanyabiashara wanapokamatwa au kubanwa, hawana ushahidi endapo kodi stahiki kwa taifa zililipwa wakati huo au ndiyo zilizotoroshewa kupitia ofisi nyingine za mfanyabiashara huyu zilizopo katika nchi zinazofahamika kama pepo za wakwepa kodi.
Kuna wakati, kwenye ushindanaji wa zabuni, Manji alifanikiwa kushindanisha makampuni yake yaliyosajiliwa ndani ya nchi; yaani Quality Trade and Distribution na Intertrade, ambayo imesajiliwa nje ya nchi katika pepo hizo za wakwepa kodi.
Jambo la kushangaza ni kwamba hata wale ambao wanawatetea wafanyabiashara wa Tanzania na wa kigeni wanaofanya shughuli zao hapa, na Manji ni mmoja wao tu, hawasemi kitu kuhusu mambo kama haya.
Kwenye hili suala la kuwa na makampuni yaliyosajiliwa katika pepo ya wakwepa kodi, Yusuf Manji wala hayuko peke yake miongoni mwa wafanyabiashara wa Tanzania kama ambavyo ripoti ya karibuni iliyofahamika kwa jina la Panama Leaks ilivyoonyesha.
Kwenye ripoti hiyo ya uchunguzi, Manji na mfanyabiashara mwengine maarufu, Rostam Abdulasul Aziz, walionekana kuwa na fedha nyingi zilizohifadhiwa nje ya nchi; ikimaanisha utajiri wa Tanzania unaohifadhiwa nje ya nchi.
Kwa vyovyote vile, kama kweli tunataka serikali ya Rais Magufuli ifanikiwe katika vita yake ya kukusanya mapato ya serikali popote pale yalipo, hakuna namna zaidi ya kumuacha ashughulike na wafanyabiashara hao wakubwa.
Vinginevyo, jitihada zake zote nyingine zitakuwa sawa na kutwanga maji kwenye kinu.
Raia Mwema