Kwanini nachangia CHADEMA Tsh 150,000 - Match mine or beat it!

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Mar 10, 2006
33,478
39,996
Habari kutoka kijijini,

Kuna mwamko mkubwa ambao haujawahi kutokea na nimeona nami nitoe mchango wangu japo kidogo. Baadaye kesho nitawasilisha mchango wangu huo ili kusaidia japo kiduchu katika kuwapa nafasi Chadema ya kufanikiwa. Kwa vile kampeni hii ina gharama kubwa sana ya kifedha naamini bila michango ya wale wanaounga mkono au kushabikia mabadiliko kujitoa kwa namna moja au nyingine.

Ninatoa changamoto kwa yeyote (hata wasiokuwa wanachama wa Chadema kama mimi) kuchangia chochote walicho nacho. Ninawashukuru wale ambao tangu asubuhi wamepokea wito wangu huo kupitia magazeti makubwa mawili nchini. Jaribu kufikia kiwangu changu hicho au jaribu kunipita. Lakini vile vile haijalishi kiasi chochote ulichonacho changia ili angalau uweze kusema kuwa na mimi nilisaidia kununua machungwa ya kusaidia timu ishinde!


Kuchanga ni kuchagua na kuchagua ni kuchangia!

Mabadiliko hayaji kwa kusubiriwa, kuombewa au kungojewa; mabadiliko yanaletwa!

Sehemu katika makala zangu za leo inatoa maelezo yafuatayo:

Kwa kuchangia Chadema tuma neno "Chadema" kwenda namba 15710 na utakuwa umechangia shilingi 350 kwa kila sms. Hii ina maana gani? Ina maana leo Jumatano wasomaji wapatao elfu kumi tu wakiamua kutuma sms moja tu kwa siku watakuwa wamechangia shilingi milioni 3.5! Na hao tu wakiamua kuchangia kiasi hicho hicho kwa mfululizo wa siku saba (yaani mara moja kila siku) hadi Jumanne ijayo watakuwa wamechangia shilingi milioni 24! Itakuwaje kama wataamua kuchangia mara mbili au mara tatu? Kwa wale wengina nao wanaweza kuchangia kununua "machungwa" kwa kutumia M-Pesa kwa kutumia namba hizi 0758 22 33 44, 0764 77 66 73 au kwa kutumia Benki akaunti ya Chadema M4C - CRDB 0J1080100600 au MNB ni akaunti 2266600140.

Pendekezo langu kwa wale wanaotaka kuchangia ni kutuma neno hilo kwenda hiyo namba, halafu wawatumie marafiki na jamaa zao kwenye simu jumbe kuwa "nimechangia mabadiliko kwa kuchangia Chadema; nawe changia: Tuma sms yenye neno "Chadema" kwenda 15710 uchangie mabadiliko". Nina uhakika kabisa, Watanzania wanaotaka mabadiliko wataona tofauti mitaani; wataona mabango zaidi ya Dr. Slaa, wabunge na madiwani katika siku chache zijazo. Lakini hilo halitatokea kwa kuombewa au kungojewa.

Lakini wale ambao nao wanaona kuwa Chadema haifai kupewa nafasi ya kuongoza na kuwa CCM inatakiwa iendelee kutawala na wao wana haki ya kukichangia kabisa chama hicho ili kiendelee kututawala. Ni lazima wachangie kwa kufuata dhamira zao wala wasione aibu. Si lazima wote wachangie upinzani kwa kufuata mkumbo! Anayechangia CCM achangie kwa sababu anaamini kwa dhamira yake kuwa kwa kufanya hivyo ni vizuri kwake na kwa watoto wake. Na yule atakayetaka kuchangia Chadema au chama kingine naye afanye hivyo hivyo bila ya kumuomba mtu msamaha au kutoa maelezo kana kwamba anafanya uhalifu.
 
Hongera Mwanakijiji.

Kama kutatokea mabadiliko Tanzania wewe binafsi utakuwa umetoa mchango mkubwa sana kusaidia harakati hizi, hiyo pesa uliyotoa ni kidogo mno kulinganisha na mchango wako kupitia makala na michango mbalimbali ya maandishi yako...

Mimi nimeshaanza muda mrefu kuchangia kwa kutuma hilo neno. Tatizo la mabenki yetu mengi ni foleni ndefu na muda mtu anaopoteza akisubiri huduma
 
Safi sana.
Napata moyo kama watu wanaweza kuchangia mageuzi ndani ya nchi yao wenyewe.
Nakupongeza sana Mwanakijiji,keep it up.
 
Kazi nzuri MMJ
Kati ya mawili "match mine or beat it" mimi nimeona nichague beat it!
Nitafanya kila niwezalo mpaka niwapenyezee Tsh 1 mil
 
Excellence is a habit! Hongera sana Mzee. Naona unaongezea pressure kupanda na kushuka.
 
Yap nimeshatuma several times,ila naona kama wanakata kidogo sana waweke namba nyingine ambayo tunaweza kuchangia angalao elfu 1000/=.
 
Asanteni WaTz KWA KUINGA MKONO chadema , Mwanakijiji asante sana mkuu.
Tunajitahidi kuhamasishana wenyewe kwa wenyewe, huku kanda ya ziwa kuna wadau wachache wanajitolea kutuwezesha katika siasa zetu za mageuzi, Tunawashukuru sana WaTz, sasa tumeamka, tuko mstari wa Mbele katika Ukombozi.
 
Mkuu kudos,

Watu huku tumekwisha anza kupambana nayo!!!

I will love to be part of changes!
 
ahsante mkuu MMJ nami nimechangia kupatia sms lakini kiwango kinachakatwa kidogo mno tutafutieni angalau cha elfu 2
 
Ni kweli, kwa wengine Tshs 350/= kwa sms moja ni ndogo sana.
ufanyike utaratibu wa kuweka namba za say, 1000/=; 2 000/=; 3000/= na 5 000/= ili kila mmoja aweze kuchangia kulingana na uwezo wake.
Wahusika pls do ze nidiful.
 
minakuuliza ni aje, mbona sisi wengine hatuna fursa ya kutuma new threads, au inakuaje tujuze kuna fees au ni mpaka muamue wenyewe? tafadhali nijulishe
 
Chadema mpo? Tunaomba muwe na namba mbali mbali ili tuweze kuchangia kiasi cha kutosha.. elfu, elfu mbili, elfu tano, elfu kumi na elfu hamsini. Tunaumia vidole kutuma kidogo kidogo
 
Huo ni mkakati mzuri na rahisi kwa watu wengi kuutekeleza. Nampongeza mtoa hoja Mzee Mwanakijiji. Lakini, pia kama huwezi kuchangia pesa, kwasababu za msingi kabisa, maombi ni muhimu kuliko hata pesa. Endeleeni kuombea uchaguzi huu uwe wa amani na pia watu wawe jasiri kupigia kura mtu mwenye sifa za kuongoza taifa hili kwa haki na hekima. Dr Slaa ameonesha sifa hizo. Chagua DR W. Slaa. Mungu atajibu maombi ya dhati kutoka kwa watu wote.
 
Ni kweli, kwa wengine Tshs 350/= kwa sms moja ni ndogo sana.
ufanyike utaratibu wa kuweka namba za say, 1000/=; 2 000/=; 3000/= na 5 000/= ili kila mmoja aweze kuchangia kulingana na uwezo wake.
Wahusika pls do ze nidiful.

Tuma kiwango chochote kile kupitia M-Pesa au ZAP Kwenyae namba alizotaja mwanakiji hapo juu au zilizopo kwenye kurasa za mbele za Tanzania Daima
 
Back
Top Bottom