Kwanini mwanamke mpumbavu na sio mbanaume mpumbavu?

Wapi walisema Mungu ni mwanaume?
unazungumzia Biblia kumuita Mungu baba?

dini zingine hazisemi Mungu ni jinsia ipi
Waislam mfano.Mungu hajatambulishwa jinsia

Very simple.....Kuna baba wa kike?

Mtume ni jinsia gani?
 
Boss kwneye kitabu cha mwanzo mungu alisema na tuumbe mtunkwa mfano wetu "And God said, Let us make man in our image, after our likeness"mwanzo 1:26
Nazani apo utakuwa ushajua Mungu ni wa jinsia gani
 
Kwa nini kwenye Ukristu anatajwa? Au mungu baba haimaanishi yeye ni mwanaume?

Inawezekana ni 'language error'
usisahau mfano kwa kiswahili
unaweza sema 'Hapo kale alikuwepo Mungu,Mungu huyo akasema kwamba watu wawe hivi na vile'

halafu kwa kiingereza ikawa 'In the past there was God,and 'he' said people should'....

sasa umeona hapo?

hakuna anaejua kwa lugha ya mwanzo ya ki hebrew kama mungu alitajwa kama baba for sue
au translation?
 
Naomba nikumbushie wanawake wa shoka, NEVER SEEN!!!
1. Easther apana chezea myahudi mwenyewe alisalimu!,
2. Delila ni noma mpaka Samsoni kamuasi mola!,
3.Rahabu nae mjeda kajipoteza,
4.Maria Magdalena nae hapana chezea,
5. Mke mwingine wa Daudi mumewe aliepangwa Warfront
ngoja niishie hapo tu katika kukumbuka maandiko! Kifupi mwanamke ukielewa your powers you can conquer the world!!!!!
 
Inawezekana ni 'language error'
usisahau mfano kwa kiswahili
unaweza sema 'Hapo kale alikuwepo Mungu,Mungu huyo akasema kwamba watu wawe hivi na vile'

halafu kwa kiingereza ikawa 'In the past there was God,and 'he' said people should'....

'In the past there was god. That god said people should be like this and like that'. Hapo sijatumia pronoun ya 'He' na maana imebaki pale pale. Sasa kwa nini wao watumie hiyo pronoun?

sasa umeona hapo?

Wewe umeona jinsi nilivyoiunda sentensi bila kutumia hiyo pronoun?

hakuna anaejua kwa lugha ya mwanzo ya ki hebrew kama mungu alitajwa kama baba for sue
au translation?

Hahahaha....kama hakuna anaejua kwa lugha ya mwanzo ya Kiibrania kama mungu alitajwa kama baba au la, kwa msingi huo huo basi hakuna anaejua chochote kuhusu mungu maana yote yanaweza yakawa yalipotea katika tafsiri.
 
Its a kind of philosophy...kuna wanaoamini hivyo na wasioamini hivyo! na mara nyingi hivi vitu hufuatana na mazingira...mfano sasa hivi mfumo dume unapigwa vita halii itafikia kwenye climax then itaingia katika hali nyingine! but mwisho wa siku uhalisia aliouweka Mungu utaendelea kubaki pale pale! ngona nikupe mfano mwingine, sasa hivi miongoni mwa nchi zilizokua zinafanya Campaign ya kutahiri wanaume zimeanza kupiga vita hiyo hali (kama mwanamke atakiwi kufanyiwa hivyo iweje mwanaume?)
 
Naomba nikumbushie wanawake wa shoka, NEVER SEEN!!!
1. Easther apana chezea myahudi mwenyewe alisalimu!,
2. Delila ni noma mpaka Samsoni kamuasi mola!,
3.Rahabu nae mjeda kajipoteza,
4.Maria Magdalena nae hapana chezea,
5. Mke mwingine wa Daudi mumewe aliepangwa Warfront
ngoja niishie hapo tu katika kukumbuka maandiko! Kifupi mwanamke ukielewa your powers you can conquer the world!!!!!

Maria magdelena alifanya nini?
 
Hayo ni maandiko kutoka vitabu vitakatifu na wala si kwamba maneno hayo yanmetungwan a wanaume!
hutakiwi kuhoji maandiko are u there?
 
Vipi Boss,mbona siku hizi majukumu hayaeleweki.

Wanaume tunajenga a house
wanawake wanajenga a home....

sasa hapa kinachozungumziwa ni a home

mwanamke mpumbavu atabomoa a home yake mwenyewe badala ya kuijenga....

nafikiri ishu ni tafsiri .....ukielewa utagundua wanawake wamepewa umuhimu na sifa kuwa
wao ndio wajenzi wa a home na wapumbavu baadhi yao hubomoa na sio kujenga.....
 
mwanamke mpumbavu huibomoa nyumba yake mwenyewe, mwanaume mpumbavu huibomoa ndoa yake mwenyewe, Wanawake wamekua regarded as kiumbe dhaifu na asiye na maamuzi binafsi, which is very wrong wanatumia tu QUOTATION za ki biblia bt in a real sense pia mwanaume ni muharibifu mkubwa wa nyumba......................
 
Wapendwa, kuna msemo mmoja maarufu sana unasema hivi,

"...Mwanamke mpumbavu huvunja ndoa yake kwa mikono yake mwenyewe..."

Hivi kwanini ni mwanake na sio mwanaume? kwani haiwezekani mwanaume mpumbavu akavunja ndoa yake kwa mikono yake mwenyewe?

Ni mwendelezo wa kutomwamini na kumdharau mwanamke au?

Ni maneno ya MUNGU kutoka katika Bible takatifu....!!
Sasa kama unapingana na maneno ya MUNGU hayaaa weeee!!
Mfano wa wanawake wapumbavu ni huu hapa!!
Hawa...
Delila..
e.t.c
 
Kitabu cha Mithali 4:1 inasema..."Kila mwanamke aliye na hekima hujenga nyumba yake, Bali aliye mpumbavu huibomoa kwa mikono yake mwenyewe".

Hapa sielewi tatizo linatoka wapi. Mimi nilidhani wanawake wangefurahi na kuona wamepewa heshima kubwa kwa tafsiri yangu; kwani hapa Neno hili linaonyesha kwamba Mungu amempa mamlaka makubwa sana mwanamke katika nyumba kuliko mwanaume. Mwanamke amepewa uwezo wa kujenga au kubomoa nyumba. Hakuna mahali kwenye Biblia yote mwanaume amepewa mamlaka haya makubwa namna hii. Kwa nini mnaegemea tu huo upande mbaya lakini huu upande wa mamlaka hamuutazami?

Hebu tutazame tu katika mtazamo wa kawaida na wa kweli, ni nani kwa sehemu kubwa anabeba uzito wa nyumba zetu, kutunza familia, kuweka mazingira ya nyumba kuwa safi na salama, furaha ya nyumba n.k. jibu la wazi ni mwanamke. Hata kama ungetunga sheria ya kunyima huyu mwanamke asifanye hizo kazi automatically atajikuta anafanya tu; kwa nini ? ndivyo Mungu alivyowaumba kwamba wawe na huruma, upendo na wapende amani.

Hivyo mwanamke mwenye hekima anatamani nyumba yake iwe na furaha, upendo na amani. Ni wanawake wachache sana wanaopenda nyumba zisizo na amani, na hili wanaliweza kutokana na moyo wa uvumilivu walio nao. Wanaume ni rahisi sana kugive-up lakini sivyo kwa wanawake. Hebu fikiri wanaume wangepewa mamlaka hayo ya kujenga na kubomoa ni ndoa ngapi leo zingekuwepo? Hebu niwaulize wanaume jambo fulani; mara ngapi wanaume wanafumaniwa kwamba wametembea na wanawake wengine huko nje. Ni nini kinatokeaaa?????????? Wanawake wanasamehe na ndoa inaendelea tena wanawake wanaficha hiyo inakuwa ni siri ya ndani. Je mwanaume akimfumania mke wake amatembea au hata kuhisia inakuwaje??????????????? ndoa huwa inaendelea??????????????????? kwa nini?????????? UVUMILIVU.

Hivyo wanawake jivunieni mamlaka haya ni neema ya Mungu na ni baraka na ndio sababu Neno la Mungu limesema "MWANAMKE MWENYE HEKIMA" sio kila mwanamke, wapumbavu ndio wanabomoa nyumba zao kwa kushindana na mwanaume.
 
Wapendwa, kuna msemo mmoja maarufu sana unasema hivi,

"...Mwanamke mpumbavu huvunja ndoa yake kwa mikono yake mwenyewe..."

Hivi kwanini ni mwanake na sio mwanaume? kwani haiwezekani mwanaume mpumbavu akavunja ndoa yake kwa mikono yake mwenyewe?

Ni mwendelezo wa kutomwamini na kumdharau mwanamke au?
Ndugu hiyo ni sehemu ya pili ya aya kakika Biblia Takatifu (Mithali 14:1).
 
Biblia iliandikwa first kwa lugha ya ki hebrew...
halafu ikatafsiriwa ki latini
halafu kiingereza
hadi ifike kiswahili......haiwezi kuwa the same thing
kuna vitu vimepotea due to translations zoote hizo

Kaka kwa hiyo unamaanisha tusiiamini kwa % zote?
 
Wapi walisema Mungu ni mwanaume?
unazungumzia Biblia kumuita Mungu baba?

dini zingine hazisemi Mungu ni jinsia ipi
Waislam mfano.Mungu hajatambulishwa jinsia

Wewe hujui Mungu anaitwa Baba Mungu na haitwi mama Mungu? So baba ni KE au ME?
 
Back
Top Bottom