Kwanini mzigo huu waliouanzisha wayahudi waachiwe waafrika?

Ebale

JF-Expert Member
Apr 20, 2016
943
1,682
Hili ni swali ambalo limekuwa likinitatiza sana! Zigo hili walilitengeneza wayahudi zaidi ya 2000 iliyopita, mara baada ya kulitengeneza wakalipeleka Italy wao wakaendelea na mfumo wao maisha wa kawaida. Waitalia wamehangaika mao sana wakisaidiana na wazungu wengine Ulaya na Marekani, walivyoona sio wakaja kuwabwagia waafrika ambao bado wanahangaika nao hadi leo! Wazungu na wanaisrsel wenyewe hawataki kuusikia mzigo huo! Swali kwanini waachiwe kuhangaika nao waafrika ambao kwa kudanganywa?
 
Binadamu akisha kuwa mwenye nguvu na afya tele anasahau aliko toka. Kama haumuamini Mungu basi usiamini pia kama kifo kipo halafu kwa imani hiyo hiyo usubirie uishi milele.

Imani leo ni zigo kwakua umepewa maisha na uwezo wa wewe kukosoa lkn kuna siku itakuja utataka kutengua kauli yako ukose nafasi hii. Punguza kufuru
 
Unaboa zigo gani sasa ushaambiwa jiwe walilokataa waashi ndilo limekuwa jiwe kuu la pembeni, na nabii hakubariki nyumbani kwao, unataka nini sasa, fanya kazi usawa wa jpm mgumu sana
Ukiwa fatilia vijana wa sasa wakienda shule kidogo tu wanajiona ndo wajuaji wa kila kitu na wapambanuaji wa mambo. ... Wamesahau kama tunaishi kwa neema tu
 
Hata waafrika pia wamelitua zigo.

Na ambao wamelibeba amma kulikumbatia wanafanya hivyo kwa ajiri ya kutafutia pesa.

Hakuna cha zaidi.
 
Ndugu Ebale, kamwe isitokee ukalewa uhai huu wa sekunde bilioni 2.2 tunazoishi hapa duniani; na hivyo ukajisahau na kuanza kukufuru!
Hata hivyo, miaka 2000 iliyopita Yesu Kristo alibeba mzigo mzito wa dhambi zako, ili baada ya uhai huu kukoma uwe miongoni mwa wale watakaoishi milele.
Uamuzi wa kukubli au kukataa ni wako wewe mwenyewe.
 
Ni kweli inashangaza sana. Ila hiyo ni 9. Kumi ni lile zigo lingine linaloamini kuua wengine utakwenda peponi. Halafu asiye wa imani yako basi sio ndugu yako. Mbaya zaidi waafrika wamepokea hata bila kuchuja, kibaya zaidi zigo hilo limefanya watu wawe wajinga hata kwenye uelewa wa mambo ya kawaida. Afadhali ya zigo lile lingine lilitia msisitizo wa elimu dunia na kila lilipopita watu walipata maendeleo kielimu tofauti na hili zigo lingine ambalo limefanya watu wadumae kiakili.
Nakumbuka miaka ya 90 kwenye mikusanyiko yao walikuwa wanahamasishana kuwa eti hawatendewi haki kwakuwa idadi yao kwenye vyuo vikuu ni ndogo sana kulinganisha na wenzao.

Kwa hiyo mleta mada upo sahihi kabisa
 
Huu ndiyo unafiki Mkubwa uliobebeshwa ujumuifu hasi.
Hata Africa wapo ambao hawaamini ulichotaka kukisema na siyo Wazungu tu.
 
Ndugu Ebale, kamwe isitokee ukalewa uhai huu wa sekunde bilioni 2.2 tunazoishi hapa duniani; na hivyo ukajisahau na kuanza kukufuru!
Hata hivyo, miaka 2000 iliyopita Yesu Kristo alibeba mzigo mzito wa dhambi zako, ili baada ya uhai huu kukoma uwe miongoni mwa wale watakaoishi milele.
Uamuzi wa kukubli au kukataa ni wako wewe mwenyewe.
Mkuu ila mleta mada hajataja kitu imani, kwanini wamlisha maneno?...pili Yesu alikufa miaka 2000 iliyopita, iweje useme ilikuwa kwajili ya kubeba dhambi za mleta mada ili hali wakati huo mleta mada hakuwa amezaliwa na kutenda hizo dhambi alizozifia Yesu?
 
Hili ni swali ambalo limekuwa likinitatiza sana! Zigo hili walilitengeneza wayahudi zaidi ya 2000 iliyopita, mara baada ya kulitengeneza wakalipeleka Italy wao wakaendelea na mfumo wao maisha wa kawaida. Waitalia wamehangaika mao sana wakisaidiana na wazungu wengine Ulaya na Marekani, walivyoona sio wakaja kuwabwagia waafrika ambao bado wanahangaika nao hadi leo! Wazungu na wanaisrsel wenyewe hawataki kuusikia mzigo huo! Swali kwanini waachiwe kuhangaika nao waafrika ambao kwa kudanganywa?
Mleta mada umekuwa creative sana....nadhani ile kauli ya kwamba Africa ni jalala ni kweli....taka nyingi sana kama vile hewa ukaa, bidhaa fake, pamoja na hii mizigo ya kizungu na kiarabu imekuwa ikitumpwa Africa....Mbaya zaidi waibebayo hawajui kama wanahangaika bure...kazi kushikilia na kutetea vitu visivyokuwepo.
 
Huyu sasa amekuwa Mzigo kwa jamii,mtu gani asiyefikiri hata mtu akifa nini hutoka na kuucha mwili kama Gogo? Kweli hili ni zigo kabisa.
 
Binadamu akisha kuwa mwenye nguvu na afya tele anasahau aliko toka. Kama haumuamini Mungu basi usiamini pia kama kifo kipo halafu kwa imani hiyo hiyo usubirie uishi milele.

Imani leo ni zigo kwakua umepewa maisha na uwezo wa wewe kukosoa lkn kuna siku itakuja utataka kutengua kauli yako ukose nafasi hii. Punguza kufuru
Umemjibu vizuri
 
Ndugu Ebale, kamwe isitokee ukalewa uhai huu wa sekunde bilioni 2.2 tunazoishi hapa duniani; na hivyo ukajisahau na kuanza kukufuru!
Hata hivyo, miaka 2000 iliyopita Yesu Kristo alibeba mzigo mzito wa dhambi zako, ili baada ya uhai huu kukoma uwe miongoni mwa wale watakaoishi milele.
Uamuzi wa kukubli au kukataa ni wako wewe mwenyewe.

Mkuu,mbona vitisho?

Alibeba mzigo mzito,nyie wanadamu mmepata wapi mizania ya kupima mzigo wa Yesu?Mbona wanadamu nyie ni wavumishi sana?

Tu-assume ni sawa,kabeba dhambi zangu,bado siku ya hukumu biblia yenu inadai nitahesabiwa mabaya yangu yote bila kuongeza wala kupunguza na nitachomwa moto sawa sawia,nikiwa sambamba na shetani wote tumehukumiwa ktk grupu moja!

Huo mzigo una-make sense kivipi hapa?Ni useless doctrine tu.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom