Kwanini naamini CCM inaanguka rasmi?

Kwanini naamini CCM inaanguka rasmi?

Yericko Nyerere

JF-Expert Member
Joined
Dec 22, 2010
Posts
17,018
Reaction score
20,489
Siasa za Afrika ni mikingamo hasi, vivyo hivyo siasa za Tanzania ni silika ya mikingamo hiyo,

Huwa ni kawaida ya vyama vinapokaribia kudondoka kuifanyia madhila na anasa siasa. Wataua hata watu wanaowatawala, Hawawezi kutoka kirahisi kama watu wanavyofikiri,

Ccm haitatoka kwa sanduku la kura pekee, Utawala africa ni utajiri sio utumishi ndio maana wanatoa roho watu,

Ndio tujiandae ccm na serikali yake watachinja kabla ya kutoka, jambo mhimu ni kusubiri kiwango cha maafa ambayo katu hayaepukiki hata kwa tone la mchanga.

Lakini anguko la ccm li juu yao, maana alama za nyakati huwa hazipingani na binadamu wa nyama na damu.

Ukawa ni njia halisi ya Mtanzania kuikomboa nchi yake.

Nishauri tu kwa wakuu wa UKAWA, Ili tuitoe ccm 2015, technical team ya vyama vinavyounda ukawa, viwekwe pamoja vijifungie ndani na vipewe hadidu za rejea kuandaa mkakati wa mda mfupi kuelekea ukombozi 2015. Ni kazi ya mwezi mmoja tu!
 
Nakuunga mkono mkuu Yericko Nyerere

Baada ya mbinu zote kufeli sasa hivi wanamtumia Kibaraka wao Francis Mutungi ambaye ni Jaji Feki ili aitumie ofisi ya Msajili kuivuruga Chadema na Ukawa.
 
Last edited by a moderator:

Hata weza mkuu, wasajili waliopita walishindwa, yeye ni mchanga wa hila za kisiasa,
 
Last edited by a moderator:
mambo yote hapa duniani yapo kwa kusudi la MUNGU,hakuna utawala wowote ambao umejisimamisha wenyewe,na mwanadamu maisha yake yote yanaratibiwa na MUNGU. kwanini tusimuachie yeye yote? hao wanahitajika kutoka madarakini na wakati huo wengine wanataka kuingia madarakani,kwa nini wasisubirie wakati wao.kila jambo linawakati wake chini ya jua.wacha wakati ufike ingawa tunapitia magumu chini ya ccm lakin tumuachie MUNGU alie muamuzi wa yote.tufanye uwepo wa ccm ni kama wakati wa kulima, na wakati wa mavuno ukifikaa basi tutafuraia. tumtafute MUNGU ndugu nae MUNGU atatuonekania na kisha atatupa utawala bora. tusiutafute ubora wakati sisi sio bora.
 
Hilo nameliona mapema sana maana wapinzania watapigwa na kuumizwa sana
 
mamluki wakitolewa, maslahi binafsi yakawekwa pembeni, daftari jipya la wapiga kura, kujitokeza kupiga kura kwa wingi na KULINDA KURA..Yakifanyika haya CCM hawana chao.
 
Nakuunga mkono mkuu Yericko Nyerere

Baada ya mbinu zote kufeli sasa hivi wanamtumia Kibaraka wao Francis Mutungi ambaye ni Jaji Feki ili aitumie ofisi ya Msajili kuivuruga Chadema na Ukawa.

Jaji feki yupoje na orijino yupoje? kumbe nawewe Una poor reasoning kiasi hiki?
 
Last edited by a moderator:
Usijipe moyo kabisa ni vyema kuangalia kwa undani suala hili , ccm wana njama za aina tofauti kinyume na unavyowaza ni vyema ukaangalia historia ya ccm kwa upande wa Zanzibar ikitokea ishara ya kushindwa kwa aina yo yote ile kuna njama za kila aina ili wakae kwa nguvu madarakani , nahisi kuna hitajika nguvu za ziada na sio kama unavyowaza
 
mambo yote hapa duniani yapo kwa kusudi la MUNGU,hakuna utawala wowote ambao umejisimamisha wenyewe,na mwanadamu maisha yake yote yanaratibiwa na MUNGU. kwanini tusimuachie yeye yote? hao wanahitajika kutoka madarakini na wakati huo wengine wanataka kuingia madarakani,kwa nini wasisubirie wakati wao.kila jambo linawakati wake chini ya jua.wacha wakati ufike ingawa tunapitia magumu chini ya ccm lakin tumuachie MUNGU alie muamuzi wa yote.tufanye uwepo wa ccm ni kama wakati wa kulima, na wakati wa mavuno ukifikaa basi tutafuraia. tumtafute MUNGU ndugu nae MUNGU atatuonekania na kisha atatupa utawala bora. tusiutafute ubora wakati sisi sio bora.

Wakati ndio huu, wa miti kusema na mawe kujibu
 
Usijipe moyo kabisa ni vyema kuangalia kwa undani suala hili , ccm wana njama za aina tofauti kinyume na unavyowaza ni vyema ukaangalia historia ya ccm kwa upande wa Zanzibar ikitokea ishara ya kushindwa kwa aina yo yote ile kuna njama za kila aina ili wakae kwa nguvu madarakani , nahisi kuna hitajika nguvu za ziada na sio kama unavyowaza

Inawezekana umesoma haraka hara hii tafakuri, nimesema wazi ccm haitatoka kwa kura "tu",
 
Back
Top Bottom